Papa Leo XIV: Dominika ya Utume wa Bahari: Mabaharia, Wavuvi na Wafanyakazi Bandarini
Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.
Mama Kanisa tarehe 12 Julai 2026 ameadhimisha Dominika ya Utume wa Bahari, fursa makini kwa Familia ya Mungu sehemu mbalimbali za dunia: Kumwomba, kumtukuza, kumsifu na kumshukuru Mungu, kwa huduma na mchango mkubwa unaotolewa na mabaharia pamoja na wavuvi kwa ajili ya ustawi, maendeleo na mafao ya watu wa Mungu. Ni siku maalum ya kutambua na kuthamini: mchango na sadaka ya watu hawa, ambao wakati mwingine, utu na heshima yao vinahatarishwa kutokana na changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo wakati wa kutekeleza dhamana na wajibu wao kwa jamii. Baba Mtakatifu Leo XIV, mara baada ya Sala ya Malaika wa Bwana, Dominika ya Utume wa Bahari, amewakumbuka: Mabaharia, wavuvi sanjari na wafanyakazi wa bandari, sehemu mbalimbali za dunia wanaokabiliana na changamoto ya kutenganishwa na wapendwa wao wakati wanapotekeleza dhamana na utume wao. Hawa ni watu wanaokabiliana na changamoto mbalimbali huko baharini, lakiini ni watu wenye mchango mkubwa katika kukuza na kudumisha biashara na maisha ya watu wengi, kupitia kazi yao inayosimikwa katika hali ya uvumilivu na utulivu.
Maadhimisho haya kwa Mwaka 2026 yananogeshwa na kauli mbiu: “Zaidi ya bidhaa na biashara: sura ya kibinadamu ya bahari” ni kauli mbiu inayokumbushia dhamana na wajibu mkubwa unaotekeleza na mabaharia na wavuvi sehemu mbalimbali za dunia. Mlango Bahari wa Hormuz (Strait of Hormuz) ni moja ya njia muhimu na nyeti zaidi za Bahari kwa uchumi na biashara ya kimataifa, kwani inakadiriwa kupitisha zaidi ya asilimia 20% ya mafuta na gesi asilia duniani. Kufungwa kwa Mlango wa Bahari wa Hormuz kunachochea mfumuko wa bei na kupunguza ukuaji wa uchumi wa Dunia na katika hali mbaya zaidi kusababisha ongezeko la umaskini kwa watu milioni 32 na njaa kali kwa watu zaidi ya milioni 45. Baraza la Kipapa la Maendeleo Fungamani ya Binadamu linasema, hii inaonesha ni kwa jinsi gani binadamu kwa asilimia kubwa anategemea huduma ya bahari kwa ajili ya ustawi, maendeleo na mafao ya wengi. Katika Maadhimisho ya Utume wa Bahari, Mama Kanisa anawakumbuka na kuwaombea mabaharia na wavuvi walioumbwa kwa sura na mfano wa Mungu; wana utu, heshima na haki zao msingi wanavyotekeleza dhamana na utume wao katika mazingira yenye matumaini na hofu, mizigo na ustahimilifu, mahusiano na ndoto zinazostahili kuonekana, kuheshimiwa, na kuthaminiwa.
Bahari, ambayo imewaunganisha watu na Mataifa kwa muda mrefu, inazidi kuwa na mvutano na kinzani; ukosefu wa usalama, vita, na hofu. Mabaharia na wavuvi sio tu kwamba wanapitia katika mazingira hatari ya bahari na njia za maji lakini pia hivi karibuni wameathiriwa na migogoro ya silaha ambayo imesababisha kufungiwa kwao kwenye meli, na haivyo kukumbana na: Uhaba wa chakula, na hata hofu ya maisha yao. Hii imeongeza hisia zao za upweke, kutengwa kwao na jamii kwa ujumla, kutengana kwao na wapendwa, na uchovu wao wa kihisia. Kwa kushangaza, hata katika enzi ya maendeleo makubwa ya mawasiliano ya kidijitali, mabaharia na wavuvi wengi bado wanaendelea kutengwa. Ule ukaribu wa kibinadamu unazidi kuwa nadra. Ni katika muktadha huu, mabaharia na wavuvi wanahitaji kuhisi uwepo, kutambua kwamba, wanakumbukwa, wanapendwa, wakakaribishwa na kusikilizwa. Waraka wa kwanza wa Kitume wa Baba Mtakatifu Leo XIV: “Magnifica humanitas” yaani: “Ubinadamu wa ajabu" Juu ya Hifadhi ya Mwanadamu Katika Enzi ya Teknolojia ya Akili Unde” unaonya kwamba, kamwe katika maendeleo makubwa ya teknolojia ya akili unde, kamwe binadamu asigeuzwe kuwa kama “mashini, takwimu au biadhaa” bali utu, heshima na haki zake msingi zinapaswa kuzingatiwa. Mabaharia na wavuvi ni kielelezo cha ushuhuda wa watu kutoka katika Mataifa, tamaduni na imani bado wana uwezo wa kujenga na kudumisha udugu wa kibinadamu, mshikamano, kwa kuheshimiana pamoja kuishi kwa amani. Kimsingi Bahari inapaswa kuwa ni daraja la kuwakutanisha walimwengu; watu kutoka katika Mataifa, tamaduni, dini na chumi mbalimbali na hivyo kutoa fursa ya ushirikiano na mshikamano; amani na utulivu na hivyo Mabaharia hawawezi kusahaulika na wala kuelemewa na upweke hasi. Walimwengu wanakumbushwa kwamba, Bahari ni sehemu ya kazi ya uumbaji, ambayo Mwenyezi Mungu amemkabidhi binadamu awajibike na kuitunza, kwani Bahari ni chemchemi ya lishe na ni nyumba ya wote. Inasikitisha kuona kwamba, leo hii bahari imegeuka kuwa ni shimo la takataka, ukwapuaji mkubwa wa rasilimali za dunia na matokeo yake ni uharibifu wa mazingira nyumba ya wote.
Baba Mtakatifu Leo XIV anakaza kusema, maendeleo ya binadamu hayana budi kuongozwa na kanuni ya: Utu, heshima, haki msingi za binadamu; ustawi, maendeleo na mafao ya wengi. Ni katika muktadha huu, ulinzi na tunza ya mazingira haina budi kwenda sanjari na ulinzi na tunza ya binadamu na kwamba, huu ni wajibu msingi wa kimaadili na utu wema, ili kujenga na kudumisha moyo wa ushirikiano na mshikamano, kwa ajili ya ustawi, maendeleo na mafao ya wengi, ili kulinda mazingira, utu, na heshima ya binadamu. Kristo Yesu katika Maandiko Matakatifu anawaalika wafuasi wake kamwe wasiogope, akiwepo kati yao, dhoruba inatulizwa bila shaka. “Akawaambia, Mbona mmekuwa waoga? Hamna imani bado? Mk 4:40. Hata leo hii, Kristo Yesu bado anaendelea kuambatana na mabaharia na wavuvi, wanaokabiliana na hali ya kutokuwa na uhakika wa usalama wa maisha yao, watu wanaokabiliana na uchovu, hatari mbalimbali sanjari na kutengwa na familia zao. Kwa kuwa Kanisa limeitwa kuendeleza utume wa Kristo Yesu ulimwenguni, nalo haliwezi kukaa mbali na hali halisi ya maisha ya wafanyakazi wa sekta ya bahari. Bwana, aliyepanda kwenye mashua pamoja na wanafunzi wake, anaendelea kuwa karibu na wale wanaosafiri baharini na kwenye njia za maji za ndani katika nyakati hizi; na Kanisa limeitwa kudhihirisha ukaribu huo kupitia uwepo wake na huduma yake. Limeitwa kupanda kwenye mashua: kuandamana, kusikiliza, kufariji, kutetea utu, heshima na haki msingi za binadamu, na kuwa ishara dhahiri ya matumaini na mahali pa kuhisi nyumbani katikati ya dhoruba za maisha ya mwanadamu. Kupitia huduma za kiroho bandarini, huduma kwa watu wa baharini, na uwepo wa kibinadamu wa unyenyekevu unaozingatia mapokeo ya muda mrefu ya Utume wa Bahari kwamba, wahusika wote wanakumbukwa, wanathaminiwa na kamwe hawako peke yao. Na kwamba hii ni huduma inayowakumbatia na kuwaambata watu wote wa Mungu.
Mama Kanisa anawashukuru na kuwapongeza wote wanaotoa huduma ya: Sala, huduma ya kichungaji na Sakramenti kwa mabaharia Wakatoliki ambao kimsingi ni sehemu kubwa ya wafanyakazi na maofisa wanaotua nanga zao za matumaini wanapofika bandarini, wakiwa mbali na nyumba, familia; na mahali pao pa kawaida pa Ibada. Baraza la Kipapa la Maendeleo Fungamani ya Binadamu linawashukuru mabaharia, wavuvi na wafanyakazi wote wa sekta ya bahari na familia zao sehemu mbalimbali za dunia, kwa kazi na utu wao na kwamba, dhabihu na sadaka zao zinategemeza biashara ya kimataifa, usalama na uhakika wa chakula; ustawi, maendeleo na mafao ya wengi. Baraza linawashukuru wahudumu wa maisha yao kwa uaminifu wao, kwa kujenga na kudumisha urafiki; kwa sala, usikilizaji na msaada wa hali na mali bandarini na katika meli sehemu mbalimbali za dunia. Dominika ya Utume wa Bahari ipyaishe ndani ya waamini wote azimio la dhati kabisa la kuwa karibu, kwa kushikamana, kwa kujali kazi ya uumbaji pamoja na watu wote wanaofanya kazi Baharini na kwenye njia za maji za ndani. Baraza linawakabidhi wote hawa mikononi mwa Bikira Maria, Nyota ya Bahari, kwa kuomba usalama, heshima, amani na matumaini kwa wote wanaosafiri na kufanya kazi majini. Mama Kanisa tarehe 12 Julai 2026 ameadhimisha Dominika ya Utume wa Bahari, fursa makini kwa Familia ya Mungu sehemu mbalimbali za dunia: Kumwomba, kumtukuza, kumsifu na kumshukuru Mungu, kwa huduma na mchango mkubwa unaotolewa na mabaharia pamoja na wavuvi kwa ajili ya ustawi, maendeleo na mafao ya watu wa Mungu. Ni siku maalum ya kutambua na kuthamini: mchango na sadaka ya watu hawa, ambao wakati mwingine, utu na heshima yao vinahatarishwa kutokana na changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo wakati wa kutekeleza dhamana na wajibu wao kwa jamii. Baba Mtakatifu Leo XIV, mara baada ya Sala ya Malaika wa Bwana, Dominika ya Utume wa Bahari, amewakumbuka: Mabaharia, wavuvi sanjari na wafanyakazi wa bandari, sehemu mbalimbali za dunia wanaokabiliana na changamoto ya kutenganishwa na wapendwa wao wakati wanapotekeleza dhamana na utume wao. Hawa ni watu wanaokabiliana na changamoto mbalimbali huko baharini, lakiini ni watu wenye mchango mkubwa katika kukuza na kudumisha biashara na maisha ya watu wengi, kupitia kazi yao inayosimikwa katika hali ya uvumilivu na utulivu.
Maadhimisho haya kwa Mwaka 2026 yananogeshwa na kauli mbiu: “Zaidi ya bidhaa na biashara: sura ya kibinadamu ya bahari” ni kauli mbiu inayokumbushia dhamana na wajibu mkubwa unaotekeleza na mabaharia na wavuvi sehemu mbalimbali za dunia. Mlango Bahari wa Hormuz (Strait of Hormuz) ni moja ya njia muhimu na nyeti zaidi za Bahari kwa uchumi na biashara ya kimataifa, kwani inakadiriwa kupitisha zaidi ya asilimia 20% ya mafuta na gesi asilia duniani. Kufungwa kwa Mlango wa Bahari wa Hormuz kunachochea mfumuko wa bei na kupunguza ukuaji wa uchumi wa Dunia na katika hali mbaya zaidi kusababisha ongezeko la umaskini kwa watu milioni 32 na njaa kali kwa watu zaidi ya milioni 45. Baraza la Kipapa la Maendeleo Fungamani ya Binadamu linasema, hii inaonesha ni kwa jinsi gani binadamu kwa asilimia kubwa anategemea huduma ya bahari kwa ajili ya ustawi, maendeleo na mafao ya wengi. Katika Maadhimisho ya Utume wa Bahari, Mama Kanisa anawakumbuka na kuwaombea mabaharia na wavuvi walioumbwa kwa sura na mfano wa Mungu; wana utu, heshima na haki zao msingi wanavyotekeleza dhamana na utume wao katika mazingira yenye matumaini na hofu, mizigo na ustahimilifu, mahusiano na ndoto zinazostahili kuonekana, kuheshimiwa, na kuthaminiwa. Bahari, ambayo imewaunganisha watu na Mataifa kwa muda mrefu, inazidi kuwa na mvutano na kinzani; ukosefu wa usalama, vita, na hofu. Mabaharia na wavuvi sio tu kwamba wanapitia katika mazingira hatari ya bahari na njia za maji lakini pia hivi karibuni wameathiriwa na migogoro ya silaha ambayo imesababisha kufungiwa kwao kwenye meli, na haivyo kukumbana na: Uhaba wa chakula, na hata hofu ya maisha yao. Hii imeongeza hisia zao za upweke, kutengwa kwao na jamii kwa ujumla, kutengana kwao na wapendwa, na uchovu wao wa kihisia. Kwa kushangaza, hata katika enzi ya maendeleo makubwa ya mawasiliano ya kidijitali, mabaharia na wavuvi wengi bado wanaendelea kutengwa. Ule ukaribu wa kibinadamu unazidi kuwa nadra. Ni katika muktadha huu, mabaharia na wavuvi wanahitaji kuhisi uwepo, kutambua kwamba, wanakumbukwa, wanapendwa, wakakaribishwa na kusikilizwa.
Waraka wa kwanza wa Kitume wa Baba Mtakatifu Leo XIV: “Magnifica humanitas” yaani: “Ubinadamu wa ajabu" Juu ya Hifadhi ya Mwanadamu Katika Enzi ya Teknolojia ya Akili Unde” unaonya kwamba, kamwe katika maendeleo makubwa ya teknolojia ya akili unde, kamwe binadamu asigeuzwe kuwa kama “mashini, takwimu au biadhaa” bali utu, heshima na haki zake msingi zinapaswa kuzingatiwa. Mabaharia na wavuvi ni kielelezo cha ushuhuda wa watu kutoka katika Mataifa, tamaduni na imani bado wana uwezo wa kujenga na kudumisha udugu wa kibinadamu, mshikamano, kwa kuheshimiana pamoja kuishi kwa amani. Kimsingi Bahari inapaswa kuwa ni daraja la kuwakutanisha walimwengu; watu kutoka katika Mataifa, tamaduni, dini na chumi mbalimbali na hivyo kutoa fursa ya ushirikiano na mshikamano; amani na utulivu na hivyo Mabaharia hawawezi kusahaulika na wala kuelemewa na upweke hasi. Walimwengu wanakumbushwa kwamba, Bahari ni sehemu ya kazi ya uumbaji, ambayo Mwenyezi Mungu amemkabidhi binadamu awajibike na kuitunza, kwani Bahari ni chemchemi ya lishe na ni nyumba ya wote. Inasikitisha kuona kwamba, leo hii bahari imegeuka kuwa ni shimo la takataka, ukwapuaji mkubwa wa rasilimali za dunia na matokeo yake ni uharibifu wa mazingira nyumba ya wote. Baba Mtakatifu Leo XIV anakaza kusema, maendeleo ya binadamu hayana budi kuongozwa na kanuni ya: Utu, heshima, haki msingi za binadamu; ustawi, maendeleo na mafao ya wengi. Ni katika muktadha huu, ulinzi na tunza ya mazingira haina budi kwenda sanjari na ulinzi na tunza ya binadamu na kwamba, huu ni wajibu msingi wa kimaadili na utu wema, ili kujenga na kudumisha moyo wa ushirikiano na mshikamano, kwa ajili ya ustawi, maendeleo na mafao ya wengi, ili kulinda mazingira, utu, na heshima ya binadamu. Kristo Yesu katika Maandiko Matakatifu anawaalika wafuasi wake kamwe wasiogope, akiwepo kati yao, dhoruba inatulizwa bila shaka. “Akawaambia, Mbona mmekuwa waoga?
Hamna imani bado? Mk 4:40. Hata leo hii, Kristo Yesu bado anaendelea kuambatana na mabaharia na wavuvi, wanaokabiliana na hali ya kutokuwa na uhakika wa usalama wa maisha yao, watu wanaokabiliana na uchovu, hatari mbalimbali sanjari na kutengwa na familia zao. Kwa kuwa Kanisa limeitwa kuendeleza utume wa Kristo Yesu ulimwenguni, nalo haliwezi kukaa mbali na hali halisi ya maisha ya wafanyakazi wa sekta ya bahari. Bwana, aliyepanda kwenye mashua pamoja na wanafunzi wake, anaendelea kuwa karibu na wale wanaosafiri baharini na kwenye njia za maji za ndani katika nyakati hizi; na Kanisa limeitwa kudhihirisha ukaribu huo kupitia uwepo wake na huduma yake. Limeitwa kupanda kwenye mashua: kuandamana, kusikiliza, kufariji, kutetea utu, heshima na haki msingi za binadamu, na kuwa ishara dhahiri ya matumaini na mahali pa kuhisi nyumbani katikati ya dhoruba za maisha ya mwanadamu. Kupitia huduma za kiroho bandarini, huduma kwa watu wa baharini, na uwepo wa kibinadamu wa unyenyekevu unaozingatia mapokeo ya muda mrefu ya Utume wa Bahari kwamba, wahusika wote wanakumbukwa, wanathaminiwa na kamwe hawako peke yao. Na kwamba hii ni huduma inayowakumbatia na kuwaambata watu wote wa Mungu. Mama Kanisa anawashukuru na kuwapongeza wote wanaotoa huduma ya: Sala, huduma ya kichungaji na Sakramenti kwa mabaharia Wakatoliki ambao kimsingi ni sehemu kubwa ya wafanyakazi na maofisa wanaotua nanga zao za matumaini wanapofika bandarini, wakiwa mbali na nyumba, familia; na mahali pao pa kawaida pa Ibada. Baraza la Kipapa la Maendeleo Fungamani ya Binadamu linawashukuru mabaharia, wavuvi na wafanyakazi wote wa sekta ya bahari na familia zao sehemu mbalimbali za dunia, kwa kazi na utu wao na kwamba, dhabihu na sadaka zao zinategemeza biashara ya kimataifa, usalama na uhakika wa chakula; ustawi, maendeleo na mafao ya wengi. Baraza linawashukuru wahudumu wa maisha yao kwa uaminifu wao, kwa kujenga na kudumisha urafiki; kwa sala, usikilizaji na msaada wa hali na mali bandarini na katika meli sehemu mbalimbali za dunia. Dominika ya Utume wa Bahari ipyaishe ndani ya waamini wote azimio la dhati kabisa la kuwa karibu, kwa kushikamana, kwa kujali kazi ya uumbaji pamoja na watu wote wanaofanya kazi Baharini na kwenye njia za maji za ndani. Baraza linawakabidhi wote hawa mikononi mwa Bikira Maria, Nyota ya Bahari, kwa kuomba usalama, heshima, amani na matumaini kwa wote wanaosafiri na kufanya kazi majini.
