Tafuta

Picha ya Papa Leo XIV wakati wa ziara ya kitume nchini Cameroon katika Hospitali Katoliki ya Mtakatifu Paulo,Douala. Picha ya Papa Leo XIV wakati wa ziara ya kitume nchini Cameroon katika Hospitali Katoliki ya Mtakatifu Paulo,Douala.  (@Vatican Media)

Papa Leo XIV:Kuboresha huduma kwa wagonjwa na kuponya majeraha ya wale wanaoteseka

Papa Leo XIV ametuma ujumbe uliosainiwa na Katibu Mkuu wa Vatican Kardinali Parolin,kwa ajili ya mkutano wa afya wa Caritas Internationalis kuhusu mada:"Mbinu kamili ya afya katika Shirikisho la Caritas kuanzia Juni 23 hadi 25,2026.Papa anawahimiza wawakilishi "kuendelea kuchangia katika utume wa Kanisa linapotangaza Ufalme wa Mungu kupitia uwepo wake miongoni mwa wagonjwa,akionesha kwamba wokovu si wazo la kufikirika bali huanza na hatua halisi ya kuponya majeraha ya wanaoteseka.

Vatican News

Msukumo mpya wa ushirikiano na mshikamano katika juhudi zenu za kuboresha huduma ya afya kwa wagonjwa, kwa kuzingatia maadili ya Injili. Haya ndiyo matokeo ambayo Papa Leo XIV anatumaini yatapatikana kupitia Mkutano wa Afya ulioandaliwa na Caritas Internationalis huko Castel Gandolfo, Roma kuanzia Juni 23 hadi 25, kwa mada "Mbinu Kamili ya Afya katika Shirikisho la Caritas." Katika ujumbe uliosainiwa na Katibu wa Vatican,  Kardinali Pietro Parolin, Papa anakumbuka Maandiko Matakatifu, ambayo mara nyingi yanamwonesha Yesu "kama daktari wa kimungu anayeleta afya kwa wagonjwa kwa kuponya aina mbalimbali za mateso ya kiakili, kimwili, na kiroho yaliyowasababishia maumivu, aibu, na kutengwa."

Utu wa Kila Mwanadamu

Ujumbe huo pia unataja kifungu kutoka katika waraka wake wa Magnifica Humanitas, unaosema kwamba: "utu wa kibiolojia ni wa kila mwanadamu kwa sababu tu ya kuwepo, kwa kuwa ametamaniwa, ameumbwa, na kupendwa na Mungu," na kwa hivyo "hupita hali ya mtu binafsi." "Kwa kurejesha afya, Yesu anafunua utu huu wa asili na hivyo anaelekeza kwenye wokovu wetu wa milele katika Mungu," Papa anasema.

Kuwapa Huruma na Ukarimu Wale Wenye Uhitaji

Kwa hivyo Papa Leo XIV anawahimiza wawakilishi katika Mkutano "kuendelea kuchangia katika utume wa Kanisa linapotangaza Ufalme wa Mungu kupitia uwepo wake miongoni mwa wagonjwa, akionesha kwamba wokovu si wazo la kufikirika bali huanza na hatua halisi ya kuponya majeraha ya wale wanaoteseka." Askofu wa Roma anatumaini kwamba kazi yao "itakuwa na lengo la kuleta huruma na wema wa Mungu kwa wale walio na uhitaji zaidi."

PAPA CARISTAS INTERNATIONALISI

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku. Just click here.

24 Juni 2026, 17:15