Tafuta

Waraka wa Kitume wa Papa Leo XIV wa Magnifica Humanitas. Waraka wa Kitume wa Papa Leo XIV wa Magnifica Humanitas.  (ANSA)

Papa:Magnifica humanitas,kuanzia matumizi mabaya ya AI hadi manufaa ya wote!

Katika ujumbe uliosainiwa na Katibu Mkuu wa Vatican,Kardinali Pietro Parolin wakati wa Mkutano Mkuu wa Kimataifa wa matumizi bora ya AI 2026,Papa Leo XIV,alisisitiza nia ya Vatican ya kushiriki katika mazungumzo wakati wa "mabadiliko ya enzi" yanayosababishwa na teknolojia mpya.Katika muktadha huo alisisitiza pia hitaji la kutambua "njia mpya kwa ajili ya manufaa ya wote."

Vatican News

Katika ujumbe uliochapishwa tarehe 8 Julai 2026 wa Baba Mtakatifu Leo XIV, uliosainiwa na Katibu Mkuu wa Vatican, Kardinali Pietro Parolin, wakati wa Mkutano Mkuu wa Kimataifa kuhusu Matumizi bora ya AI 2026, ulioandaliwa na Umoja wa Kimataifa wa Mawasiliano (ITU), kwa ushirikiano na mashirika mengine ya Umoja wa Mataifa, na pamoja na serikali ya Uswiss anabainisha kuwa, “Sauti na ripoti zinazotia wasiwasi zinarejea kupotea kwa uhuru wa kibinadamu katika maeneo muhimu sana, kama vile teknolojia mpya. Kusikia sauti hizi kumesababisha hitaji la haraka la Waraka wa Kitume unaozungumzia mada ya akili unde na ulinzi wa mwanadamu wakati wa mabadiliko ya enzi."

Kusikiliza Mwongozo wa Teknolojia Mpya

Tukio hilo, lililozinduliwa Julai 7 na linaendelea hadi tarehe 10, huku likichunguza baadhi ya masuala muhimu zaidi ya wakati wetu, na linachochewa na hitaji la mazungumzo ambayo hayamzuii mtu yeyote, ili tuweze "kutambua njia mpya kwa manufaa ya wote na kukuza maisha yenye heshima kwa wote." Magnifica Humanitas, Waraka ambao Papa Leo XIV aliutoa  kwa mada hii, ulizaliwa kutokana na kuwasikiliza wanasayansi na wahandisi wanaofanya kazi "kwa shauku ya dhati kuhusu teknolojia zinazoweza kupunguza mateso makubwa"; kwa viongozi wa kisiasa na wasimamizi wa umma ambao "wametafuta kwa bidii kanuni za usawa"; na kwa wazazi na walimu wanaojali sana mustakabali wa vizazi vichanga.

Hata hivyo, pia ilisababishwa na historia zenye kusumbua sana kuhusu matumizi mabaya ya mashine na kupotea kwa uhuru wa kibinadamu katika maeneo muhimu. Ujumbe wa Papa unahitimishwa  kwa kuhawakikishia kuwakumbuka katika sala kwa ajili ya "mabadilishano yenye kujenga na yenye matunda" katika kujitolea kwao "kwa ajili ya huduma ya ubinadamu."

Ujumbe wa Papa Mkutano kuhusu AI

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.

08 Julai 2026, 12:26