Papa Leo XIV,Agostinian:Ushirika na umoja uwe ishara katika ulimwengu wa kihistoria!
Vatican News
Dominika alasiri tarehe 7 Juni 2026 kabla ya kufika kwenye Jengo la Uwanja wa Movistar jijini Madrid kwa ajili ya Mkutano wenye mada: “kusuka mitandao na Ulimwengu wa Utamaduni, Sanaa, Uchumi, na Michezo," ikiwa ni siku yake ya Pili akiwa katika ziara yake ya 4 ya Kitume Baba Mtakatifu Leo XIV alikutana na takriban Mapadre wa Kiagostiniani 220 kutoka Jumuiya mbalimbali na wajumbe kadhaa wa familia ya Kiagostinian walioko Hispania.
Ofisi ya Habari ya Vatican ilitangaza hili kupitia chaneli yake ya Telegram, ikiripoti kwamba: “Baada ya salamu kutoka kwa Mkuu wa Kanda, Papa alitoa shukrani kwa wale waliokuwepo kwa fursa ya kukutana, huku akisisitiza jinsi ushirika na moyo wa umoja miongoni mwa waagostinian unavyoweza kuwa ujumbe kwa ulimwengu katika wakati huu wa kihistoria.”
Huu ulikuwa ni ujumbe wa kuwafikishia vijana, kama wale 600,000 waliokusanyika katika Uwanja wa Lima Jumamosi usiku tarehe 6 Juni 2026, ambao walishirikisha maswali yao na juhudi zao za kiroho. Na, akitaja uwepo wa dada zao watawa wa ndani, Papa Leo XIV alisisitiza "thamani ya wito wao, pia katika kutoa maana kwa vitendo vya kijamii, wakati ambapo ukimya na uwezo wa kuingia moyoni mwa mtu unapotea," Ofisi ya habari ilitaarifu.
Hatimaye kabla ya kuwasalimia mmoja mmoja, Papa Leo XIV aliwaalika waliokuwapo kusali pamoja sala ya Baba Yetu, na kuwapatia Baraka ya kitume.
"Vijana, ni kama taa ya asubuhi"
"Wakati wa mkutano huu mzuri na kama wa kifamilia kweli, alizungumzia kwa undani mada ya utunzaji wa kichungaji, hasa huduma ya vijana," Padre José alitoa maoni yake kwa waandishi wa habari wa Vatican. "Papa Leo alivutiwa sana na vijana wa kiume na wa kike wa Hispania", kwa maana ya wale aliokutana nao usiku wa mkesha.
"Alituambia kwamba vijana ni kama taa ya asubuhi, 'nyota.' Kwa Kihispania, brillio - mng'ao. Mnaitaje kwa Kiitaliano?" Padre Herranz aliuliza. "Pia alizungumzia huduma ya vijana na kazi yote ambayo sisi Waagostinian tunafanya na vijana. Alitushukuru kwa kile tunachofanya hapa Hispania na kututia moyo na ujasiri wa kusonga mbele na kufanya kazi kwa bidii kwa ajili ya watu wa Mungu," alisema Padre huyo.
Imesasishwa tarehe 7 Juni 2026, saa 2.00 usiku na Angella Rwezaula .
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.
