Tafuta

2026.06.25 Wajumbe wa Shirikisho la Michezo wa Kuogelea nchini Italia. 2026.06.25 Wajumbe wa Shirikisho la Michezo wa Kuogelea nchini Italia.  (@Vatican Media)

Papa Leo XIV:Kuishi kunamaanisha kujifunza kuishi kwa amani na wengine!

Papa Leo XIV alikutana katika Ukumbi wa Clementine wa Jumba la Kitume Juni 25 na viongozi wa Shirikisho la Kuogelea la Italia na washiriki wa kimataifa katika Kombe la 62 la ‘Sette Colli ambapo amesisitiza kuwa ni muhimu“kukuza kujitolea,mshikamano na uaminifu,ambayo ni maadili yanayodumu hata wakati umri wa michezo ya ushindani unapita.Michezo huungana zaidi ya tofauti na inatoa ishara ya ulimwengu wenye amani.”

Na Angella Rwezaula - Vatican.

Kwa wanariadha kutoka ulimwenguni watakaoshiriki Toleo la 62 la Kombe la Kuogelea la "Sette Colli" mjini Roma katika siku zijazo, Baba Mtakatifu Leo XIV alibainisha kuwa hii ni "ishara ya matumaini, ishara ya ulimwengu tunaoutaka." Papa alikutana nao pamoja na viongozi wa Shirikisho la Kuogelea la Italia Alhamisi asubuhi tarehe 26 Juni 2026 katika Ukumbi wa Clementine mjini Vatican, wakati wa Mashindano ya Kimataifa ya Kuogelea, yatakayofanyika kuanzia  tarehe 25 - 28 Juni  2026 katika Ukumbi wa Foro Italico.

Mchezo unachangia ukuaji wa kiroho

Papa Leo XIV alisema kwamba "Nyinyi nyote, kiukweli, kutoka nchi tofauti, mmekusanyika hapa, mkiongozwa na shauku ile ile na maadili yaleyale, zaidi ya tofauti yoyote ya lugha, utaifa, au utamaduni. Ukweli huu, wa kawaida wa matukio ya michezo ya kimataifa, unatoa ishara ya matumaini, ishara ya ulimwengu tunaoutaka; unachangia makutano ya amani kati ya watu na udugu." 

Papa na Shirikisho la Michezo ya Kuogelea nchini Italia
Papa na Shirikisho la Michezo ya Kuogelea nchini Italia   (@VATICAN MEDIA)

Papa Leo XIV alisema, "wakati mazoezi yanafanywa vizuri," huendeleza ukuaji wa "viungo mbalimbali vya mtu," ikithamini "kujitolea, mshikamano, na uaminifu." Zaidi ya hayo, si dawa ya mwili na roho tu, bali pia fursa ya ukuaji wa kiroho. Kwa njia hiyo kuogelea, hasa, kwa kuogelea  majini, kwa mfano hukumbusha kipengele cha msingi cha ubinadamu.

Kueneza maadili ya michezo

Papa Leo XIV alisisitiza kwamba "Kuishi kunamaanisha kujifunza kuishi kwa amani na wengine na mazingira yanayotuzunguka. Kwetu sisi Wakristo, maji ni ishara ya Ubatizo na maisha mapya katika Kristo." Kadhalika Papa aliwahimiza wanariadha kuendelea "kufanya mazoezi na kueneza" maadili ya michezo, hata zaidi ya taaluma zao: "Umri wa michezo ya ushindani hupita, lakini maadili hayo hubaki!" Hatimaye, aliwakabidhi wote kwa maombezi ya Mtakatifu Pier Giorgio Frassati, "mwanariadha kijana aliyependa kupanda milima sana."

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku. Just click here.

25 Juni 2026, 14:25