Tafuta

Papa Leo XIV kwa viongozi wa Utamaduni:Tujiulize tunapanda nini leo na nini kinastawi?

Mkutano wa "Kusuka mitandao na Ulimwengu wa Utamaduni,Sanaa,Uchumi na Michezo"katika Uwanja wa Movistar,Madrid,Juni 7 jioni kwa siku ya II ya Ziara ya kitume Hispania,Papa Leo XIV aliuliza:"Ni nini kinachochanua na kufifia kimya kimya katika jamii yetu?Vyuo vikuu na uchumi viwe vya huduma ya mtu.Tuna hatari ya kuwa wataalamu wa vyombo vya habari na ufanisi katika uzalishaji,lakini hatujui ni kwa nini,madhumuni gani na kwa ajili ya nani tunazalisha."

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Maswali ya kutoka ya zamani yamerudi kwenye wakati uliopo na mpango wa wakati ujao katika maono yaliyotolewa na Baba Mtakatifu Leo XIV, jioni ya Dominika tarehe 7 Juni 2026, katika hotuba yake kwenye Uwanja wa Movistar, jijini Madrid nchini Hispania ambapo alishiriki katika mkutano wa mada: “Kusuka Mitandao na ulimwengu wa utamaduni, sanaa, biashara, na michezo. Hili lilikuwa tukio la mwisho kwa umma katika siku yake ya  pili ya Ziara ya 4 ya Kitume nchini Hispania. Kwa hakika ilikuwa ni sherehe ya hisia za ndani kabisa za ubinadamu: kuanzia furaha hadi tumaini, huzuni hadi kuchanganyikiwa.

Papa katika Uwanja wa Movistar Madrid
Papa katika Uwanja wa Movistar Madrid   (@Vatican Media)

Hisia hizi zilizidi kuongezeka katika Uwanja huo ambao ni eneo la kawaida la michezo ya mpira wa kikapu wa Real Madrid na matamasha mbali mbali ya  bendi. Katika uwanja huo makofi yalisikika mara kadhaa kwa takriban ya watu 15,000 waliohudhuria wakati wa kuwasili Papa Leo XIV na mengine  yakichukua karibu dakika kumi, yalivutia vivyo hivyo, na kila wakati, tukio likiendelea. Papa Leo XIV alionekana kushangaa na kuwa na hisia katika Uwanja huo.

Tuna hatari ya kuwa wataalamu katika vyombo vya habari na wenye ufanisi katika uzalishaji, lakini hatujui ni kwa nini, kwa madhumuni gani, na nani, na kwa ajili ya nani tunazalisha. Papa alibainmisha katika hotuba yake. Katika muktadha huu, Kanisa, likifahamu mafanikio yake na makosa yake katika historia yote, linatamani kubaki katika mazungumzo na ulimwengu wa kisasa. Papa alikumbusha kauli ya mtangulizi wake, Mtakatifu Paulo VI, katika Umoja wa Mataifa kwamba: kama "mtaalamu wa ubinadamu," Kanisa halijali chochote cha kibinadamu. Kinyume chake, anatualika kuhoji maana halisi ya kuwa binadamu, akishirikisha kwamba katika Yesu tumepata jibu la maswali ya ndani kabisa kuhusu maisha na ukamilifu wake. Kwa hivyo jumuiya ya Kanisa inakusudia kujiunganisha kikamilifu katika muktadha wa kiutamaduni wa kisasa, ambapo "mwanadamu kama mwanadamu ni zaidi," kwa kutumia zana zake kurudi kwenye mzizi wa asili wa utamaduni: kilimo. 

Mkutano na Ulimwengu wa Utamaduni na sanaa
Mkutano na Ulimwengu wa Utamaduni na sanaa   (@Vatican Media)

Papa alisema: Tumeitwa kujiuliza tunachopanda leo hii, ni nini kinachostawi na ni nini kinachonyauka kimya kimya katika jamii yetu; ni maadili gani tunayohifadhi na ni yapi tunayoruhusu yafe. Haya ni maswali mazito na muhimu ambayo hayawezi kupuuzwa. Ili kujibu maswali haya, ni muhimu kujenga mitandao ya mazungumzo ya kijamii ambayo inafahamu lugha nyingi za jamii ya kisasa, iliyoandikwa, ya mdomo, ya kidijitali, ya kuona, na kutoegemea upande wowote. Kila usemi unaweza kuponya au kuharibu, yaani kuharibu matarajio au kufungua upeo mpya, kupanda migawanyiko au kuamsha tena matumaini ya kujenga kitu halisi cha kibinadamu pamoja. "Kwa hivyo, mtandao ni mazungumzo kati ya taasisi zinazozingatia utu wa binadamu. Hii ina maana, kwa mfano, kwamba vyuo vikuu havipaswi kugeuza visogo  kwenye ulimwengu wa kazi au kukataa ukweli; kwamba biashara hazipaswi kuwafikiria wafanyakazi kama sababu tu kwa maslahi yao wenyewe; na kwamba sanaa haipaswi kuwa na wasomi kama kusudi lake pekee; kwamba michezo haipaswi kupunguzwa kuwa tamasha au kubadilishwa kuwa biashara tu; kwamba maendeleo ya kiteknolojia yanapaswa kuzingatia wazee, maskini, na wale ambao hawana sauti."

Papa alikutana na Carolina Marin,mshindi wa Olimpiki ya Badminton huko Rio de Janeiro 2016 na Teresa Parales Mshindi wa Walemavu (Paralimpiki) ya kuongelea
Papa alikutana na Carolina Marin,mshindi wa Olimpiki ya Badminton huko Rio de Janeiro 2016 na Teresa Parales Mshindi wa Walemavu (Paralimpiki) ya kuongelea   (@Vatican Media)

Papa alikazia kusema kuwa, mchango wa Kanisa katika mabadilishano haya unatokana na ufahamu kwamba "Muumba amewasuka wanadamu kwa nyuzi za upendo" ambazo, kwa maneno ya Papa Benedikto XVI, anatoa ushairi, muziki, na furaha kupitia imani. Na kwa hivyo uzuri. Kwa sababu kila mtu, kwa kiwango kikubwa au kidogo, "amepata kitu kizuri" cha kutosha kubadilisha "ndani."Kutangazwa kwa Habari Njema hakuhusiani na mvuto huu. Nchini Hispania, wimbo wa kidini wa kiutamaduni wa Andalusia wa saeta unaambatana na maandamano ya Juma Takatifu; mashairi ya fumbo na fasihi kubwa ni pamoja na waandishi kama vile Lope de Vega,  Mtakatifu Teresa wa Ávila, Mtakatifu Yohane wa Msalaba, na Calderón de la Barca, hadi  Mtakatifu Thomas wa Aquinas, ambaye kazi zake baadhi ya nyimbo za Mwili na Damu ya Yesu Kristo( Corpus Christi,) zinazosherehekewa leo, zimetokana naye, Papa Leo alieleza. Yote haya yanaonesha uhusiano kati ya nyenzo na kiroho zinazounda uwepo wetu.

Ngoma ya kiutamaduni ya kusisimua
Ngoma ya kiutamaduni ya kusisimua   (@Vatican Media)

Urithi huu wa kibinadamu mara nyingi hutafsiriwa kuwa huduma isiyo na ubinafsi na, shukrani kwa imani, husababisha kazi halisi kama vile hospitali na shule. Hili linaongoza kwenye tafakari zaidi: Hii ndiyo sababu ni halali kuuliza kwa uaminifu ikiwa dunia na hasa Ulaya ingeunda utambulisho wake bila chapa ya kiroho ambayo imeenea katika historia yake. Hili si jambo la kuchochea, bali ni mwaliko wa kutafakari kama umilele, ambao umeenea katika wakati na nafasi kupitia mwili wa Yesu Kristo, unaoweza kupatanishwa na maisha ya kila siku, Papa alisisitiza. Na swali jipya: Je, inawezekana kweli kuamini kwamba Ulaya, ambayo tunaipenda sana, ingekuwa sawa bila chapa ya imani? Kwa nini tuogope kwamba umilele unaenea katika maisha yetu ya kila siku? Kilio cha watangulizi wangu bado kipo: Msiogope! Fungueni milango kwa Kristo! Yesu Kristo hachukui chochote kutoka kwetu na anatupa kila kitu, " Papa alipaza sauti ambayo iliitikiwa kwa makofi.

Washiriki wa Mkutano wa kiutamaduni, sanaa na muziki
Washiriki wa Mkutano wa kiutamaduni, sanaa na muziki   (@Vatican Media)

Kisha Baba Mtakatifu Leo XIV alipanua mtazamo wake, akichukua Waraka wa kitume Dilexite te, “Nilikupenda”, na kuuelekeza kwa wale ambao hawawezi kuelezea kikamilifu fadhila zao: wahitaji, ambao huwapa changamoto watu binafsi na mifumo ya kisiasa na kiuchumi, na Kanisa lenyewe, lililoitwa kuzima uchoyo na kukuza matumaini bila kumwacha mtu yeyote. Wazo pia lilirudiwa katika waraka wa Magnifica Humanitas. "Kanisa hili, mtaalamu wa ubinadamu, hata kama wakati mwingine linapingana na nafaka, linasisitiza kwamba miundo ya kiuchumi na kitaasisi ni kwa kiwango tu kwamba inahudumia maendeleo fungamani ya mtu na kuhamasisha ushiriki wa uwajibikaji wa wote."

Washiriki wa shuhuda
Washiriki wa shuhuda   (@Vatican Media)

Kwa kuhitimisha hotuba yake, Papa Leo XIV  alijikita katika michezo, ambayo mara nyingi, zaidi ya hotuba nyingi, hufundisha heshima kuwa adui wa mtu, ushindi ambao haudhalilishi, na kushindwa ambako hakuzalishi chuki. Mtakatifu Yohane Paulo II tayari alikumbusha jinsi, katika nyakati ambapo kitambaa cha mshikamano wa kijamii kinachanika, michezo inaweza kutoa ushuhuda unaong'aa wa mshikamano, amani, na umoja." Wapendwa marafiki, kwa hivyo ninawaalika kuwa nyuzi mpya za kusuka mitandao mipya inayounganisha maeneo yote ya maisha, kusuka jamii mpya ambayo wakati imejaa umilele, utamaduni huhifadhi kumbukumbu na kuhamasisha mazungumzo, elimu inakuza utafutaji wa ukweli kwa roho ya kukosoa, sanaa inahamasisha mshangao na hutoa hisia nzuri, biashara inatambua hadhi ya mtu na kazi inaendelea kuwa nguvu inayoongoza ya matumaini.”

Askofu Mkuu wa Jiji la Madridi akitoa utangulizi
Askofu Mkuu wa Jiji la Madridi akitoa utangulizi   (@Vatican Media)

Askofu Mkuu wa Madrid alimkaribisha Papa.

Kabla ya ushuhuda wa watu mbali mbali na hotuba ya  Papa, Kardinali José Cobo Cano, Askofu Mkuu wa Madrid, alitoa maneno machache ya makaribisho, akirudia kauli mbiu ziara yake ya  kitume, "inua macho yako," na mada hiyo ya kusuka mitandao kwamba maana yake inaweza  kueleweka tu kwa kuziangalia pamoja kwa ujumla. Kinachovunja katika wakati wetu ni "ukosefu wa kuwa na maswali ya  maana, ambayo inaweza kutengenezwa tu  kwa kuunganisha vipande vya ukweli vilivyotawanyika, kama ilivyo vigae vya dirisha lililokubwa la vioo, ili kurejesha nuru kwa wanadamu," alisema.

Walioshiriki Mkutano wa Kusuka mitandao na Ulimwengu wa Utamadunu sanaa, uchumi na michezo
Walioshiriki Mkutano wa Kusuka mitandao na Ulimwengu wa Utamadunu sanaa, uchumi na michezo   (@Vatican Media)

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.

07 Juni 2026, 19:33