Tafuta

Papa Leo XIV:kufungua mlango kwa Mungu,Kanisa na mioyo yetu!

Tunahitaji kujigundua katika Mungu kama Baba ambaye anatupenda,anajenga Kanisa mahali ambapo wote wanajihisi kuwa nyumbani na kufanya kukua katika ulimwengu wa kidugu,ambamo amani inatawala kati ya watu wote.Kama mitume wa kwanza,tumkabidhi kwa maombezi ya Bikira Maria,Kikao cha Roho Mtakatifu na Mama wa Kanisa.Ni katika tafakari ya Papa Leo XIV kabla ya Sala ya Malkia wa Mbingu katika sherehe za Pentekoste Dominika Mei 24.

Na Angella rwezaula – Vatican.

Tunaweza kujiuliza hata leo hi; ni milango gani inafunguliwa na Roho Mtakatifu? Mlango wa kwanza ni Mungu mwenyewe, wa pili wa Karamu kuu ya Kanisa na milango ya mioyo yetu. Ametumia swali hili na kujibu katika tafakari yake Baba Mtakatifu Leo XIV, kabla ya Sala ya Malkia wa Mbingu kwa waamini na mahujaji waliokuwa katika Uwanja wa Mtakatifu Petro, Dominika tarehe 24 Mei 2026, katika kuadhimisha Sherehe ya Pentekoste, siku kuu kubwa ya kuzaliwa kwa Kanisa. Papa Leo XIV alianza kusema: “Katika sherehe za Pentekoste, tunaitwa kutafakari zawadi ya Roho Myakatifu, alishuka kwa wingi  juu ya Kanisa linalozaliwa na leo hii kwa upya kujitoa kwa wajumbe wake, kama mwanga na nguvu ambayo inaliongoza kwa kila hali ya maisha."

waamini katika sala ya Malkia wa Mbingu
waamini katika sala ya Malkia wa Mbingu   (@Vatican Media)

Papa aliendelea kwamba "Tunaweza kusima kutafakari juu ya picha ya roho ambaye tunakabidhiwa katika liturujia ya leo hii: Roho Mtakatifu anafungua mlango. Injili kiukweli inatueleza kuwa milango ilikuwa imefunga mahali ambapo mitume walikuwa huku wanaogopa wayahudi(Yh 20,19) na wakati huo huo, kitabu cha Matendo ya Mitume kinasimulia kuwa Roho aliingia kama upepo mkali (Mdo 2,2) ambao ulifungua milango na kusukuma mitume kutoka nje kutangaza Habari Njema ya Kristo Mfufuka. Papa Leo XIV aliendelea kusema kuwa “Tunaweza kujifuliza hata leo hi; ni milango gani inafunguliwa na Roho Mtakatifu?"

Mlango wa kwanza ni Mungu mwenyewe

Mlango wa kwanza Papa alijibu "ni ule wa Mungu mwenyewe, katika maana ya kwamba anatufungulia fumbo la Mungu kama alivyojifanya katika Yesu Kristo. Kwa zawadi ya Roho wake, Mungu anatupatia imani ya kweli, inatufanya kuelewa maana ya maandiko, inatufanya kuelewa jinsi alivyo karibu na kuturuhusu kushiriki katika maisha yake mwenyewe. Roho Mtakatifu anatusaidia kufanya uzoefu wa kibinafsi na Mungu kukutana na Yesu na si tu katika kushikilia sheria, ba kumtambua  katika sisi na kugundua ishara za uwepo wake kila siku ya maisha yetu."

Mlango wa pili ni Karamu kuu ya Kanisa

Mlango wa pili ni ule wa Karamu kuu yaani wa Kanisa. Papa alisema kwamba "Bila moto wa Roho,  Kanisa linabaki mfungwa wa hofu, woga mbele ya changamoto za dunia, limefunga lenyewe na hivyo kutokuwa na uwezo wa kuingia katika mazungumzo na kipindi kinachobalika. Roho anafungua milango ya Kanisa kwa sababu liwe karibu  na kukaribisha wote, hata kwa yule anayefungia milango Mungu, wengine, kwa matumaini na kwa furaha ya kuishi. Kama alivyokumbusha Papa Francisko. Tunaalikwa kuwa “Kanisa ambalo linabariki na kutia moyo(…), Kanisa lenye milango iliyowazi kwa wote (Mahubiri,Ufunguzi wa Sinodo 4 Oktoba 2013)"

Waamini waliokuwa katika Uwanja wa Mtakatifu Petro Mei 24
Waamini waliokuwa katika Uwanja wa Mtakatifu Petro Mei 24   (@Vatican Media)

Roho anafungua milango ya mioyo yetu

Hatimaye, Baba Mtakatifu Leo XIV alieleza kuwa Roho Mtakatifu anafungua milango ya mioyo yetu, kwa kutusaidia kushinda  upinzani, ubinafsi, shaka na hukumu, na kutufanya kuwa na uwzo wa kuishi kama wana wa Mungu na ndugu kati yetu. Mahali penye Roho wa Bwana kunazaliwa udugu kati ya watu, makundi, watu wa dunia, na wote wanazungumza lugha moja ya upendo, ambayo inaunganisha na kuleta maelewano kati ya utofauti. Kwa kuhitimisha Papa alisema kuwa hata katika siku zeu, hasa katika siku hii ya Pentekoste, tunapaswa kumuomba Roho Mtakatifu, kwa sababu afungue milango yote ambayo bado imefungwa. Tunahitaji kujigundua katika Mungu kama Baba ambaye anatupenda,anajenga Kanisa mahali ambapo wote wanajihisi kuwa nyumbani na kufanya kukua katika ulimwengu wa kidugu,ambamo amani inatawala kati ya watu wote. Kama mitume wa kwanza, tumkabidhi kwa maombezi ya Bikira Maria, Kikao cha Roho Mtakatifu na Mama wa Kanisa.

Tafakari ya Papa kabla ya Sala ya Malkia wa Mbingu

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.

24 Mei 2026, 12:30