Tafuta

Bado wanaendelea kutafuta watu kwenye vifusi huko La Guaira,Venezuela kufuatia tetemeko la ardhi. Bado wanaendelea kutafuta watu kwenye vifusi huko La Guaira,Venezuela kufuatia tetemeko la ardhi. 

Papa Leo XIV anaendelea kuonesha ukaribu wa sala kwa watu wa Venezuela

Papa Leo XIV, mwishoni mwa sala ya Malaika wa Bwana,mawazo yake yalielekea Venezuela, liyopigwa sana na mitetemeko miwili mikubwa ambayo imesababisha vifo vya karibu watu 3,000. Papa alikumbuka kutangazwa mwenyeheri wa Vietnam Francis Xavier Tru'o'ng Bǚu,aliyeuawa kwa sababu ya chuki ya imani.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Mara baada ya Tafakari na sala ya Malaika wa Bwana, Dominika tarehe 5 Julai 2026, Baba Mtakatifu Leo XIV alielezea ukaribu wake kwa  waathirika wa tetemiko la Ardhi nchini Venezuela na kusema kuwa  “Ninaendelea kuwakumbuka katika sala zangu wahanga wa tetemeko la ardhi na watu wote wa Venezuela. Bwana awategemeze katika wakati huu wa shida kubwa.” Nchi hiyo sasa inahesabu  watu 3,000 waliokufa katika tetemeko la ardhi lililotokea mara mbili, moja ya tetemeko lenye nguvu zaidi na lenye uharibifu mkubwa wa Amerika Kusini. Watu wengi waliokimbia makazi yao bado wako mitaani au wamejificha katika hali mbaya, na timu za uokoaji za kimataifa zinaendelea  hatua kwa hatua utafutaji wao wa manusura katikati ya vifusi.

Kutangazwa mwenyeheri Padre Francis Xavier Tru’o’ng Bǚu
Kutangazwa mwenyeheri Padre Francis Xavier Tru’o’ng Bǚu

Hata hivyo kabla ya hayo alianza kukumbusha  tukio la kutangazwa kwa mwenyeheri kutokotokea huko Vietnam: Kaka  na dada wapendwa, Alhamisi iliyopita, tarehe 2 Julai, Padre Francis Xavier Tru’o’ng Bǚu alitangazwa kuwa mwenyeheri katika Madhabahu ya Tac Say huko Vietnam. Aliuawa mwaka wa 1946 kwa chuki ya imani (katika odium fidei). Katikati ya ukandamizaji na vurugu, alitetea haki za watu na hakuwaacha waumini wake. Maombezi na sala zake ziwaimarishe wale wote wanaotangaza Injili katika hali za mateso leo.”

Mahujaji mjini Vatican
Mahujaji mjini Vatican   (@Vatican Media)

Salamu kwa mahujaji

Baba Mtakatifu Leo XIV alitoa salamu mbalimbali: “Ninatoa salamu zangu za joto kwenu nyote mliokusanyika leo katika Uwanja wa Mtakatifu Petro. Ninawakaribisha kwa uchangamfu mahujaji kutoka Brazil na kwa Kwaya ya Chuo Kikuu cha Mérida huko Venezuela.” Aliwakaribisha kwa lugha ya Kireno.

Makundi katika uwanja wa Mtakatifu Petro
Makundi katika uwanja wa Mtakatifu Petro   (@Vatican Media)

Papa aliendelea kuwakaribisha makundi kadhaa kutoka Poland: mapadre wapya waliowekwa wakfu wa Shirika la Ndugu Wadogo  Wakapuchini  wa Kraków; Kwaya ya Watoto ya Jimbo Kuu la Łódź, ikiambatana na Askofu Msaidizi wao; na kundi kutoka Jimbo la  Legnica. Pia aliwasalimu vijana kutoka Bellagio na Kwaya ya Jubilaeum kutoka Augusta, Sicilia, pamoja na meya wao na Padre  wao. Hatimaye aliwatakia wote  Dominika  njema!

Makundi kutoka Poland
Makundi kutoka Poland   (@Vatican Media)
Papa Leo XIV katika Sala ya Malaika wa Bwana

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku.  Just click here.

05 Julai 2026, 13:00