Tafuta

2026.05.25 Waraka wa Papa Leo XIV wa "Magnifica Humanitas" 2026.05.25 Waraka wa Papa Leo XIV wa "Magnifica Humanitas"  (@Vatican Media)

Magnifica Humanitas:simu kati ya Papa na Waziri mkuu Carney,wa Canada

Baba Mtakatifu Leo XIV,Mei 29 alizungumza kwa simu na Waziri Mkuu wa Nchi ya Amerika Kaskazini yaliyolenga mada za Waraka uliochapishwa hivi karibuni,lakini pia kuhusu kujitolea kwa ajili amani kati ya watu,hasa katika Mashariki ya Kati na Ukraine na kuhusu masuala yenye maslahi ya pamoja.

Vatican News

Mazungumzo ya simu kati ya Papa Leo XIV na Mark Carney, Waziri Mkuu wa Canada, yalifanyika alasiri tarehe 29 Mei 2026 katika fursa ya  kuchapishwa kwa waraka wake wa Kwanza wa Kitume wa Magnifica Humanitas hivi karibuni tarehe 25 Mei 2026. Katika taarifa kutoka Ofisi ya Vyombo vya Habari ya Vatican iliripoti kwamba umuhimu wa kujadili maendeleo ya akili unde kutoka katika mtazamo wa kimaadili na mbinu inayozingatia binadamu ilijadiliwa. Mazungumzo yaliendelea, huku yakizingatia masuala ya maslahi ya pande zote katika ngazi za kikanda na kimataifa, hasa kwa kuzingatia kujitolea kwa ajili ya amani miongoni mwa watu, hasa katika Mashariki ya Kati na Ukraine.

Mkutano mwishoni mwa Misa ya kuadhimisha kuapishwa kwa upapa wake

Ikumbukwe Waziri Mkuu wa Canada Carney alikutana na Papa Leo XIV mjini  Vatican mnamo tarehe 18 Mei 2025, katika fursa ya kuadhimisha Misa ya kuanza kwa upapa wake. Bwana Carney, niMkatoliki anayefanya kazi na alikuwa amesafiri kuja Roma na familia yake.  Bwana Carney, mwenye umri wa miaka 61, amekuwa Waziri Mkuu tang Machi 2025. Ni mchumi, mwanabenki, meneja, na mwanasiasa, kiongozi wa Chama cha Liberal cha Canada, ambaye anafamilia ya mke Diane na  watoto wanne.

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.

29 Mei 2026, 19:30