Tafuta

2026.07.22 Papa atembelea Madhabahu ya Utatu Mtakatifu ya Vallepietra. 2026.07.22 Papa atembelea Madhabahu ya Utatu Mtakatifu ya Vallepietra.  (@Vatican Media)

Papa Leo XIV atembelea Madhabahu ya Vallepietra:"Mungu hatuachi kamwe"

Jumatano Julai 22,Papa Leo XIV alikwenda kusali katika Madhabahu ya Utatu Mtakatifu kwenye mpaka kati ya Lazio na Abruzzo.Mkuu wa Madhabahu alisema:"Ziara isiyotarajiwa lakini maalum.Aliacha kikombe kama zawadi na kuwasalimu mahujaji wote waliokuwepo,zaidi ya mia moja kwa idadi."Akizungumza kwa furaha kutoka kwenye Balkoni ya Madhabahu Papa alikumbusha"hamu ya mioyo yetu ya kumtafuta Mungu,utakatifu na msaada wa Bwana."

Na Alessandro Di Bussolo – Vatican.

Akitazama kutokea kwenye Balkoni ya Madhabahu ya Utatu Mtakatifu ya Vallepietra, iliyoko kwenye uso wa miamba inayotazamana Mlima wa Autore, Papa Leo XIV aliwasalimia na kuwabariki waamini mia moja, mahujaji, na wanachama wa Udugu wa Madhabahu.  Ni wakati wa hadhara unaoashiria ziara hii fupi, ya kushtukiza, iliyodumu kama nusu saa, kuelekea mashariki mwa Lazio, siku mbili baada ya kusimama kwake katika Abasia ya Montecassino. Katika salamu yake, alielezea kuwa "madhabahu ni mahali pazuri sana kiasi kwamba panatukumbusha "hamu katika mioyo yetu yote ya kumtafuta Mungu, utakatifu, na msaada wa Mungu ambaye hatuachi kamwe."

Papa akisali katika madhabahu ya Utatu Mtakatifu
Papa akisali katika madhabahu ya Utatu Mtakatifu   (@Vatican Media)

"Ziara isiyotarajiwa lakini maalum"

Haya yote yalijiri tu alipofika asubuhi  Jumatano tarehe 22 Julai 2026 katika eneo hilo la ibada ya kale, katika mita 1,337 juu ya usawa wa bahari katika mji mdogo kwenye mpaka kati ya Lazio na Abruzzo, Mkuu wa Madhabahu hiyo Monsinyo Alberto Ponzi alielezea  akizungumza na Vyombo vya habari vya Vatican kwamba: "Papa Leo XIV, alipokelewa na shauku ya waamini, ambao walishangaa kama Padre mwenyewe  ambaye alikuwa amearifiwa saa chache tu mapema kabla ya kufika kwake. "Kwetu sisi, ilikuwa ziara isiyotarajiwa lakini maalum, na ilidumu angalau nusu saa," mkuu wa Madhabahu hiyo ambaye tayari alikuwa  amehudumu katika nafasi hiyo wakati wa Mtakatifu Yohane Paulo II alipotembelea mahali hapo Patakatifu wakati wa Jubilei ya 2000 mnamo Oktoba 3, alieleza, "lakini siku hiyo nilikuwa kwenye mkutano na wakuu wa madhabahu huko Canneto."

Il saluto del Papa ai fedeli riuniti all'estero del Santuario di Vallepietra

Papa akisalimia waamini waliokusanyika katika Madhabahu ya Vallepietra   (@Vatican Media)

Sala mbele ya picha ya Utatu Mtakatifu

Mara tu aliposhuka kwenye gari, Papa alipanda hadi madhabahu na kusimama mbele ya sanamu ya Utatu, inayojulikana kama " L'afresco delle Tre Persone", - "Picha ya Watu Watatu." Kisha akahamia kwenye Balkoni ya Madhabahu, mahali ambapo aliwasalimia  mahujaji na kuwabariki," Monsinyo Ponzi alisimulia. " Kisha nikamwonesha vyumba vyote vya Madhabahu hiyo naye alifurahi sana. Kisha nikampeleka kwenye chumba chetu cha kupumzikia, ambapo akanywa kahawa, na Ndugu John na katibu pia walikuwepo. Wakanywa kahawa na maji.

Papa Leone XIV con il rettore del Santuario di Vallepietra, visita la mostra fotografica con la storia del luogo sacro dedicato alla Santissima Trinità

Papa Leo XIV na Mkuu wa Madhabahu ya Vallepietra,akimuonesha maonesho ya picha na historia ya mahali patakatifu pa Utafu Mtakatifu(@Vatican Media)

Sehemu ya marejeo kwa wale wanaotaka kuungamana

Kisha mkuu huyo akakumbuka kwamba Madhabahu ni sehemu ya marejeo kwa wale wote wanaotaka kupokea Sakramenti ya Kitubio. “Nilimuonesha Papa sehemu ya maungamo: wengi wanaokuja hapa hupokea sakramenti, ndiyo maana huwa  kuna  mapadre  wanaopatikana kila wakati. Na leo hii Papa Leo XIV aliwakuta mapadre watatu ambao wako pamoja nasi usiku kucha na wanapatikana kwa ajili ya maungamo.” Hatimaye,  tulihamia kwenye madhabahu ya nje, ambapo mtu anaweza kuona mandhari yote ya bonde. Na kabla ya kuondoka Mahali Patakatifu, Papa Leo XIV alimsalimia kila mhujaji aliyekuwepo mmoja baada ya mwingine.

Il Papa contempla il panorama dall'altare all'aperto sul piazzale del Santuario della Santissima Trinità a Vallepietra

Papa akitazama madhari iliyoko juu ya madhabahu ya Utatu Mtakatifu huko Vallepietra(@Vatican Media)

Zawadi Kubwa kwa Jimbo na Madhabahu

"Ilikuwa zawadi nzuri kwa Jimbo na Madhabahu" alihitimisha Monsinyori Ponzi, ambaye alisema alivyozungumza na Papa "kuhusu mahujaji wanaokuja hapa, makampuni, vikundi vingi vilivyopangwa. Nilielezea kidogo kuhusu maisha ya Madhabahu hii. Kisha nikamwambia Papa: 'Baba Mtakatifu, hakika tutakutana Jumatano ya katekesi, mwishoni mwa Septemba au Oktoba, pamoja na mahujaji wote kutoa shukrani kwa zawadi hii kubwa, ikiwa ni pamoja na Askofu.'" Hatimaye alisisitiza furaha ya kuona nyuso zenye furaha za mahujaji, "katika siku hii nzuri na yenye upepo, kumuona Papa Leo XIV miongoni mwa watu."

Papa aliacha kikombe kwenye Madhabahu kama kumbukumbu na akawapatia  kila mtu rozari. "Hata hivyo, hatukuwa tayari, kwa hivyo nilimwambia: 'Baba Mtakatifu, tutaonana mapema haraka iwezekanavyo katika Basilika ya Mtakatifu Petro kwa ajili ya Katekesi na  tutafikiria juu yake.' 'Ndiyo, ndiyo, ndiyo, usijali,' alijibu."

Imesasisishwa tarehe 22 Julai 2026 saa 12.13 jioni na Angella Rwezaula.

PAPA KATIKA MADHABAHU YA VALLE PIETRA

 

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.

22 Julai 2026, 18:13