Papa Leo XIV:"Kutoa ushuhuda wa umoja,wa furaha na halisi!
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Leo XIV katika fursa ya kumbukizi ya Miaka 70 ya Baraza la Umoja wa Wakuu wa Mashirika ya kiume nchini Marekani alituma ujumbe kwa Padre Frank Donio, S.A.C. Mkurugenzi Mkuu wa Baraza hilo, ili kueleza alivyofahamishwa kwa furaha kuhusu hafla hiyo wanayoadhimisha wakati wa Mkutano mkuu wao unaofanyika huko Phoenix, Arizona, na anawatumia matashi yake mema wote wanaoshiriki.
Kuchangia kuongeza nguvu ya ushuhuda wa umma kwa waliowekwa wakfu
Papa Leo XIV anaandika kwamba “Katika kusheherekea miaka sabini ya kuhamasisha ushirikiano kati ya watawa wa kiume huko Marekani, ni fursa ya kutoa shukrani Mungu kwa neema walizopokea wakati wa miaka hii. “Katika juhudi zao za kutoa nafasi kwa ajili ya mazungumzo na usaidizi wa uongozi wa jumuiya ambazo wanashiriki Baraza, walichangia kuongeza nguvu ya ushuhuda wa umma kwa waliowekwa wakfu ambao wanaishi maisha yao huku wakijikita katika huduma ya Injili.”
“Wamoja katika Kristo: Maisha ya Jumuiya leo hii”
Papa aidha anabainisha kwamba, “kwa kutafakari mada ya mkutano wa mwaka huu “Wamoja katika Kristo: Maisha ya Jumuiya leo hii,’ “ninapenda kuwatia moyo kufikiria maisha ya jumuiya kama sehemu ya kujitakatifuza na chanzo cha kuchota msukomu, ushuhuda na nguvu katika utume (Hotuba kwa Mashirika manne ya Kitawa mnamo Septemba 18, 2025). Kiukweli, ni kwa njia ya kishirikishana wema wote, ukijumuisha mali zote, uzoefu wa kiroho, mawazo ya kitume na huduma ya upendo, ambapo uwepo uliojificha katika Bwana mfufuka unajionesha katikati yenu”(Mtakatifu Yohane Paulo II, Wosia wa kitume baada ya Sinodi –‘Vita consecrata,’ n. 42).”
Kuchanganua kwa kina ushirika wa kidugu
Papa Leo XIV anaamini kwamba “siku hizi za tafakari, mazungumzo na sala vitawaruhusu kuchang’anua namna ya kutafakari kwa kina, ushirika wa kidugu, uwe wa ndani ya Taasisi zao, na uwe kati yao , na hivyo kuweza kuendelea kutoa ushuhuda wa umoja, furaha na wa kweli wa Kristo katika jumuiya tofauti na katika utume wao mbalimbali, ambao wanautoa. Kwa hisia hizo anawahakiishia “ukaribu wangu wa kiroho na ninawakabidhi Mkutano wa Kitaifa kwa upendo wa maombezi Mwenyeheri Bikira Maria, Mama wa Kanisa.” Hatimaye Papa Leo XIV kwa wote wanawapatia kwa moyo wote “Baraka za kitume na kuzipanua kwa utashi kwa wajumbe wa Mashirika yao, mahali wanapotoa huduma.” Ujumbe wa Papa Leo XIV unahitimishwa uliotiwa saini mjini Vatican, tahere 16 Julai 2026 ambao umechapishwa, Julai 22, 2026.
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.
