Tafuta

Ghana: Mapadre na Watawa wa Jimbo Jipya la Donkorkrom. Ghana: Mapadre na Watawa wa Jimbo Jipya la Donkorkrom.  (© Sr. Sylvie Lum Cho, MSHR)

Jimbo Jipya la Donkorkrom (Ghana) na Askofu wake wa kwanza

Papa ameinua Vikarieti ya Kitume ya Donkorkrom nchini Ghana,kuwa Jimbo na kumteua Askofu mpya wa Kwanza wa Jimbo hilo,Mhesh.Padre John Alphonse Asiedu, SVD,.

Vatican News

Baba Mtakatifu Leo XIV, Jumanne tarehe 12 Mei 2026, ameipatia wadhifa Vikarieti ya Kitume ya Donkorkrom, nchini Ghana, kuwa Jimbo jipya, lenye jina moja na mpangilio wa kieneo, kuwa  Jimbo, kutoka katika jimbo kuu la jiji la Accra. Na wakati huo huo Baba Mtakatifu amemteua Mheshimiwa Padre John Alphonse Asiedu, SVD, ambaye hadi uteuzi  alikuwa msimamizi wa Kitume wa Donkorkrom, kama Askofu wa kwanza wa Jimbo la Donkorkrom, Ghana.

Jimbo la Donkorkrom

Jimbo Jipya la  Donkorkrom liko mashariki mwa Ghana. Linashughulikia eneo la kilomita za mraba 5,040 na lina idadi ya watu 228,754, ambapo 37,462 ni Wakatoliki. Jimbo hilo lina Parokia 9, taasisi katoliki  14 za elimu, na mashirika 3 ya upendo. Kuna mapadre 14 wa jimbo, Mapadre 8 watawa na masista 22 wa mashirika mbali mbali; kuna waseminari 2.

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.

 

13 Mei 2026, 09:05