Tafuta

Papa Leo XIV:Kila mageuzi lazima yatanguliwe na utafiti wa kitaalimungu,kihistoria na kichungaji

Baba Mtakatifu Leo XIV ameendeleza tafakari ya Mtaguso wa II wa Vatican,Mei 27,kwa kujikita juu ya Upatanisho:"Liturujia,tamaduni na maendeleo huunganisha na kukuza maisha ya Kikristo.Ibada ya Kanisa imekuwa ikijumuishwa katika aina za kiutamaduni za kila enzi na kuwa nguvu inayoendesha uinjilishaji."

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Mediator Dei, ni waraka wa kumi na mbili uliochapishwa na Papa Pio XII mnamo tarehe 20 Novemba, 1947. Unashughulikia liturujia. Unafuata mageuzi ya liturujia yaliyotekelezwa na Kanisa Katoliki wakati wa karne ya 20, na kufikia kilele katika katiba ya kitume ya Mtaguso wa Pili wa Vatican Sacrosanctum Concilium, ambao umekuwa kiini cha katekesi ya Baba Mtakatifu Leo XIV, Jumatano tarehe 27 Mei 2026, ikiwa ni mwendelezo wa tafakari kuhusu Katiba ya Mtaguso.

Baba Mtakatifu akiwageukia waamini na mahujaji waliofika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro alisema “Katika Waraka wa Mediator Dei, Mtumishi wa Mungu Pio XII, aliandika kwamba:  "Kanisa ni kiumbe hai, na kwa hivyo, hata kuhusu liturujia takatifu, huku likidumisha uadilifu wa mafundisho yake, hukua na kuiongezea huku, likibadilika na kuendana na hali na mahitaji yanayotokea baada ya muda" (I,V). Kwa mwendelezo kamili wa kanuni hii, Mtaguso wa Pili wa Vatican katika Utangulizi wa Katiba Sacrosanctum Concilium (SC), unatambua "wajibu wake wa kupendezwa sana na mageuzi na uendelezaji wa liturujia" (namba1).

Papa na wanandoa wapya
Papa na wanandoa wapya   (@VATICAN MEDIA)

Kikao cha Mtaguso kiliitishwa, Papa Leo XIV alieleza kuwa kiukweli, kwa lengo la "kuendeleza zaidi maisha ya Kikristo miongoni mwa waamini, kuzoea vyema mahitaji ya wakati wetu, taasisi hizo ambazo zinaweza kubadilika, kuhimiza kila kitu kinachoweza kuchangia muungano wa waamini wote katika Kristo, na kuimarisha chochote kinachosaidia kuwaita watu wote kifuani mwa Kanisa." Wakati huo katika historia, kulikuwa na hitaji kubwa la kupyaishwa kwa aina za ibada za kiliturujia ambazo Kanisa kwa karne nyingi lilikuwa limefanikisha utukufu wa Mungu na utakaso wa watu Wakristo.

Shukrani kwa harakati ya Liturujia, imani hiyo ilikuwa imekomaa, ambayo baadaye ilioneshwa na Mtakatifu Yohane Paulo II, kwamba "kuna uhusiano wa karibu sana na wa kina kati ya kupyaishwa  kwa liturujia na kupyaishwa kwa maisha yote ya Kanisa. Kanisa halitendi tu bali pia linajieleza katika liturujia, na kutoka katika liturujia hupata nguvu kwa ajili ya maisha" (Dominicae Cenae, 13). Ili kurahisisha ufikiaji wa waamini kwa utajiri wa zawadi za neema zinazotolewa na liturujia takatifu, Katiba Sacrosanctum Concilium inaonesha kwa kanuni yenye ufanisi sana mwelekeo wa kufuata: "kuhifadhi tamaduni  nzuri na kufungua maendeleo halali" (SC, 23).

Papa na baadhi ya wanahija
Papa na baadhi ya wanahija   (@VATICAN MEDIA)

Papa Benedikto wa XVI katika tangazo hili la nia alielezea "mpango wa mageuzi" wa Mababa wa Mtaguso, "kwa usawa na utamaduni mkuu wa kiliturujia wa zamani na ujao," akibainisha jinsi "tamaduni  na maendeleo mara nyingi hutofautishwa vibaya," huku "kiukweli, dhana hizo mbili zikikamilishana: tamaduni yenyewe kwa namna fulani inajumuisha maendeleo. Kana kwamba mto wa tamaduni pia hubeba ndani yake chanzo chake na huelekea kwenye mdomo wake,"(Mkutano wa maadhimisho ya miaka  50 ya Mfuko wa Taasisi ya Kipapa ya Mtakatifu  Anselmeo taqrtehe 6 Mei 2011).

Mtaguso unathibitisha uhalali wa maendeleo haya, yenye mizizi katika Mapokeo halisi, yakitofautisha ndani ya liturujia "sehemu isiyobadilika, kwa sababu imeanzishwa kimungu," kutoka "sehemu zinazoweza kubadilika, ambazo baada ya muda zinaweza au hata lazima zibadilike, ikiwa vipengele visivyoendana na asili ya ndani ya liturujia yenyewe vimeingia ndani yake, au vinapaswa kuwa visivyofaa" (SC, 21). Mabadiliko kama hayo yametokea kila mara katika karne nyingi, yakiwawezesha waamini kushiriki kwa matunda, kupitia matendo ya ibada, katika Fumbo la Pasaka la Kristo, msingi wa imani ya Kikristo. Kwa hivyo, ibada ya Kanisa imekuwa "iliyojumuishwa" katika aina za kitamaduni za kila enzi na imekuwa na uwezo wa kuzishawishi na hata kuzibadilisha. Kwa hivyo, liturujia imekuwa, kwa karne nyingi, nguvu inayoendesha uinjilishaji.

Papa Leo na kundi la wanahija
Papa Leo na kundi la wanahija   (@Vatican Media)

Papa Leo XIV alisisitiza kwamba leo nguvu hii lazima ifanywe upya katika mwendelezo na tamaduni  halisi na hai ya Kikatoliki, yaani, kulingana na nguvu inayolenga kuwatambulisha waamini kwenye utimilifu wa ukweli. Kwa hivyo inaeleweka kwa nini Mababa wa Mtaguso walipendekeza kwamba marekebisho ya ibada, wakati yanapolingana na "faida ya kweli na iliyothibitishwa ya Kanisa," yanapaswa kufanywa kila wakati "kwa uangalifu kwamba aina mpya kwa namna fulani zikue katika kiungo  kutoka kwa zile zilizopo"(SC, 23). Kwa manufaa ya Kanisa lote, kila mageuzi lazima "yatanguliwe na utafiti makini wa kitaalimungu, kihistoria, na kichungaji."

Majisterio ya Mtaguso, kwa njia hii, inatoa wito wa kuepuka mkanganyiko miongoni mwa waamini kwa kumzuia mtu yeyote kuongeza, kuondoa, au kurekebisha chochote katika mambo ya kiliturujia kwa hiari yao wenyewe (taz. SC, 22). Maendeleo yaliyotokana na Katiba ya Mtaguso hayaathiri ushirika wa Kanisa kwa vyovyote vile: bali, yanakusudiwa kuithibitisha na kuiendeleza. Kwa hivyo  Papa alitpa ,woto kwamba “ninawasihi wote walioitwa kuandaa maadhimisho ya  mafumbo ya Mungu, hasa mapadre wanaotekeleza huduma ya uongozi wa kiliturujia, kudumisha heshima hiyo kwa maandiko na kanuni za liturujia zinazotokana na mtazamo wa ndani wa uwazi na kumwamini Mungu, kuonesha unyenyekevu mbele ya ukuu wake na uaminifu wa dhati kwa ushirika wa Kanisa.”

KATEKESI PAPA MEI 21

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.

27 Mei 2026, 11:35