Papa kwa chakula cha mchana na maskini:udhaifu kama nguvu kwa jamii
Na Antonella Palermo -Vatican.
Tumaini, karibu, ujumuishaji. Hizi ndizo shauku zilizowatia moyo waandaaji wa mpango wa "Chakula cha Mchana na Papa", utakaofanyika tarehe 11 Julai 2026 katika bustani za Castel Gandolfo. Watu mia mbili (watoto 35) walio katika mazingira magumu wakisindikizwa na Jimbo Kuu la Roma na vyama vinavyohusiana nayo vya upendo na watatumia siku nzima wakiwa wamezama katika uzuri na hali ya kiroho ya mahali hapo pa ajabu.
"Mahali hapa pa thamani, palipofungwa kwa ulimwengu kwa miaka 400, kisha kufunguliwa na Papa Francisko, na leo kufunguliwa na Papa Leo XIV panawakaribisha watu hawa ambao ni wageni wetu wa heshima," alisisitiza hayo Donatella Parisi, mratibu wa mawasiliano wa Kituo cha Laudato Si' cha Mafunzo ya Juu. Misa ya asubuhi itaongozwa na Kardinali Fabio Baggio, mkurugenzi mkuu wa Kituo cha Laudato Si' cha Mafunzo ya Juu; akiwa pamoja na Mkuu wa Baraza la Kipapa la Huduma ya Upendo, Askofu Mkuu San Martín. Baada ya hapo, vinywaji na ziara itakayoongozwa wahudumu wa Borgo Laudato si' kwa wageni hawa.
Kanisa ni familia, iliyo wazi kwa wote
Borgo Laudato si' "inatuambia mengi kuhusu historia ya Roma, pamoja na mabaki ya jumba la Domitian, na historia ya Mapapa ambao wamekuja hapa tangu 1600 kupumzika na kisha kujitumbukiza katika uzuri wa asili pamoja na bustani ya mimea yenye mimea zaidi ya 4,000 ya spishi 300 tofauti." Hifadhi ya hazina ya uzuri na maelewano inayofungua milango yake, ikiashiria Kanisa lisilo na vizuizi. "Ndiyo, ujumbe pia ni kwamba Kanisa lazima liwe wazi zaidi kwa wote, hasa kwa wale wanaoishi pembezoni mwa kuwepo kwake. Papa Leo XIV anarudia hili mara kadhaa, na sisi pia tunaona tukio hili kama hatua inayofuata safari ya kwenda Lampedusa, ambapo Papa alionesha umakini wa ulimwengu kwenye kisiwa hiki kidogo katikati ya Mediterania, ambacho kimekuwa shahidi wa hiari wa maelfu ya vifo baharini, watu wanaotafuta mustakabali bora, mara nyingi wakikimbia vita, umaskini, na dhuluma ya kijamii.
"Kwa hivyo leo hii tuko hapa usiku wa tukio," Parisi aliendelea, "ambalo linajithibitisha kama fursa ya kuthibitisha kwamba Kanisa liko wazi kwa kila mtu na ni familia, jamii, na mahali salama kwa wale wanaohitaji zaidi hivi sasa." Ni maskini wanaobadilisha mitazamo. Wazo ni kwamba kila mwaka tukio hili litawakaribisha watu kutoka majimbo tofauti. Mwaka jana (2025)ilikuwa Albano, mwaka huu ni Roma. Kutakuwa na wakimbizi, akina mama wenye watoto bila wanaume, watu ambao wamekamilisha kozi ya mafunzo ya kazi huko Borgo na wanarudi kusherehekea safari ambayo leo hii inaonekana kwa ujasiri mpya wa kuungana na kupata ajira."
Watu wanaotoa na kutajirisha Kanisa
Kuna watu wenye uwezo tofauti, na kutakuwa na wawakilishi wa sehemu hiyo ya jamii na Kanisa ambayo mara nyingi huchukuliwa kuwa "wale wanaohitaji." Kiukweli, tunapata uzoefu kila siku hapa Borgo Laudato si' kwamba ni watu wale wale wanaotoa, na kutoa zaidi. Wanatoa mengi na kutajirisha Borgo na, ningesema, Kanisa lote kwa uwepo wao na mahitaji yao ya maono tofauti ya jamii, mtazamo unaobadilisha udhaifu kuwa nguvu mpya kwa jamii zetu. Chakula cha mchana kilitolewa kwa ukarimu na hiari na mgahawa wa Roma, iutwao “L'Isola della Pizza; viburudisho vya asubuhi vilitolewa na Bar ya “Duomo” huko Albano, ambayo inahusika kwa karibu katika Mpango wa Borgo Laudato si'. "Ni ushuhuda mzuri wa kujitolea kwa mpango kama huu," anasema Parisi. Menyu hiyo itaangazia vyakula vya Kiitaliano, ikilenga wale kutoka asili na tamaduni zingine.
Viumbe Miongoni mwa Viumbe
Mpango huu ni sehemu ya heshima kubwa ya Papa kwa mahali hapa: "Baba Mtakatifu anapenda sana bustani za kipapa, na anafuatilia mpango huu kwa karibu," alithibitisha Parisi, akiwakumbusha mkutano huko Vatican aliokuwa nao mnamo Juni 19, mwishoni mwa mkutano wa siku mbili wa Borgo. Mijadala, ambayo iliwaleta pamoja wawakilishi wa vyombo vingi vya kimataifa vya viwanda na biashara kujadili jinsi ya kufanya michakato ya uzalishaji na mazingira ya kazi kuwa endelevu zaidi ili "kuzidi kuwajibika na kupunguza ukandamizaji." Msukumo, ambao tayari upo katika Hati za Francisko na kurudiwa katika Waraka wa Kitume wa Magnifica Humanitas, unabaki kuwa wa kujiona kama "viumbe miongoni mwa viumbe."
Imesasishwa tarehe 10 Julai 2026 saa 9.24 alasiri na Angella Rwezaula.
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.
