Tafuta

Waraka wa kwanza wa Kitume wa Baba Mtakatifu Leo XIV unajulikana kwa Lugha ya Kilatini kama: “Magnifica humanitas” yaani:"Utu wa Kupendeza" Juu ya Hifadhi ya Mwanadamu Katika Enzi ya Teknolojia ya Akili Unde” Waraka wa kwanza wa Kitume wa Baba Mtakatifu Leo XIV unajulikana kwa Lugha ya Kilatini kama: “Magnifica humanitas” yaani:"Utu wa Kupendeza" Juu ya Hifadhi ya Mwanadamu Katika Enzi ya Teknolojia ya Akili Unde”  (@Vatican Media)

Papa Leo XIV Waraka wa Kitume "Magnifica humanitas": Utu wa kupendeza

Waraka wa kwanza wa Kitume wa Papa Leo XIV: “Magnifica humanitas” yaani: “Ubinadamu wa ajabu" Juu ya Hifadhi ya Mwanadamu Katika Enzi ya Teknolojia ya Akili Unde” umetiwa mkwaju, tarehe 15 Mei 2026, kama sehemu ya kumbukizi ya Miaka 135 tangu Papa Leo XIII alipochapisha Waraka wake wa Kitume “Rerum Novarum” yaani “Mambo Mapya” msingi wa Mafundisho Jamii ya Kanisa kunako tarehe 15 Mei 1891. Alisema, kazi ni utimilifu wa utu na heshima ya binadamu.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Waraka wa kwanza wa Kitume wa Baba Mtakatifu Leo XIV: “Magnifica humanitas” yaani: “Utu wa kupendeza" Juu ya Hifadhi ya Mwanadamu Katika Enzi ya Teknolojia ya Akili Unde” umetiwa mkwaju, tarehe 15 Mei 2026, kama sehemu ya kumbukizi ya Miaka 135 tangu Papa Leo XIII alipochapisha Waraka wake wa Kitume “Rerum Novarum” yaani “Mambo Mapya” msingi wa Mafundisho Jamii ya Kanisa kunako tarehe 15 Mei 1891 na alisema, kazi ni utimilifu wa utu na heshima ya binadamu, ina thamani na heshima yake ya asili. Aligusia kuhusu haki msingi za wafanyakazi, mshahara na wajibu wa wafanyakazi; Umiliki wa binafsi wa mali; wajibu wa Serikali, sanjari na kuwalinda wanyonge ndani ya jamii; Ustawi, maendeleo na mafao ya wengi.

Waraka wa kwanza wa Kitume wa Papa Leo XIV "Magnifica humanitas"
Waraka wa kwanza wa Kitume wa Papa Leo XIV "Magnifica humanitas"   (@Vatican Media)

Waraka wa kwanza wa Kitume wa Baba Mtakatifu Leo XIV: “Magnifica humanitas” yaani: “Utu wa kupendeza" Juu ya Hifadhi ya Mwanadamu Katika Enzi ya Teknolojia ya Akili Unde” utazinduliwa rasmi tarehe 25 Mei 2026 kwenye Ukumbi wa Sinodi ya Maaskofu, kwa uwepo na ushiriki wa Baba Mtakatifu Leo XIV na hitimisho litatolewa na Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican. Wawezeshaji wakuu katika mchakato wa uzinduzi wa Waraka huu wa Kitume ni Pamoja na: Kardinali Víctor Manuel Fernández, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa, Kardinali Michael Czerny, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Huduma ya Maendeleo Fungamani ya Binadamu; Profesa Anna Rowlands, Taalimungu ya Siasa inayojumuisha Mafundisho Jamii ya Kanisa, Kanuni Maadili ya Taalimungu Mintarafu Uhamiaji, Kitivo cha Taalimungu na Dini kutoka Chuo Kikuu cha Durham, nchini Uingereza; Christopher Olah, mwanzilishi mwenza wa “Anthropic (USA)” na Mkuu wa Idara ya Utafiti juu ya kufasiri matumizi ya Teknolojia ya Akili unde na hatimaye ni Profesa Leocadie Lushombo i.t., Taalimungu ya Siasa, Mafundisho Jamii ya Kikatoliki, Shule ya Wanataalimungu Wayesuit katika Chuo Kikuu cha “Santa Clara”, California. Mwishoni mwa tukio hili la uzinduzi wa Waraka wa kwanza wa Kitume wa Baba Mtakatifu Leo XIV “Magnifica humanitas”  yaani "Utu wa kupendeza" Juu ya Hifadhi ya Mwanadamu Katika Enzi ya Teknolojia ya Akili Unde, Baba Mtakatifu atawapatia baraka zake za kitume washiriki wote.

Papa Leo XIV Magnifica humanitas

 

19 Mei 2026, 15:33