Papa Leo XIV kwa vijana huko Lamego,Ureno:Bwana yupo pamoja nasi na sababu ya furaha yetu
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Leo XIV amewatumia ujumbe kwa njia ya video kwa ajili ya Mkutano wa vijana unaoongozwa na mada“ furahi," ikiwa ni Siku ya vijana Kitaifa huko Lamego nchini Ureno kuanzia tarehe 24-26 Julai 2026.
Ufuatao ni ujumbe kamili wa Papa Leo XIV.
Wapendwa vijana,"Furahi katika Bwana, daima!“(Fil 4,4), hapo Lamego, na kila mahali: katika familia zenu, katika shule, katika maparokia, katika harakati na katika makundi tofauti ambayo ninyi ni sehemu yake. Furahi katika Bwana pamoja na Maaskofu wenu na wahusika ambao wanawasindikiza na vijana wengi huko Ureno. Furahini na wao, ambao wanawasaidia kukua katika imani na kufungulia milango ya moyo kwa Kristo, Njia, Ukweli na Maisha.” Baba Mtakatifu Leo XIV anaendelea: “nimepata kujua kwa furaha kwamba, mnatafuta kutunza mwali unaowaka wa Siku ya vijana Duniani wa mwaka 2023. Zilikuwa ni siku angavu na furaha, kwa maelewano kati ya wote; lugha na tamaduni tofauti; lakini hasa, kwa mkutano wa kina na Bwana Yesu na kwa uzoefu wa ajabu ambao Kristo aliye hai, anatimiza tunapoungana pamoja kwa jina lake.”
Bwana yupo pamoja nasi na sababu ya furaha yetu
Papa Leo XIV aliendelea kusema, “Yeye yupo pamoja nasi na Yeye ni sababu ya fura yetu! Ni Yeye sababu ya umoja wetu. Katika In illo uno unum: “sisi licha ya kuwa wengi, tu mwili mmoja katika Kristo (Rm 12,5). Kwa kutoa ushuhuda binafsi, Papa Leo XIV alisema: “Niliweza kuishi kile ambacho huko Lisbon waliishi mwaka mmoja uliopita, katika Jubilei na katika ziara ya kitume ya hivi karibuni huko Hispania. Kukaa na vijana daima ni tendo maalum, kwa sababu shauku ya maisha yenu ya imani yanaambukiza! Upendo mnao uonesha kwa Kristo ni wa faraja! Ni maajabu, katika nyakati zetu, kuona vijana, kama ninyi, waliojaa imani bila hofu ya kuitangaza.
Msigope kutotulia
Papa anawapongeza: “Ni vizuri kuona kwamba mna kiu ya kina ya ukweli, na hata furaha kwa moyo wa dhati. Ni vizuri kuona kwamba mna njaa ya haki na ya ukweli, na hamfurahii thamani zinazopita-Ni vizuri kutazama kwamba mnapenda uzuri, kwa namna ya pekee uzuri wa zama za kale na mpya sana kama Mungu wetu, ambaye anatusibiri kwa kina wa kuwa sisi.Kwa salamu hizo, Papa amebainisha anavyopenda kuwatia moyo kwenda mbele. Moja ya tabia za vijana ni kutokuwa watulivu. Msiogope kutotulia ambako mna ndani mwenu! Tumia fursa ya nguvu hiyo kwa kukaribia zaidi Kristo na kuhudumia thamani ya Injili. Kwa kushikilia Neno la Yesu, kwa kusoma Injili kila siku, msiache kamwe kuota dunia mahali ambapo kuna amani na udugu, kwa kutazama ulimwengu kwa maajabu, ya kukabiliana mstakabali katika mwanga wa matumaini.
Muwe binadamu kama alivyo Kristo
Wapendwa vijana, msiache chochote kile na yeyote yule kuwaibia matumaini! Ninawaalika hata kwa kutumia fursa ya kile ambacho kinawafanya kutotulia, ili katika wakati wa sala na kwa ukimya, katika mazungumzo na Dio, muulize Yeye: Bwana unataka nifanye nini katika Kanisa na katika Ulimwengu? Wito wangu ni upi? Unaniita niunde familia katika ndoa? Au unaniita katika maisha ya Upadre? au maisha ya utawa? Ni maswali ambayo ji muhimu kujiuliza, bila kusahau uhakika ambao unatoaumoja katika maisha yetu ya ndani. Mungu anaita daima kuwa watakatifu na watakatifu kwa kina ni binadamu. Kwa hiyo muwe binadamu kama alivyo Kristo, kwa hakika, mtabadilisha ulimwengu huu kkuwa ubora. Na Mama Yetu wa Fatima, Mama wa Shauri jema anawasaidie nyote!
Hitimisho na mwaliko wa WYD 2027 huko Seoul
Kwa kuhitimisha Papa Leo XIV anabainisha kwamba "Wapenda marafiki, sasa ninawaombe niny, juu yenu vijana wa Ureno, juu ya wachungaji wenu na wahusika wenu wa uchungaji wa vijana, wingi wa neema za Mbingu. Awabariki Mungu Mwenyezi, Baba, Mwana na Roho Mtakatifu. Amina. Ninawatakia mwendelezo wa furaha ya kukutana katika mji wa Lamego! Na ninatumaini kuwaona mwezi Agosti mnamo 2027 huko Seoul. Asante"
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.
