Tafuta

Papa Leo XIV:Tusisahau wale wanaoteseka na kufa na migogoro"

Mara baada ya sala ya Malaika wa Bwana,akiwa huko Castel Gandolfo alitoa wito kufuatia na vita na migogoro inayoendelea kwamba:"Tusiwasahau wale wanaoteseka na kufa kwa sababu ya migogoro,na pia tuongeze maombi yetu ya kila mara kwenye ahadi yetu ya ukarimu kwa ajili ya amani.”

Na Angella Rwezaula – Vatican.

“Tunaendelea kufuatilia kwa wasiwasi kinachoendelea katika nchi mbalimbali zilizoharibiwa na vita na vurugu.” Aliyasema hayo Baba  Mtakatifu Leo  XIV akiwa katika lango la Jumba la kitume huko Castel Gandolfo Dominika tarehe 19 Julai 2026. Mara baada ya Sala ya Malaika wa Bwana  alisema:  “wapendwa kaka na dada wakati ninapopumzika kwa siku chache, ninarudia salamu zangu na shukrani kwenu nyote, wakazi wa Castel Gandolfo, na ninawakaribisha kwa furaha mahujaji wanaowasili kutoka ulimwenguni kote!

Tusiwasahau wanaoteseka

Papa Leo XIV aliendelea na kutoa wito kuwa: “Tunaendelea kufuatilia kwa wasiwasi kinachoendelea katika nchi mbalimbali zilizoharibiwa na vita na vurugu. Tusiwasahau wale wanaoteseka na kufa kwa sababu ya migogoro, na pia tuongeze maombi yetu ya kila mara kwenye ahadi yetu ya ukarimu kwa ajili ya amani.”

Papa wakati wa sala ya Malaika wa Bwana
Papa wakati wa sala ya Malaika wa Bwana   (@Vatican Media)

Salamu

“Nawasalimu Jumuiya ya Cenacolo ya Mama Elvira, iliyokusanyika Saluzzo kwa ajili ya Sikukuu ya Uzima, Harakati ya Familia Mpya ya Harakati ya Focolare iliyokusanyika kwa ajili ya Shule ya Kimataifa, wanafunzi wa Mexico wanaoshiriki katika Shule ya Majira ya kiangazi APRA, na kikundi cha Ushirika wa Mtazamo wa Ulimwengu wa Kikatoliki.”

Kwa lugha ya kiingereza Papa ..alisema “Nawasalimu vijana wanachama wa Regnum Christi wanaoshiriki katika Kozi ya Kimataifa ya Malezi. Na pia nawasalimu wale wanaoshiriki katika "Hija ya Simba", wakiambatana na Askofu Anthony Percy, Askofu msaidizi kutoka Sydney, Australia.”

Waamini huko Castel Gandolfo
Waamini huko Castel Gandolfo   (@Vatican Media)

Na tena kwa lugha ya kiitaliano "Pia nawasalimu familia na watoto na Masista wa Upendo wa Mungu,  Roma, vijana kutoka Parokia ya Mtakatifu Salvatore huko Gerusalemme, Kikundi cha Vijana kutoka Parokia ya Mtakatifu Agostino wa Bovolenta, na mahujaji kutoka Chuo cha Liturujia cha Rzeszów.” Hatimaye Papa Leo XIV aliwatakia wote Dominika njema yenye amani! Kabla ya kurudi ndani ya Jengo la kitume Papa Leo XIV  kwa kigari kidogo aliwasalimia watu akiwazungukia.

BAADA YA ANGELUS

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.

19 Julai 2026, 12:25