Papa atoa wito wa maadili ya mshikamano na nia ya kusikiliza kwa taasisi za benki
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Leo XIV alikutana na Wakuu na wafanyakazi wa benki kadhaa za Italia Jumamosi tarehe 16 Mei 2026 mjini Vatican katika Ukumbi wa Clementine wa Jumba la Kitume. Katika hotuba yake alitafakari juu ya jukumu la benki na taasisi za mikopo katika jamii. Kwa kuanzishwa ili kuunga mkono ujasiriamali na fedha za umma na za kibinafsi kwa nyakati tofauti na katika miktadha mbalimbali, taasisi za benki, kwa karne nyingi, zimekuwa kitovu cha michakato mikubwa ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii na zimekuwa ukweli unaozidi kuwa mgumu na wenye pande nyingi, unaoweza kuathiri maisha ya watu,”Papa alibainisha.
Nyuma ya namna kuna nyuso za binadamu
Kiukweli, Papa Leo XIV alisema kuwa mkusanyiko wa mtaji na upatikanaji wa ujuzi uliohitimu umeupatia mfumo wa benki rasilimali kubwa za kiuchumi, na kuuwezesha, kwa njia chanya, kukuza ugawanaji sawa kwa ustawi wa jumla na, kinyume chake, kuwa mhamasishaji wa mkusanyiko wa ubinafsi, chanzo cha ukosefu wa usawa na umaskini. Lakini katika benki, sio mtaji unaoingia katika uchambuzi wa awali, bali ni watu, Papa alisisitiza, akikumbuka kwamba nyuma ya namba hiyo kuna wanawake na wanaume, na familia zinazohitaji msaada. Na hivyo, katika ulimwengu wa leo, ambapo kiwango cha juu cha kompyuta kinalazimisha upatanishi unaozidi kuwa wa kina na mashine katika mahusiano ya kibinadamu, umakini wa kibinadamu ni muhimu katika benki.
"Mnaitwa kuhakikisha kwamba wale wanaopata huduma zenu hawajisikii wameachwa na ubaridi wa mifumo ya algoriti, hata iwe na ufanisi na usahihi wa hisabati, lakini kwamba nyuma ya zana za kiufundi wanazoona, leo kama ilivyokuwa zamani, na uwepo wa watu walio tayari kusikiliza na wenye hamu ya kufanya mema. “Kipengele kingine cha msingi cha shughuli za benki Papa Leo XIV alisema ni ushawishi wao mkubwa katika mageuzi ya kimuundo ya jamii na maendeleo yake ya kitamaduni. Kiasi kikubwa cha mtaji, uwekezaji, na maamuzi ya kiuchumi lazima yachukuliwe kama vyombo kwa manufaa ya ubinadamu.
Mu awe katikati kila wakati
Papa Leo XIV alisema kuwa uwepo wao ni wa thamani kwa sababu ya kuwakumbusha wale ambao kwa urahisi huangukia kwenye maadili ya kimwili, na kutatanisha malengo na njia maishani, kwamba hata katika kiwango cha kifedha, mtu lazima awe katikati kila wakati, na kwamba juu ya nguzo hiyo lazima kujengwe miundo mbadala ya kijamii tunayohitaji. Ahadi ya benki ni hai na inafaa, Papa Leo XIV alibainisha, ikithibitishwa na mipango yao mingi ya kibinadamu na kiutamaduni. Hivyo basi kutiwa moyo kuendelea kufanya kazi, kudumisha wito wao kama taasisi za usaidizi wa pande zote na kuelekeza ahadi yao kuelekea maadili ya mshikamano.
Mwanzo wa Benki kuonesha ujasiri na ubunifu
Akifuatilia historia ya benki na vyama vya mikopo, Askofu wa Roma kisha alikumbuka mwanzo, ambao uliooneshwa kwa ujasiri na ubunifu, unashuhudia ulinganifu kati ya akiba na uwekezaji, wa kibinafsi na wa umma, kwa ajili ya utambuzi wa manufaa ya pamoja na kwa ukuaji imara wa uchumi. Pia aliakisi jukumu la waendeshaji wa fedha. Papa alisema kuwa "Wale wanaohusika katika soko la fedha wanaweza kufanya mema si tu kwa kutenda ipasavyo, bali pia kwa kuwafahamisha na kuwafunza watu na mazingira wanayofanyia kazi ili kutumia rasilimali kwa busara na ipasavyo kimaadili, wakichanganya usikivu, akili, uaminifu, na upendo, na kwa kukuza 'vigezo vya kibinadamu [...] ambapo faida na mshikamano havipingani tena.'"
Utume uliokabidhiwa na Mungu
Papa Leo XIV asisitiza kwamba, taasisi za fedha, kwa njia mbalimbali, zimependelea ushirikiano wa haki na ugawaji upya wa utajiri miongoni mwa watu binafsi, biashara, na taasisi, na kufanya matumizi yake kupatikana kwa wote na kuthamini mchango wa kila mmoja. Hii ni "kazi ya kijamii inayoendana vyema na utume uliokabidhiwa na Mungu kwa wanadamu kuwa mlinzi wa uumbaji," Papa aliema, ambayo lazima iongoze "kila shughuli ya mwanadamu" ili kuzaa matunda, kwa kutumia "kwa ukarimu na haki zawadi ambazo Mungu awali aliziweka kwa wote na kukuza kwa uaminifu mbegu hizo za wema zilizoandikwa, kama ahadi ya kuzaa matunda, katika Uumbaji wote." Kwa upande wa Baba Mtakatifu Leo XIV alizihimiza taasisi za benki kubaki aminifu kwa asili zao, na pendekezo la mwisho: Msisahau kamwe upendo; badala yake, muufanye uwe kigezo kinachoongoza zaidi cha chaguo zenu za kiprogramu."
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.
