Papa Leo XIV huko Castel Gandolfo:kipindi cha mapumziko,sala na mazoezi
Vatican News
Bango lililofunikwa juu ya kwenye balcony ya Jumba la Kitume lilitangaza kuwasili kwa Papa Leo XIV kwa waamini waliokusanyika katika uwanja wa Castel Gandolfo. Baada ya ziara ya kichungaji ya Jumamosi tarehe 4 Julai 2026 huko Lampedusa na Sala ya Malaika wa Bwana Dominika tarehe 5 Julai katika Uwanja wa Mtakatifu Petro, Baba Mtakatifu Leo XIV, alasiri alikwenda hadi mji mwingine wa Lazio mahali palipo na Jumba la Kipapa. Huko Papa atapumzika hadi Jumatatu tarehe 27 Julai kama ilivyotangazwa katika taarifa kutoka kwa Nyumba ya Kipapa.
Mkutano daima ni wakati muhimu
Akiwa kwenye dirisha kubwa la Jengo la makazi yake, alitoa maneno machache ili kurudisha furaha ya wakazi wa eneo hilo waliokuwa wakimsubiri kwa hamu kwa mwezi wa Julai, ambao kwa kawaida hutengwa kwa mapumziko kutoka ahadi zake.
Habari za jioni na jioni njema, Castel Gandolfo! haya yalikuwa maneno ya kwanza ya Papa. Asante. Ninafurahi sana kuwa hapa miongoni mwenu, kuweza kutumia Juma chache zijazo kwa kupumzika, kusali, kusoma, na pengine michezo hapa Castel Gandolfo! Mkutano daima ni wakati muhimu, kwa hivyo ninafurahi kwamba nyote mko hapa. Asante kwa makaribisho, asante kwa kuwa kaka na dada.
Sala ya Papa
Mbele ya umati uliokuwa ukipiga kelele ya kumkaribisha "Karibu" na kupiga makofi, Papa Leo XIV alitoa baraka zake, huku akiwaalika kukutana nao katika sala ya Malaika wa Bwana Domika ijayo na labda "wakati mwingine."
Nawahakikishia maombi yangu, daima, lakini hasa katika juma zijazo...Mungu awe nanyi daima!
![]()
Huko Castel Gandolfo Papa Leo XIV atapumzika hadi Julai 27 (@Vatican Media)
Papa Leo XIV alimsalimia Padre wa Parokia na Parokia ya Mtakatifu Tommaso wa Villanova, ambapo aliadhimisha Misa mnamo tarehe 13 Julai 2025. Katika kipindi hiki cha mapumziko, Katekesi zote zimesimamishwa, ambazo zitaanza tena Jumatano, tarehe 5 Agosti 2026, pamoja na mikutano ya kibinafsi na maalum. Wakati sala ya Malaika wa Bwana, ijayo itafanyika katika Uwanja wa "Pizza della Libertà yaani 'Uwanja wa Uhuru' huko Castel Gandolfo,"
![]()
Waamini wakiwa katika Uwanja wa Uhuru wakimsalimia Papa(@VATICAN MEDIA)
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.
