Papa:Wasaidieni watu wanaoteseka wa Gaza na kuheshimu haki za binadamu
Vatican News
Heshimu haki za binadamu za wote na kuwasaidia watu wa Gaza. Ni wito wa Baba Mtakatifu Leo XIV ukitokea huko Castel Gandolfo. Wakati akiondoka huko Villa Barberini, baada ya kutumia masaa ya kupumzika na kufanya kazi huko, Papa alijibu maswali ya waandishi wa habari kuhusu wanaharakati wa Global Sumud Flotilla waliosimamishwa na jeshi la Israeli walipokuwa wakijaribu kupeleka msaada Gaza. Waliripoti kupigwa na kutendewa vibaya, na alisisitiza kwamba "chuki zaidi" inachochewa. "Vurugu hazisaidii," aliongeza. Tunahitaji "kurudi kwenye mazungumzo, kujaribu kutatua matatizo kupitia mazungumzo, tukiheshimu haki za binadamu za wote." "Kwa bahati mbaya, watu wa Gaza bado hawapokei misaada ya kibinadamu. Hii inasababisha maandamano, matatizo, na hata matendo ya wale walioshiriki katika Flotilla," alibainisha Papa, ambaye alitoa wito kwa "mamlaka zote kuwasaidia na kusindikizana na watu wa Gaza ambao wanateseka, na pia kusaidia tayari kuanza kujenga upya."
Pia aliulizwa kuhusu Akili Unde, kufuatia kuchapishwa kwa Waraka wake wa Magnifica Humanitas, ambapo Papa Leo XIV alihimiza mazungumzo ya kuendelea na makampuni makubwa ya AI na alitaja kazi ambayo Baraza la Kipapa la Kuhamasisha Maendeleo Fungamani ya Binadamu linafanya na Anthropic, hii (ni kampuni ya usalama na utafiti ya AI inayofanya kazi ili kujenga mifumo ya AI inayoaminika, inayoweza kufasiriwa, na inayoweza kuendeshwa). "Nadhani ni muhimu sana kuendelea na mazungumzo na kutafuta akili unde isiyo na silaha," alisema, akibainisha kuwa "vita leo vinaendelea kutumia AI," kama ilivyo huko "Lebanon" na katika "maeneo mengine duniani, bila kuzingatia maisha ya binadamu ambayo ni waathiriwa wa haya yote. Hivyo basi wito mpya wa amani."
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.
