Tafuta

2026.05.25 Papa alikutana na Rais Bajram Begaj, wa Jamhuri ya Albania. 2026.05.25 Papa alikutana na Rais Bajram Begaj, wa Jamhuri ya Albania.  (@VATICAN MEDIA)

Papa akutana na Rais wa Albania

Baba Mtakatifu Leo XIV, amekutana katika Jumba la Kitume mjini Vatican na Bajram Begaj,rais wa Jamhuri ya Albaia na baadaye kisha akafanya majadiliano katika Sekretarieti ya Vatican yaliyolenga masuala ya kimataifa,hasa kwa kuzingatia Balkani za Magharibi na mchakato wa kujiunga na Umoja wa Ulaya.

Vatican News

Baba Mtakatifu Leo XIV, Jumatatu asubuhi tarehe 25 Mei 2026 alikutana na Bajram Begaj, Rais wa Jamhuri ya Albania, katika jengo la kitume na ambaye baadaye alikutana na Kardinali Pietro Parolin, Katibu Mkuu wa Vatican akiambatana na  Askofu Paul Richard Gallagher, Katibu wa Vatican Mahusiano na Mataifa na Mashirika ya Kimataifa 

Majadiliano katika Sekretarieti ya Vatican.

Kama ilivyoelezwa katika taarifa kutoka Ofisi ya Vyombo vya Habari ya Vatican, "Wakati wa majadiliano ya kirafiki katika Sekretarieti ya Vatican, shukrani zilitolewa kwa uhusiano mzuri wa pande mbili na nia ya kuendeleza ushirikiano katika maeneo yenye maslahi ya pande zote." "Wakati wa mazungumzo," taarifa inaendelea kuwa "masuala mbalimbali ya kimataifa yalijadiliwa, kwa kuzingatia hasa eneo la Magharibi mwa Balkani na mchakato wake wa kujiunga na Umoja wa Ulaya.

Papa akutana na Rais wa Albania

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.

 

25 Mei 2026, 11:49