Tafuta

2026.04.22 Viaggio Apostolico in Guinea Equatoriale - Incontro con i giovani e le famiglie Tahariri

Uinjilishaji na Ukaribu na Wahamiaji:Ziara Kuelekea Kiini cha Changamoto za Ulaya

Kutoka Madrid hadi Barcelona hadi Visiwa vya Kanari:Changamoto za Hija ya Papa Leo XIV kwenda Hispania katika Maadhimisho ya Miaka Mia Moja ya Kifo cha Gaudí,Mbunifu wa Kanisa Kuu la Familia Takatifu.Ndivyo mwariri wetu mkuu wa Taariri wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano anaandika.

Andrea Tornielli

Safari ya siku saba ambayo Papa Leo XIV anakaribia kufanya nchini Hispania, ambayo itampeleka hadi mji mkuu Madrid, kisha Barcelona, ​​​​na hatimaye hadi Visiwa vya Kanari, ni hija ya kuelekea katikati ya changamoto za Ulaya. Au bora zaidi, ni ziara inayofupisha katika hatua tatu zenye changamoto kubwa zinazokabili Kanisa katika Bara la Kale. Baada ya Türkiye-Uturuki na Lebanon, yenye umuhimu mkubwa wa kiekumeni na kwa amani katika nchi Ardhi ya Mierezi, ambapo katika miezi ya hivi karibuni mgogoro mkubwa umeibuka kwa idadi ya watu walioathiriwa na mabomu ya Israeli; baada ya ziara  ya haraka sana kwenda Monaco na ziara ya mwezi Aprili uliopita kwa  siku 11 ya  kwenda nchi nne za Afrika("hija ya kimisionari" ambayo  Papa Leo alitamani iwe ya kwanza ya upapa wake), leo hii Mrithi wa Petro anakutana na jamii ya Ulaya iliyogawanyika sana: Hispania. Kituo cha kwanza, Madrid, kitaakisiwa hasa na mkutano na wabunge: wakati muhimu wa kukumbuka mtazamo wa Kanisa kuhusu siasa na kujitolea kwa manufaa ya wote.

Mtazamo ambao sasa uko mbali na aina yoyote ya upatanishi, na pia kutoka katika kupunguzwa kwa imani ya Kikristo hadi kwa uhasama unaotetewa na itikadi ya kidunia. Mbali na ulinganifu, kwa sababu Kanisa, ili liwe lenyewe na kutangaza Injili, haliwezi na halipaswi kutegemea nguvu, na kuanzisha miunganisho ambayo huishia kuficha utume wake. Mbali na upendeleo, kwa sababu imani imeumbwa mwilini na Wakristo wameitwa kushuhudia Injili kupitia kujitolea kwa dhati kwa kuifanya jamii iwe na utu zaidi, haki zaidi, na angalau kuzingatia zaidi. Kanisa la Hispania, lililoitwa kushuhudia umoja wa sauti nyingi katika wakati wa mgawanyiko na migogoro, limevumilia, pamoja na watu wote wa Amerika Kusini mikasa ya vita vya wenyewe kwa wenyewe katika karne iliyopita, na majeraha fulani bado hayajapona kikamilifu.

Injili inatangazwaje leo hii katika muktadha wa jamii iliyo na alama kubwa ya tamaduni  kubwa ya Kikristo ambayo imeunda utambulisho wake, lakini ambayo leo hii inaonekana kuwa ya kidunia zaidi? Hili ndilo swali litakaloenea katika hija nzima ya Askofu wa Roma Huko Barcelona, ​​​​hasa wakati wa ziara yake kwenye Basilika  kubwa ya Familia Takatifu(La Sagrada Familia), ambapo Papa atazindua mnara mrefu zaidi uliowekwa wakfu kwa Yesu Kristo, jibu linalowezekana liko: kupitia lugha ya uzuri. Kanisa limekuwa likizungumza na kila mtu kupitia sanaa, na hasa kupitia picha. Katekesi nyingi kwa karne nyingi zimefanywa kupitia picha nyingi, miundo mizuri na sanamu. Familia Takatifu, tunda la imani na fikra ya mbunifu wa Kikatalani aliyekufa miaka mia moja iliyopita na sasa kuna mchakato wa  kuelekea altareni, ni mfano mzuri wa lugha hii ya uzuri: Yeyote anayesimama mbele ya Basilika anaambatana na safari kupitia kiini cha imani ya Kikristo.

Kinara cha Basilika ya Familia Takatifu
Kinara cha Basilika ya Familia Takatifu

Kwa hivyo fundisho la Antoni Gaudí ni la wakati muafaka sana, hasa kwa wakati wetu na kwa Ulaya, ambapo uenezaji wa imani ndani ya familia umekatizwa kwa ufanisi na ambapo uinjilishaji wa kwanza hauwezi kuchukuliwa kirahisi. Hatimaye, kituo huko Kisiwa kikubwa cha  Kanari na Tenerife kinatoa uzoefu wa moja kwa moja wa hali ngumu ya wahamiaji. Wakipona kwa kuvuka, wanagonga milango ya Ulaya, ingawa bara hilo mara nyingi hushindwa kushughulikia dharura hii kwa njia iliyoratibiwa na kupangwa, na kuziacha nchi zilizo hatarini zaidi, ikiwa ni pamoja na Hispania pekee yake.

Inajulikana sana kwamba kituo hicho katika Visiwa vya Kanari kilikuwa ni hamu ambayo tayari ilioneshwa na Papa Francisko, ambayo sasa mrithi wake anaitimiza. Oktoba iliyopita(2025), Papa Leo XIV alichapisha Waraka wa kitume wa Dilexi te," matunda ya mwendelezo wa  kazi iliyoanza wakati wa upapa wa awali. Andiko hilo lilisisitiza uhusiano kati ya upendo wa Kristo na wito wake wa kutuleta karibu na maskini, wasio na bahati, wanaoteseka, na "wageni" waliotajwa na Yesu katika Injili. Katika waraka wa "Magnifica Humanitas," Papa anatoa wito wa "kupata mtazamo tofauti wa kutazama ulimwengu kutoka chini, kwa mtazamo wa macho ya wale wanaoteseka, si kwa mtazamo watu wazima bali kwa kutazama historia kupitia macho ya walio wadogo na si kwa mtazamo wa wenye nguvu; na kutafsiri matukio ya historia kutoka katika mtazamo wa mjane, yatima, mgeni, mtoto aliyejeruhiwa, aliye uhamishoni na mkimbizi." Kwa hivyo, kituo cha Visiwa vya Kanari kinachunguza mwili hai wa mateso ya wasiobahatika, kikiwaita Wakristo kutoa ushuhuda wa kiinjili. Na, wakati huo huo, kinatuita  sisi sote kwa jukumu letu la pamoja: kubaki wanadamu.

Taariri : Tornielli

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.

Ndugu msikilizajia tunakualika usikose kutufuatilia ziara ya Papa Leo XIV kuanzia mwanzoni mwa ziara hadi mwisho wake yaani kuanzia tarehe 6 hadi 12 Juni 2026. Tuko pamoja kuwajuza hatua kwa hatua ya kile ambacho Papa atatekeleza nchini Hispania.

05 Juni 2026, 14:36