Tafuta

La Sagrada Familia na maadalizi ya kufika kwa Papa  Leo  XIV La Sagrada Familia na maadalizi ya kufika kwa Papa Leo XIV 

Msimamizi wa'Familia Takatifu:Ziara ya Papa inatualiaka kuinua macho yetu juu

Padre Josep Maria Turull alizungumza na vyombo vya habari vya Vatican kuhusu maandalizi ya baraka ambayo Papa Leo XIV atatoa mnamo Juni 10,akizindua Mnara wa Yesu katika Kanisa kuu huko Barcelona,wakati wa ziara yake ya kitume ya Hispania.Anakumbuka maneno ya mtu aliyejitolea maisha yake kwa mpango huo,Mtumishi wa Mungu Antoni Gaudí:"Uhalisi unajumuisha kurudi kwenye asili,ambapo uumbaji ni,kazi ya Mungu,ambaye ndiye mwalimu bora."

Edoardo Giribaldi – Vatican.

“Alzad la mirada” yaani “Inueni macho yenu.” Sio tu kauli mbiu ya Ziara yake ya Kitume ya Papa Leo XIV kwenda Hispania kuanzia Juni 6 hadi 12. Huu ni mwaliko ambao Sagrada Família yaani Familia Takatifu huko Barcelona inamnong'oneza mtu yeyote anayevuka kizingiti chake, kwa lugha ambayo haihitaji tafsiri na inasimulia historia ya ulimwengu hata kwa wale ambao bado hawajuhi kusoma. Kwa sababu kila mtu, katika minara ya "Biblia hii iliyochongwa kwa jiwe" inayopenya anga la jiji la Kikatalani, hupata kitu cha uzoefu wao wenyewe, ambacho huwa tofauti kila wakati: majumba ya mchanga, matawi, vidole vinavyoelekea Mnara wa Yesu Kristo. Mita 172: mnara mrefu zaidi wa Basilika kubwa, iliyoundwa na kujengwa kwa sehemu na Mtumishi wa Mungu  Antoni Gaudí, ambaye Papa atazindua na kubariki Jumatano, tarehe 10 Juni 2026.

Kinara cha Basilika ya Familia Takatifu
Kinara cha Basilika ya Familia Takatifu   (©Basílica de la Sagrada Familia, Barcelona, España)

“Kazi ya Mungu”

Padre Josep Maria Turull, Msimamizi wa Kanisa Kuu hilo, anaelezea katika mahojiano na vyombo vya habari vya Vatican kwamba anaweza kufichua kwa sehemu tu maelezo ya ziara ya Askofu wa Roma. Anazungumza na utulivu wa subira wa mtu anayejua kwamba mambo makubwa huchukua muda. Utulivu unaowafaa wale wanaotunza mahali ambapo, tayari kuna zaidi ya miaka 140, bado haujakamilika. Baada ya yote, kama Gaudí mwenyewe, ambaye mchakato wake wa kutangazwa kuwa mtakatifu unaendelea na ambaye ametangaza kazi yake kuwa "kazi ya Mungu," alisema, "mteja wangu hana haraka."

“Kurudi katika asili”

Padre Turull, alieleza Papa, atazindua Mnara, ambao juu yake kutakuwa na msalaba unaoonekana kutoka jiji lote: "Mwaliko wa kurudi kwenye asili, kwa Yesu Kristo anayeunganisha dunia na mbingu." Gaudí, "mbunifu wa Mungu," hakuweza kukamilisha kazi hiyo kutokana na ajali mbaya iliyompata akiwa na umri wa miaka 73. Aligongwa na tramu, lakini hakuna mtu aliyeweza kumtambua, hasa ukizingatia alivyo kuwa na mavazi machafu. Kwa sababu yeye alikuwa mtanashati; alipenda kuvaa vizuri," anaelezea mkuu huyo. "Kisha, alijihusisha zaidi na ujenzi wa Familia Takatifu, hatimaye akijitolea kikamilifu kwake."

Basilika ya Familia Takatifu
Basilika ya Familia Takatifu

Njia ya kwenda chini katika kaburi  la Gaudi

Katika kaburi lililohifadhiwa mabaki ya Gaudí, kaburi hilo, ambalo ni bamba la mawe lisilopambwa, limezungukwa na Kikanisa rahisi, chenye alama ya mtindo wa neo-kiGothic: msingi ambao mbunifu wa Kikatalani, na baada yake vizazi vya wafuasi, walijenga Sagrada Família. Padre Turull anakaa kwenye maelezo, hata ya ajabu zaidi, kama vile visima vya maji matakatifu vilivyotengenezwa kwa maganda makubwa ya Ufilipino. "Ninaamini," anasema, "kwamba moja ya miujiza yenye ufasaha zaidi ni hii: yeyote anayeona kazi hii kwa mara ya kwanza, hasa ndani, anashangaa, midomo yake ikiwa wazi mbele ya uzuri kama huo." Hiki ndicho kizingiti: taalimungu halisi ambayo Gaudí aliikanda kuwa jiwe. Sio pambo, bali lango. Njia ya uzuri kuelekea Mungu kupitia pulchritudinis, ambayo Padre  Turull anakumbuka wakati akikumbuka ziara ya Papa Benedikto XVI mwaka 2010 kwa ajili ya kuwekwa wakfu kwa Basilika hiyo: “Alielewa kwamba Familia ya Takatifu ni kazi bora katika njia ya uzuri. Na kuwasili kwa Papa Leo XIV kunaendana na hilo."

Ndani ya Basilika ya Familia Takatifu
Ndani ya Basilika ya Familia Takatifu

"Sijawahi kuzoea uzuri huu."

Kifungu kutoka kwenye kilima hadi kwenye Kanisa hakijafichuliwa na picha au historia yoyote. "Watu huachwa bila kusema, na kutokana na mshangao huo, hufungua mioyo yao kwa mwandishi wa uzuri huu, ambaye ni Mungu." Kama Gaudí alikuwa na ulimwengu ndani, aliubadilisha kuwa mwanga na kioo. Upande wa mashariki, ule wa Kuzaliwa kwa Yesu, njano, machungwa, na kijani kibichi hutawala: rangi za alfajiri na mwanzo wa maisha. Upande wa magharibi, upande wa Mateso, bluu, zambarau, na kijivu hutawala: rangi za machweo na fumbo. Katikati, juu ya madhabahu, nyeupe, kana kwamba mwanga wote ulikusanyika na kupata utulivu wake hapo.

Kaburi la Mwanzilishi wa kanisa hilo
Kaburi la Mwanzilishi wa kanisa hilo

Siri za Basilika ya Familia Takatifu

Kila sehemu ya mbele ni Injili iliyochongwa. Sehemu ya mbele ya Pango la Kuzaliwa kwa Yesu, ambayo linaitazama unapotoka kwenye treni ya chini ya ardhi ya jiji, imejaa uhai; Sehemu ya mbele ya Mateso  ina watu wengi sawa lakini ikiwa na pembe kama maombolezo: uwanja karibu na maumbo ya ujazo yanaonesha uzito wa maumivu katika jiwe. "Sijui siri zote pia, sikuweza hata kutoa asilimia," anakiri Padre Turull, ambaye, hata hivyo, anafurahi kuelezea maana ya umbo lililojaa namb karibu na matukio ya uchungu wa Yesu: "Uwanja wa ajabu," karibu kuna  sanamu ya Busu la Yuda. Ndani yake, jumla kwenye safu, nguzo, mlalo, kwenye masanduku ya kati, na kwenye pembe—daima ni 33: marejeo dhahiri ya umri wa Yesu wakati wa kusulubiwa.

Kati ya nyota na majumba

Pia kuna kipengele kinachopendwa sana na mkuu wa Basilika hiyo: Mnara wa Maria, wenye nyota yenye ncha kumi na mbili iliyozinduliwa mwaka 2021. "Imebadilisha mtazamo wa wale wanaoishi hapa. Nakumbuka wazee, wagonjwa walioinua macho yao juu kwenye nyota hiyo kila asubuhi na kuilaki jioni kabla ya kulala." "Uhalisia unajumuisha kurudi kwenye asili," ulikuwa msemo wa Gaudí, uliokumbukwa na Padre Turull kwamba: "Rudi kwenye uumbaji, ambao ni mwalimu bora." Kundi la nyota linalowaongoza wazee katika huzuni yao, mchezo wa utotoni uliopanuliwa hadi kiwango kikubwa, Basilika ya 'Sagrada Família' haihitaji mada ya ziara ya kitume. "Inueni macho yenu" tayari inasema, kwa jiwe. Kwa kila mtu.

Basilika nzuri sana
Basilika nzuri sana

Imesasishwa tarehe 6 Juni 2026 saa 5.00 asubuhi na Angella Rwezaula 

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.

06 Juni 2026, 10:48