Tafuta

2026.07.19 Sala yaSala ya Malaika wa Bw3ana 2026.07.19 Sala yaSala ya Malaika wa Bw3ana  (@Vatican Media)

Papa Leo XIV:"Mungu anapendelea udogo"

Katika tafakari ya Injili ya Siku ambapo Papa Leo XIV kabla ya sala ya Malaika wa Bwana,Dominika tarehe 19 Julai 2026 akiwa katika lango la Jumba la Kitume huko Castel Gandolfo mahali anapopitia wakati wa mapumziko yake ya Kiangazi alisema:"Wakati mwingine,sisi tunasubiri jambo kuu,tunatamani,Mungu aingilie kati kutoka juu,kwa kung’oa haraka magugu ya ubaya.Tunamfikiria Mungu mwenye nguvu na madaraka na kwa bahati mbaya,mawazo haya yanakuwa kwa wakristo na kwa Kanisa.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Leo XIV aliongoza tafakari na sala ya Malaika wa Bwana, katika Dominika ya XVI ya Mwaka, tarehe 19 Julai 2026, akiwa katika lango la Jumba la Kitume huko Castel Gandolfo, mahali ambapo anapitia kipindi chake cha mapumziko ya kiangazi.  Kwa kutazama Injili ya Siku aliwageukia umati wa waamini na mahujaji, licha ya joto kali, waliokusanyika katika Uwanja wa Uhuru, Baba Mtakatifu Leo XIV alianza kutafakari kuwa: “Baada ya mfano wa mpanzi, Yesu anaendelea kuzungumza na umati kwa njia ya baadhi ya mifano: ngano nzuri na magugu, mbegu ya ahaladali, chahchu katika unga(Mt 13,24-43). Papa Leo XIV alibainisha kuwa “hii ni mifano mitatu midogo ambayo inataka kutoa mwito wa kufikia Ufalme wa Mungu katika historia, utendaji wake katika maisha ya watu, namna ambavyo unakua, unapanuka na kubadilisha Ulimwengu kutoka ndani.

Mungu anapendelea udogo

Kwa simulizi hizi, Papa anaongeza kusema “Yesu anatupa onyo dhidi ya kishawishi cha kufikiri Mungu kama vile sura ya nguvu, ambaye analazimisha kwa nguvu, anayechukua nafasi ili kumiliki, na anayefika kama mshindi.” Kinyume chake, Mungu anapendelea udogo, ishara ya upendo wake nyeti, ambaye anayeacha uhuru wa kukaribishwa au kukataliwa, ambaye anatafuta kuwa njia,  hata katikati ya magugu mabaya, ambaye anatenda kwa namna iliyofichika na isiyoonekana kama mbegu iliyo ndogo zaidi ya zote na kuchachua unga kutoka ndani bila kelele. Papa Leo XIV aliendelea  kusema kuwa “kwa mifano hiyo, Yesu anatueleza jambo muhimu kuhusu namna ambayo Mungu anatenda katika historia ya maisha yetu na katika historia kwa ujumla. Wakati mwingine, sisi tunasubiri jambo kuu, tunatamani, Mungu aingilie kati kutoka juu, kwa kung’oa haraka magugu ya ubaya.

Papa akitafakari kabla ya Sala ya Malaika  wa Bwana
Papa akitafakari kabla ya Sala ya Malaika wa Bwana   (@Vatican Media)

Tunamfikiria Mungu mwenye nguvu na madaraka

Tunamfikiria Mungu mwenye nguvu na madaraka na kwa bahati mbaya, mawazo  haya tunayakubali hata kwa namna yetu ya kuwa wakristo na kuwa Kanisa; Kinyume chake, Ufalme wa Mungu unaenea hata katikati ya magugu mabaya na unatuomba kuwa na mtazamo wenye uwezo wa kupokea wema ambao unachipuka hata kati ya giza la ubaya, bila hukumu yote na haraka: unakuja kama mbegu iliyo ndogo zaidi na kuomba kwa hiyo uvumilivu wa kuja kusindikiza mchakato kwa kumtambua katika udogo wa kila siku, na katika urahisi wa maisha ya kawaida; unakua kwa njia  isiyoonekana, kama chachu kwenye unga na hivyo kutuokoa dhidi ya kukata tamaa na kutualika kuwa na imani hata wakati unafikiri Mungu hayupo. Kwa sababu kiuhalisia, Yeye anatusindikiza daima na upendo wake daima unatenda kwa ajili yetu.

Waamini huko Castel Gandolfo
Waamini huko Castel Gandolfo   (@Vatican Media)

Tuishi mtindo wa Mungu wa kuishi kibinafsi na kama Kanisa

Baba Mtakatifgu Leo XIV alisistiza tena kuwa, “mtindo huo wa Mungu lazima ugeuke hata kwa namna ambayo iwe kwa kibinafsi na kama Kanisa, tunaishi katika hali halisi ambayo inatuzunguka. Tumeitwa kuchukua mtindo mmoja wa Kiinjili, bila kujipinga kwa haraka na hukumu zisizo na maana, bila kulazimisha kwa mamlaka na kwa nguvu, bila kupoteza imani katika matendo ya Mungu.  Kama alivyokuwa akisema wakati huo Kardinali Ratzinger: “hii ni kuhusu kujisalimisha katika mantiki ya mbegu ambayo si ile ya mafanikio na ya ukuu, bali tunaomba kujifanya wadogo na kuhudumia maisha ya watu (Hotuba ya Mkutano na Makatekista na walimu wa dini(10 Desemba 2000). Kwa njia hiyo, sisi wenyewe tutakuwa kama mbegu ndogo ya Injili ambayo inachipua na kama chachu ya upendo ambao unabadilisha unga wa Ulimwengu.” Kwa huhitimisha Papa Leo XIV alisema “Tusali kwa Maria Mtakatifu, ambaye alitambua kukaribisha mbegu ya Neno katika udogo , ili yeye atusaidie katika safari na kutuombea sisi.”

Papa aliwazungukia waamini huko Castel Gandolfo
Papa aliwazungukia waamini huko Castel Gandolfo   (@Vatican Media)
TAFAKARI PAPA JULAI 20

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.

19 Julai 2026, 12:25