Tafuta

Hospitali ya Faraja ya Padre Pio huko San Giovanni Rotondo. Hospitali ya Faraja ya Padre Pio huko San Giovanni Rotondo.  (Michele Martino)

Papa aanzisha Tume ya kuzindua upya"Nyumba ya Mateso ya Padre Pio"

Katika maandishi ya mkono wake Papa Leo XIV ameanzisha Tume mpya ya uongozi wa kuzindua upya Mfuko wa upendo ulioanzishwa na Mtakatifu Pio wa Pietrelcina.Tume mpya itaongozwa na Mkuu wa Sekretarieti ya Uchumi,Vatican Dk.Maximino Caballero Ledo,kuratibiwa na Katibu wa APSA Fabio Gasperini.Wajumbe wengine ni pamoja na Askofu MkuuPaolo Rudelli,Naibu Katibu wa Vatican,Giordano Piccinotti,Rais wa APSA na Giorgio Ferretti,Askofu Mkuu wa Foggia-Bovino.

Vatican News

Casa Sollievo della Sofferenza, yaani ni Nyumba ya Faraja ya Mateso ni Kotu  kikuu cha kiafya kilichozaliwa kutokana na ndoto ya Mtakatifu Padre Pio wa Pietrelcina huko San Giovanni Rotondo kinajiandaa kuanza enzi mpya ya ufufuaji. Hii ni kwa sababu Papa Leo XIV alitia saini barua ya mkono wake (chirograph) ambayo  inayoanzisha Tume ya kuiongoza na kuisimamia Mfuko wake wenye mamlaka ya kutambua suluhisho bora za kuimarisha ufanisi, ubora, na uendelevu wake baada ya muda. Uamuzi huu unatokana na upendo wa Kiti Kitakatifu cha  Kitume kwa kazi za upendo  na ufahamu kwamba taasisi kubwa, ili kubaki waaminifu kwa dhamira yao, lazima ziweze kukabiliana na changamoto za mabadiliko.

"Mageuzi ya nyakati, teknolojia, sheria, na uchumi," maadhishi ya Papa yanasema "yanaweka utume wa Kanisa mbele ya changamoto ya uboreshaji endelevu," hasa katika sekta za afya zinazohitaji maono, uwekezaji, na usimamizi wa busara. Miongoni mwa taasisi hizi ni Casa Sollievo della Sofferenza, iliyoanzishwa "kwa lengo la kutoa ukarimu, msaada, na utunzaji kwa wagonjwa, mahujaji, na familia zao, ikichota msukumo kutoka kwa hali ya kiroho na sura ya mwanzilishi wake Mtakatifu."

Ili "kukabiliana na changamoto hii," Papa Leo XIV ameamua kuanzisha "Tume ya Uongozi na Usimamizi kwa ajili ya 'Casa Sollievo della Sofferenza – Opera di San Pio da Pietrelcina, O.F.M. Cap.' Foundation,  yaani  ‘Nyumba ya Faraja ya Mateso- Mfuko wa kazi  ya Mtakatifu Pio wa Pietralcina,OFM Cap ) yenye jukumu la kuchambua hali ya sasa ya Mfuko huo, kutambua suluhisho bora za kuongeza ufanisi, ubora, na uendelevu wa muda mrefu wa kazi na dhamira yake, na kutekeleza suluhisho zilizotambuliwa."

Tume itafanya kazi katika nyanja zote: za kifedha  na kiutendaji, kwa uwezo kamili wa kutekeleza vitendo muhimu vya kawaida na vya ajabu vya kiutawala, ikiripoti moja kwa moja kwa Papa kabla ya uamuzi wowote muhimu na kwa vyovyote vile kabla ya kupitisha vitendo muhimu au vyenye athari kubwa na muhimu kwa mali za Mfuko  au kurekebisha Sheria yake.” Papa Leo XIV kwa kufanya hivyo alimteua Dkt. Maximino Caballero Ledo kama Rais wa Tume hiyo, na Dkt. Fabio Gasperini na wajumbe wengine: Askofu Mkuu Paolo Rudelli, Askofu Mkuu Giordano Piccinotti, Askofu Giorgio Ferretti,” na kuteuliwa katika Kamati ya Ufundi:  “Dk. Benjamin Estévez de Comes, Dkt. Gino Gumirato, na Wakili Alessandro Ela Oyana.”

Ikumbukwe  Casa Sollievo, yaani,  Nyumba ya Faraja ilizaliwa kutokana na imani thabiti ya Padre Pio, ambaye aliamini kwamba kutunza mwili ilikuwa sehemu muhimu ya utume wa  Kikristo. Leo hii, miongo kadhaa baadaye, hisia hiyo bado haijabadilika. Katika maadhimishi ya mkono ya Papa  Leo XIV, inabanisha kuwa “ ni ishara ya utunzaji: Utunzaji uleule ambao mtakatifu wa Pietrelcina aliutumia ulihakikisha kwamba hakuna mgonjwa, mhujaji, au mwanafamilia atakayeachwa bila kukaribishwa na kusaidiwa.” Kwa hivyo, uzinduzi mpya wa Casa Sollievo “ni kitendo cha uaminifu kwa mwanzilishi, kwa utume wa taasisi hiyo, na kwa wale wote wanaopita milango yake kila siku wakitafuta uponyaji na matumaini.”

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.

 

27 Mei 2026, 17:10