Tafuta

Hija ya Kitume ya Papa Leo XIV,Hispania,CEDIA:Hatuwezi kuwasahau maskini

"Unapotoa sadaka yako,je unamtazama machoni anayomba sadaka?Sadaka siyo ufadhili."Alipenda kuuliza Papa Francisko.Alimnukuu katika hotuba ya Papa Leo XIV katika mkutano na wahudumu na wanaohudumiwa wa Mpango wa Kijamii "CEDIA saa 24" huko Madrid,Hispania,Jumamosi jiini Juni 6 akiwa katika Ziara ya Kitume.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Leo XIV Jumamosi jioni tarehe 6 Juni 2026 akiwa katika ziara yake ya IV ya Kitume  nchini Hispania, inayoongozwa na kauli mbiu: "Alzad la mirada," yaani "Inueni macho yenu”(Yh 4:35,) alikutana na Wahudumu na wale wanaohudumiwa wa Mpango wa kijamii "CEDIA masaa 24," huko Madrid. Katika hotuba yake mara baada ya Kardinali kutoa utangulizi, na shuhuda mbali mbali, alieleza furaha kubwa ya kuanza ziara yake huko Madrid. Kama alivyokuwa ametangulia kusema Mwadhama kwamba: “aliyeko Madrid ni mwana Madrid,” Baba Mtakatifu aliongeza: “Nami niko katikati yenu kama mwanamadrid.” Shukrani Madrid kwa makaribisho haya ambayo yananifanya nihisi kuwa sehemu kubwa, familia ya ajabu ambayo kama ilivyo kwa kila familia miujiza ya upendo hutokea," alibainisha Papa. "Kwa namna ya pekee katika nyumba hii, aliongeza Papa "mahali ambapo hakuna anayeachwa peke yake.”

Hotuba ya Papa katika Kituo cha Mpango wa kijamii wa CEDIA masaa 24
Hotuba ya Papa katika Kituo cha Mpango wa kijamii wa CEDIA masaa 24   (@Vatican Media)

CEDIA inatembea katika njia ya Injili

Papa Leo XIV aliendelea kusema kuwa, hapo furaha na uchungu wa kila mmoja, ni furaha na uchungu wa wote na katika kusikilizana, changamoto zinakabiliwa pamoja, bila kudharau ugumu wa hali na wakati huo huo bila kukosa mahitaji ya upendo na haki, katika mazungumzo na wote ambao wanahangaika kwa hakika ubinadamu na ulimwengu wake (Papa Benedikto XIV katika Waraka wa, Deus Caristas est, 25). Papa Leo XIV alisema kwa hivyo CEDIA inatembea katika njia ya Injili, katika nyayo za Yesu, Mwana wa Mungu ambaye alijifanya mwanadamu, si kwa kuponyesha magonjwa yetu na taabu zetu tu, bali kwa ajili ya kutuondolea dhambi na kuishi kama mmoja wa udhaifu anakujitambulisha kwa kila mmoja anayeteseka hadi kutueleza kuwa:“Yote mliyo mtendea mmoja wa ndugu zangu hawa mlinitendea mimi(Mt 25,40)."

Shuhuda wa mama wa mapacha
Shuhuda wa mama wa mapacha   (@Vatican Media)

Papa Leo XIV akikumbuka tena  hotuba ya Mwadhama aligusia juu ya safari ambayo kutoka Bethlehemu inaelekea Mbinguni. Madrid ni maarufu hata kwa mapango ambayo  ina thamani katika kipindi cha Noeli. Uzuri wake lakini ni cheche tu ya maajabu ambayo bado ni makubwa na ya kina ambayo leo hii tunajikuta nayo hapana,” alisema Papa. Papa alinukuu Waraka kuwa: “Wakristo pia, mara nyingi hujiruhusu kuathiriwa na mitazamo inayoundwa na itikadi za kidunia au mwelekeo wa kisiasa na kiuchumi unaosababisha ujumlishaji usio wa haki na hitimisho potofu.

Mkutano wa Papa katika Kituo cha CEDIA masaa 24
Mkutano wa Papa katika Kituo cha CEDIA masaa 24   (@Vatican Media)

Hatuwezi kuwasahau masikini kama tunataka mkondo utiririke kutoka katika Injili

Ukweli kwamba utekelezaji wa upendo unadharauliwa au kudhihakiwa, kana kwamba ni shauku ya wachache na sio kiini cha utume wa Kanisa, unanifanya nifikirie kwamba lazima tusome tena Injili kila wakati, isije ikabadilishwa na mawazo ya kidunia. Hatuwezi kuwasahau maskini ikiwa hatutaki kuachana na mkondo hai wa Kanisa unaotiririka kutoka Injili na kutajirisha kila wakati wa histori(Dilexi te,15).

Kukuza mwoyo wa huruma kwa wengine

Maneno ya Yesu Papa alisema pia ni mwaliko wa kukuza moyo wa huruma mbele ya mahitaji ya wengine (Zab 112,1-9)kwa kuzingatia uhai ndani mwetu wa shauku ya wema ambao Mungu aliweka katika maisha yenyewe ya ubinadamu na ambao imani inakomboa na kuweka nguvu. Baba Mtakatifu Leo XIV alisema Papa Francisko kutokana na hili alikuwa akisema kuwa: “mbele ya fumbo la maisha binafsi, na changamoto za kijamii, anayeamini anaomba huruma, ndani ya kukua kwa ajili ya manufaa ambayo yanamsukuma kujitolea akiwa mstari wa mbele (Marsilia 23,Septemba 2023,) na alikuwa akiweka mtazamo wake dhidi ya hatari ya moyo usioshtuka, wa baridi, unafurahia kuishi kwa mahangaiko, unaojilinda na sintofahamu na kugeuka, usiopenda, wala kusukuma damu zaidi na kupelekea kifo cha mtu."

Wahudumu wa Kituo cha CEDIA kwa masaa 24
Wahudumu wa Kituo cha CEDIA kwa masaa 24   (@Vatican Media)

Je wewe unapotoa sadaka yako unamtazama mtu machoni?

Papa Leo XIV hata hivyo alipenda kusisitiza mantiki ya mwaliko wa Bwana ambao pia unasisitiza kutazama machoni na mkumbatio wa Bwana kwa yule anayetoa sadaka. Alikumbusha jinsi ambavyo Papa Francisko alipenda kusisitza sana akiuliza “Je wewe unapotoa sadaka yako, unamtazama machoni unayempatia sadaka yako? Je unamgusa mkono ili kuhisi mwili wake(Sala ya Malaika wa Bwana 27 Oktoba 2024). Wale wanaopenda kweli  hawazuiliwi kutoa kitu: wanasilisha wanazungumza, wanatafuta kuelewa  hali na sababu, wako makini kwa mahitaji  kimwili na hata yale ya kiroho, hata uhamasishaji fungamani wa mtu,(Ujumbe wa Siku ya VII ya Maskini dunia 13,Juni 2023).

Papa aliwakabidhi kwa Bikira Maria 

Papa Leo XIV alihitimisha kwa kumtazama Mama Maria, ambaye upendo wake wote unapata utimilifu: katika moyo wake wa upendo unaojali huko Kana(Yh 2, 1-11). Kwa shauku ya nyayo za mwanae (Lk2,41-49; 8,19-21), karibu na kushiriki hadi mwisho chini ya Msalaba (Yh 19,25-27). Kwake Yeye Papa Leo XIV alimkabidhi wote na kazi zao, katika ardhi hiyo ambayo yeye amewekwa wakfu, na kuwatakia daima wawe na roho yake ya umama wa ulimwengu na kuongozwa na imani. Kwa pamoja alisema tusema “ tufundisha kukuja Mama, kisima cha huruma, tumbo la msamaha, mkunbatio wa tumaini, mlango wa Utukufu”(Sala ya Mtakatifu Yohane Paulo II kwa Bikira wa Almudena, 15 Juni 1993).

Papa akisaidi kitabu cha Wageni katika Kituo cha Caritas
Papa akisaidi kitabu cha Wageni katika Kituo cha Caritas   (@Vatican Media)

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.

06 Juni 2026, 19:48