Tafuta

Askofu Msaidizi Simon Peter Kamomoe ameteuliwa kuliongoza Jimbo la Wote nchini Kenya ambaye hadi uteuzi alikuwa msimamizi wa Kitume. Askofu Msaidizi Simon Peter Kamomoe ameteuliwa kuliongoza Jimbo la Wote nchini Kenya ambaye hadi uteuzi alikuwa msimamizi wa Kitume. 

Papa amteua Askofu Kamomoe kuwa Askofu wa Jimbo la Wote,Kenya

Papa amemteua Askofu wa Jimbo la Wote chini Kenya Askofu Simon Peter Kamomoe,ambaye hadi uteuzi alikuwa anahudumu kama Askofu Msaidizi na Msimamizi wa Kitume wa kiti kilicho wazi cha kiti hicho hicho.

Vatican News

Baba Mtakatifu Leo XIV tarehe 13 Mei 2026, amemteua Askofu wa Jimbo la Wote nchini Kenya, Mwashamu Askofu Simon Peter Kamomoe, ambaye hadi uteuzi huo alikuwa Askofu Msaidizi na Msimamizi wa Kitume wa Jimbo hilo ambalo lilikuwa wazi.

Wasifu wake

Askofu Simon Peter Kamomoe alizaliwa tarehe 26 Novemba 1962 huko Gatundu ,Wilaya ya Kiambu, Jimbo Kuu la Nairobi, Kenya na kupewa daraja la upadre kunako tarehe 18 Juni 1994. Baba Francisko, alikuwa amemteua  kuwa Askofu wa Kiti cha Tubune ya Numidia na Msaidizi wa  Jimbo Kuu la Nairobi, tarehe  13 Februari  2024, na kuwekwa wakfu wa kiaskofu tarehe 6 Aprili 2024. Na kisha tarehe 5 Julai 2025,  Baba Mtakatifu Leo XIV akamteua kuwa Msimamizi wa Kitume wa Jimbo la Wote, nchini Kenya.

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.

 

 

13 Mei 2026, 18:23