Tafuta

Tetemeko la Ardhi nchini Colombia Tetemeko la Ardhi nchini Colombia 

Papa ametuma msaada wa fedha katika maeneo yaliyokumbwa na Tetemeko huko Colombia

Mara baada ya Katekesi yake,Agosti 12,mawazo ya Papa Leo XIV yaliwaelekea wathiriwa na majeruhi wa tetemeko kali la ardhi lililosababisha vifo vya mamia ya watu na uharibifu mkubwa wa miundo mbinu.Kupitia Ofisi ya Misaada ya Papa,iliwasisha moja kwa moja katika Ubalozi wa Papa na Baraza la Maaskofu mchango wa haraka ili kusaidia majimbo yaliyoathiriwa zaidi.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Mwishoni mwa salamu zake kwa waamini wanaozungumza lugha ya Kihispania, mara tu  baada ya Katekesi yake Jumatano  tarehe 12 Agosti  2026, Baba Mtatakatifu Leo XIV alionesha tena "ukaribu" wake na "kaka  na dada zetu wa Colombia ambao wameteseka kutokana na tetemeko la ardhi la hivi karibuni, ambalo lilisababisha waathiriwa na majeraha mengi, pamoja na uharibifu mkubwa wa mali."

Huku akimwomba Bwana "kwa ajili ya pumziko la milele kwa marehemu," Papa Leo  XIV pia alihakikisha sala zake kwa ajili ya familia za marehemu na wale wanaopamabania maisha yao, na "kwa wote walioathiriwa na msiba huu." Kwa kuongezea alisema “Ninatoa shukrani zangu kwa wale wote waliofanya kazi katika shughuli za kutoa misaada na kuwasaidia waathiriwa."

Ukaribu wa Papa Leo XIV na msaada wa dhati

Ukaribu wa Papa Leo XIV uliwaendea wote ambao wako katikati ya vifusi na vumbi la Colombia, lililoharibiwa na tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 7.4 lililotikisa sehemu ya magharibi ya nchi. Ukaribu wa Papa unachukua umbo la nyenzo na mgao wa kwanza wa haraka wa fedha zilizotumwa na Papa kupitia Baraza la Kipapa la Huduma ya Upendo - Ofisi ya Misaada ya Kitume.  Fedha hizo zitatengwa kwa majimbo yaliyoathiriwa na tetemeko la ardhi, kutokana na mawasiliano ya mara kwa mara ya Mwenyekiti wa Baraza hilo, Askofu Mkuu Luis Marín de San Martín, na Balozi wa Vatican nchini Colombia pamoja na Baraza la Maaskofu mahalia.

Papa akitoa Baraka
Papa akitoa Baraka   (@Vatican Media)

Uharibifu wa Kanisa

"Picha ya mfano wa haya yote ilikuwa Kanisa Kuu la Manizales, ishara muhimu sana ya eneo hili la nchi, la mtindo wa Ki Gothic, ambalo lilipata uharibifu mkubwa. Haya yalisema katika mahojiano na Vatican na Askofu José Miguel Gómez Rodríguez, mkuu wa Manizales huko Colombia, baada ya tetemeko la ardhi la ukubwa wa 7.4 lililotokea Agosti 10, ambalo lilisababisha vifo vya zaidi ya watu 200 na kusababisha mamia ya vifo vya watu, kulingana na ripoti rasmi za hivi karibuni.

Baada ya Katekesi Agosti 12

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku. Just click here.

12 Agosti 2026, 11:47