Tafuta

Papa Leo XIV alikula chakula cha usiku kwa Balozi wa Marekani anayewakilisha nchi yake katika Kiti Kitakatifu Julai 4,2026. Papa Leo XIV alikula chakula cha usiku kwa Balozi wa Marekani anayewakilisha nchi yake katika Kiti Kitakatifu Julai 4,2026. 

Papa Leo XIV katika makao makuu ya Ubalozi wa Marekani Julai 4

Ofisi ya Habari ya Kiti Kitakatifu iliripoti kupitia Telegram kwamba,wakati wa sikukuu ya kitaifa,Papa Leo XIV alikubali mwaliko wa Balozi Burch kwa kwenda nyumbani kwake jioni Julai 4,2026.

Vatican News

Akikubali mwaliko wa Brian Burch, Balozi wa Marekani anayewakilisha nchi yake katika Kiti Kitakatifu huko Roma, Papa Leo XIV mara baada ya ziara yake ya Kichungaji  ya asubuhi huko Lampedusa nchini Italia alikwenda nyumbani kwake jioni ya Jumamosi, tarehe 4 Julai 2026, ili kuadhimisha pamoja siku kuu ya kitaifa. Hii iliripotiwa na Ofisi ya Vyombo vya Habari ya Kitakatifu kupitia chaneli yake ya Telegram.

Ubalozi wa Marekani katika Kiti Kitakatifu, vile vile  kupitia akaunti yake rasmi ya X @UsinHolySee, uliandika kwamba "Papa Leo XIV alisherehekea miaka 250  kuzaliwa kwa Marekani  pamoja na Balozi Burch, Bi. Burch, na familia yao."

"Nimeheshimiwa sana kusherehekea siku hii maalum na Mmarekani mwenzangu, Askofu wa Roma," Burch mwenyewe alisema.

Papa kwa chakula cha jioni katika Ubalozi wa Marekani katika fursa ya siku ya huru Marekani

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.

 

05 Julai 2026, 09:30