Tafuta

Sherehe ya Watakatifu Petro na Paulo: Mahujaji wa imani, matumaini na mapendo: Maaskofu wakuu wapa 35 kupewa Pallio Takatifu Sherehe ya Watakatifu Petro na Paulo: Mahujaji wa imani, matumaini na mapendo: Maaskofu wakuu wapa 35 kupewa Pallio Takatifu  (@Vatican Media)

Sherehe ya Watakatifu Petro na Paulo: Pallio Kwa Maaskofu Wakuu Wapya 35 Wanne ni Kutoka Afrika

Maaskofu wakuu wapya walioteuliwa kati ya Mwaka 2025 hadi mwaka 2026 wanapewa Pallio takatifu ni kitambaa cha sufi safi kinachotengenezwa kwa manyoya ya kondoo wachanga; na kinavaliwa na Baba Mtakatifu pamoja na Maaskofu wakuu wa majimbo makuu ya Kanisa pamoja na Mapatriaki wa Makanisa ya Mashariki. Hii ni alama ya Kristo mchungaji mwema aliyesadaka maisha yake kwa ajili ya kumkomboa mwanadamu kutoka katika lindi la dhambi na mauti!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Leo XIV, katika Sherehe ya Watakatifu Petro na Paulo Miamba wa imani, Jumatatu tarehe 29 Juni 2026, anatarajia kuadhimisha Ibada ya Misa Takatifu pamoja na kuwapatia Pallio Takatifu, Maaskofu wakuu 35 walioteuliwa katika kipindi cha Mwaka 2025-2026. Kati yao kuna Maaskofu wakuu wanne kutoka Barani Afrika nao ni: Askofu mkuu Sithembele SIPUKA: Jimbo kuu la Cape Town (Afrika ya Kusini); Askofu mkuu François SYLLA, Jimbo kuu la Conakry (Guinea); Askofu mkuu Isaac Jogues Kodjo Agbéménya GAGLO Jimbo kuu la Lomé (Togo) n hatimaye ni Askofu mkuu Dennis Kofi AGBENYADZI, S.M.A, Jimbo kuu la Berbérati (Jamhuri ya Watu wa Afrika ya Kati.)

Watakatifu Petro na Paulo Miamba wa imani
Watakatifu Petro na Paulo Miamba wa imani   (@Vatican Media)

Pallio takatifu ni kitambaa cha sufi safi kinachotengenezwa kwa manyoya ya kondoo wachanga; na kinavaliwa na Baba Mtakatifu pamoja na Maaskofu wakuu wa majimbo makuu ya Kanisa Katoliki pamoja na Mapatriaki wa Makanisa ya Mashariki. Hii ni alama ya Kristo mchungaji mwema aliyesadaka maisha yake kwa ajili ya kumkomboa mwanadamu kutoka katika lindi la dhambi na mauti. Kama ilivyokuwa kwa Kristo Yesu, Mchungaji mwema, hata Maaskofu wakuu wanahamasishwa kuwabeba kondoo wao kama kielelezo cha wachungaji wema; wakumbuke kwamba, wameteuliwa si kwa ajili ya mafao yao binafsi, bali kwa ajili ya kondoo wa Kristo Yesu. Maaskofu wakuu wapya wanapaswa pia kusadaka maisha yao kwa ajili ya Kristo Yesu na Kanisa lake. Pallio takatifu ni alama ya umoja na mshikamano kati ya Maaskofu wakuu pamoja na Khalifa wa Mtakatifu Petro.

Maaskofu wakuu wapya 35 kupewa Pallio Takatifu
Maaskofu wakuu wapya 35 kupewa Pallio Takatifu   (@Vatican Media)

MAASKOFU WAKUU WANAOPOKEA PALLIO TAKATIFU 29 JUNI 2026

1. Kard. Grzegorz RYŚ

Askofu mkuu wa Jimbo kuu Kraków (Poland)

2. Kard. Konrad KRAJEWSKI

Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Łódź (Poland)

3. Askofu mkuu Shane Anthony MACKINLAY

Jimbo kuu la Brisbane (Australia)

4. Askofu mkuu Mark S. RIVITUSO

Jimbo kuu la Mobile (Marekani)

5. Askofu mkuu Antonysamy SAVARIMUTHU

Jimbo kuu la Madurai (India)

6. Askofu mkuu Alberto S. UY

Jimbo kuu la Cebu (Ufilipin)

7. Askofu mkuu Júlio Endi AKAMINE, S.A.C.

Jimbo kuu la Belém do Pará (Brazil)

8. Askofu mkuu Andrzej PRZYBYLSKI

Jimbo kuu la Katowice (Polond)

Kardinali Krajewski Jimbo kuu la Lodz, Poland
Kardinali Krajewski Jimbo kuu la Lodz, Poland

9. Askofu mkuu Charles DUVAL, C.Ss.R.

Jimbo kuu la Grouard-McLennan (Canada)

10. Askofu mkuu Charlie M. INZON, O.M.I.

Jimbo kuu la Cotabato (Ufilipin)

11. Askofu mkuu Elias FRANK

Jimbo kuu la Calcutta (India)

12. Askofu mkuu Josef GRÜNWIDL

Jimbo kuu la Wien (Austria)

13. Askofu mkuu David William V. ANTONIO

Jimbo kuu la Nueva Segovia (Ufilipin)

Watu wa Mungu kutoka Cabada wamemsindikiza Askofu mkuu
Watu wa Mungu kutoka Cabada wamemsindikiza Askofu mkuu   (AFP or licensors)

14. Askofu mkuu Susai JESU, O.M.I.

Jimbo kuu la Keewatin-Le Pas (Canada)

15. Askofu mkuu Stephen Andrew HERO

Jimbo kuu la Edmonton (Canada)

16. Askofu mkuu Luciano MAZA HUAMÁN

Jimbo kuu la Piura (Perú)

17. Askofu mkuu Ronald A. HICKS

Jimbo kuu la New York (Marekani)

18. Askofu mkuu Charles Phillip Richard MOTH

Jimbo kuu la Westminster (Uingereza)

19. Askofu mkuu Marco Aurélio GUBIOTTI

Jimbo kuu la Juiz de Fora (Brazil)

20. Askofu mkuu José Roberto FORTES PALAU

Jimbo kuu la Sorocaba (Brazil)

Kuna kundi kubwa la Maaskofu kutoka Canada
Kuna kundi kubwa la Maaskofu kutoka Canada   (AFP or licensors)

21. Askofu mkuu Sithembele SIPUKA

Jimbo kuu la Cape Town (Afrika ya Kusini)

22. Askofu mkuu José Armando ALVAREZ CANO

Jimbo kuu la Morelia (Mexico)

23. Askofu mkuu Stanislav PŘIBYL, C.Ss.R.

Jimbo kuu la Praha (Jamhuri ya Watu wa Czech)

24. Askofu mkuu James R. GOLKA

Jimbo kuu la Denver (Marekani)

25. Askofu mkuu James Francis CHECCHIO

Jimbo kuu la New Orleans (Marekani)

26. Askofu mkuu Francesco Antonio SODDU

Jimbo kuu la Sassari (Italia)

27. Askofu mkuu Luis Augusto CAMPOS FLÓREZ

Jimbo kuu la Bucaramanga (Colombia)

Papa Leo XIV mwaka 2025-2026: Maaskofu wakuu 35
Papa Leo XIV mwaka 2025-2026: Maaskofu wakuu 35   (ANSA)

28. Askofu mkuu François SYLLA

Jimbo kuu la Conakry (Guinea)

29. Askofu mkuu Mário Antônio DA SILVA

Jimbo kuu la Aparecida (Brazil)

30. Askofu mkuu Khalid REHMAT, O.F.M. Cap.

Jimbo kuu la Lahore (Pakistan)

31. Askofu mkuu Isaac Jogues Kodjo Agbéménya GAGLO

Jimbo kuu la Lomé (Togo)

Papa Francisko akiwa na Baraza la Maaskofu Ghana
Papa Francisko akiwa na Baraza la Maaskofu Ghana   (Vatican Media)

32. Askofu mkuu Guy BOULANGER

Jimbo kuu la Sherbrooke (Canada)

33. Askofu mkuu Dennis Kofi AGBENYADZI, S.M.A.

Jimbo kuu la Berbérati (Jamhuri ya Watu wa Afrika ya Kati)

34. Askofu mkuu Michele AUTUORO

Jimbo kuu la Benevento (Italia)

35. Askofu mkuu Giampaolo DIANIN

Jimbo kuu la Gorizia (Italia).

Maaskofu wakuu wapya
28 Juni 2026, 12:56