Tafuta

Maadhimisho ya Jubilei ya Miaka 100 tangu kutangazwa “Nuestra Señora del Sagrario” yaani “Mama Yesu wa Tabernakulo” Maadhimisho ya Jubilei ya Miaka 100 tangu kutangazwa “Nuestra Señora del Sagrario” yaani “Mama Yesu wa Tabernakulo”  

Papa Leo XIV Jubilei ya Miaka 100 ya B. Maria Mama Yetu wa Tabernakulo, Toledo

Papa Leo XIV anataja sifa kuu za Kanisa hili ambalo ni la kwanza kujengwa: ni Hekalu la Jimbo kuu la Toledo, ukumbusho wa uchaji wa Mungu na ukarimu kwa watu wa Zama za Kati, baada ya Jiji hili kupata uhuru wa kuabudu na Mababu wakatia nia ya kujenga Kanisa hili kuu na kubwa, zote hizi ni sifa ambazo zimelipamba Kanisa hili ambalo lina umri wa miaka 800 tanu kujengwa kwake. Ni Kanisa ambalo limepata msukumo mkubwa na wenye utukufu tangu mwanzo wake.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Leo XIV amemtea Askofu mkuu Alejandro Arellano Cedillo, Dekano wa Mahakama Kuu ya Rufaa ya Kipapa “Rota Romana”, kuwa ni Mjumbe na Mwakilishi wake katika Maadhimisho ya Jubilei ya Miaka 100 tangu kutangazwa “Nuestra Señora del Sagrario” yaani “Mama Yesu wa Tabernakulo” kuwa ni Msimamizi, Mlinzi na Mwombezi wa Jimbo kuu la Toledo, nchini Hispania na kilele cha maadhimisho haya ni tarehe 30 Mei 2026. Katika msafara huu, Askofu mkuu Alejandro Arellano Cedillo anaambatana na: Monsinyo Raul Muelas Jimenez, Makamu Askofu, Jimbo kuu la Toledo pamoja na Padre Juan Pedro Sanchez Gamero, Dekano wa Jimbo kuu la Toledo!

Bikira Maria Mama Yetu wa Tabernakulo
Bikira Maria Mama Yetu wa Tabernakulo

Baba Mtakatifu Leo XIV anataja sifa kuu za Kanisa hili ambalo ni la kwanza kujengwa nchini Hispania, ni Hekalu la Jimbo kuu la Toledo, kielelezo na ukumbusho wa uchaji wa Mungu na ukarimu kwa watu wa Zama za Kati, baada ya Jiji hili kupata uhuru wa kuabudu na Mababu wakatia nia ya kujenga Kanisa hili kuu na kubwa, zote hizi ni sifa ambazo zimelipamba Kanisa hili ambalo lina umri wa miaka 800 tanu kujengwa kwake. Ni Kanisa ambalo limepata msukumo mkubwa na wenye utukufu tangu kuanza kwa ujenzi wake na uzuri wake umeendelea kutamalaki pasi na mfano. Huu ni mchango mkubwa uliotolewa na Mtakatifu Hildephon, Askofu wa Toledo, mrithi wa ulinzi wa Bikira  Maria Mtakatifu wa Madhabahu haya na kwamba, Sanamu ya Bikira Maria wa Madhabahu haya, miaka mia moja iliyopita ilivikwa Taji la Dhahabu safi.

Askofu mkuu Cedillo ameteuliwa kuwa mwakilishi wa Papa Toledo
Askofu mkuu Cedillo ameteuliwa kuwa mwakilishi wa Papa Toledo   (@Vatican Media)

Sanamu hii inaheshimiwa sana na watu wa Mungu ndani na nje ya Jimbo kuu la Toledo. Maadhimisho haya yamepewa uzito wa pekee, ili kuweza kumshukuru na kumshangalia Bikira Maria, ili aendelee kuchochea karama, toba, wongofu wa ndani sanjari na waamini kujikita na kuambata utakatifu wa maisha. Mjumbe wa Baba Mtakatifu atashiriki maandamano makubwa kama sehemu ya maadhimisho ya Sherehe hizi. Askofu mkuu Alejandro Arellano Cedillo, Dekano wa Mahakama Kuu ya Rufaa ya Kipapa “Rota Romana”, ni Mwenyeji wa Jimbo kuu la Toledo, na kwamba, ni mshiriki mwaminifu na wa upendo katika huduma ya haki na ukweli, kumbe hii ni fursa kwake, kuyapamba Maadhimisho ya Jubilei ya Miaka 100 tangu Bikira Maria alipovikwa taji la Dhahabu kwa kupokea roho mpya kwa ukuaji na ukuzaji sahihi wa imani, amana na urithi mkubwa kutoka kwa Mababu zao wa imani, wawe ni mifano bora ya kuigwa katika maisha yao.

Jubilei ya Miaka 100 tangu Bikira Maria Mama wa Tabernakulo avishwe Taji
Jubilei ya Miaka 100 tangu Bikira Maria Mama wa Tabernakulo avishwe Taji   (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Mwishoni, Baba Mtakatifu Leo XIV anamwomba Askofu mkuu Alejandro Arellano Cedillo, Dekano wa Mahakama Kuu ya Rufaa ya Kipapa “Rota Romana”, kumfikishia salam na matashi mema kwa watu wote wa Mungu Jimbo kuu la Toledo, ili wote hawa wapate heri na baraka kwa maombezi ya “Nuestra Señora del Sagrario.” Yaani Bikira Maria wa Tabernakulo. Mwenyezi Mungu apende kuwashushia zawadi za mbinguni pamoja na ushuhuda wa fadhili za Kibaba kutoka kwa Papa Leo XIV kwa wale wote watakaoshiriki katika maadhimisho haya mazito!

Jimbo kuu la Toledo
26 Mei 2026, 15:12