Tafuta

PANAMA-POPE-WYD

Papa Leo XIV,vijana wa Chota ya Cutervo,Peru:Ninyi ni ujana wa Kristo&Tumeitwa,kutumwa kuhudumia"

“Jinsi gani ilivyo nzuri kujua kuwa kutoka Parokia 18 za Kanda,mmeunganika kwa ajili ya kushirikishana imani katika Yesu Kristo.”Ni katika ujumbe wa Papa Leo XIV kwa njia ya video kwa vijana waliounganika kwa siku ya vijana kijimbo huko Chota ya Cutervo nchini Peru.“Kanisa la Chota na Cutervo linahitaji kutoka kwenu mapinduzi matakatifu,nguvu zenu safi,shauku zenu za kubadili hali halisi ya uchungu katika nafasi za matumaini.”

Vatican News

Baba Mtakatifu Leo XIV alitume ujumbe wake kwa njia ya video  kwa vijana wa Kanda ya Chota na Cutervo nchini Peru. Katika ujumbe huo alisema: “kwangu ni furaha kubwa kuwaelekea ninyi nyote, mliunganika katika ardhi angavu ya Cutervo ili kuadhimisha Siku ya Vijana kijimbo.” Papa aliongeza: “Jinsi gani ilivyo nzuri kujua kuwa kutoka Parokia 18 za Kanda mmeunganika kwa ajili ya kushirikishana imani katika Yesu Kristo”

Kuitwa kupenda, kutumwa kuhudumia”

Baba Mtakatifu Leo XIV aidha alisema, “wapendwa vijana, ninyi ni ujana wa Kristo na kauli mbiu yenu  ya mwaka huu inaeleza wazi kabisa: “Tumeitwa  kupenda, kutumwa kuhudumia.” Yesu hataki vijana waliokaa katika sofa,” waliolala au kubaki na kasumba za “ tumezoea kufanya hivyo daima.”

Papa aliongeza  kuwa “Kanisa la Chota na Cutervo  linahitaji kutoka kwenu mapinduzi matakatifu, nguvu zenu safi, shauku zenu za kubadili hali halisi ya uchungu katika nafasi za matumaini. Kusikiliza wito wa kuwa wamisionari katika shule zenu, katika vyuo vikuu vyenu, katika barabara zenu  na katika vijiji vyenu.”

Ujumbe wa Papa kwa njia ya Video kwa vijana nchini Peru

Toeni huduma kwa furaha kwa waliosahulika

Kwa njia hiyo aliwaomba kwamba “Toeni huduma kwa furaha, hasa kwa waliosahulika zaidi, kwa sababu ni hapo ambapo panapatikana uso wa Yesu anayeteseka. Kwa kuhitimisha, Papa anawakabidhi kwa Maria, Mama Yetu Mpalizwa, Msimamizi wa Cutervo. “ Awalinde na kuwaongoza daaima.” “Siku Njema ! Na Mungu awalinde! Na Baraka ya Mungu Mwenyezi, Baba, Mwana na Roho Mtakatifu iwashukie ninyi, na ibaki nanyi daima. Amina.”

PAPA VIJANA WA CUTERVO PERU

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.

25 Julai 2026, 22:30