Tafuta

Uwanja wa Mtakatifu Petro na njia ya Conciliazione mahali ambapo kuna makao makuu ya  Kamati ya Kipapa ya Sayansi ya Kihistoria. Uwanja wa Mtakatifu Petro na njia ya Conciliazione mahali ambapo kuna makao makuu ya Kamati ya Kipapa ya Sayansi ya Kihistoria. 

Papa Leo XIV ateua wajumbe watatu wapya wa Kamati ya Kipapa ya Sayansi ya Historia

Hawa ni wanahistoria Umberto Longo,mkurugenzi wa Taasisi ya Kihistoria ya Italia ya Zama za Kati, Roma,Italia;Francesco Cesareo,rais mstaafu wa Chuo Kikuu cha Kupalizwa huko Worcester,Marekani;na Anna Barańska,Profesa msaidizi katika Kitivo cha Binadamu katika Chuo Kikuu Katoliki cha Lubelski Jana Pawła II (Poland).

Vatican News

Alhamisi tarehe 13 Agosti 2026, Papa Leo XIV aliwateua maprofesa wafuatao katika Kamati ya Kipapa ya Sayansi ya Kihistoria: Umberto Longo, Mkurugenzi wa Taasisi ya Kihistoria ya Italia ya Enzi za Kati, jijini Roma, Italia; Francesco Cesareo, rais mstaafu wa Chuo Kikuu cha Kupalizwa huko Worcester, Marekani; Anna Barańska, profesa msaidizi katika Kitivo cha Binadamu katika Chuo Kikuu Katoliki cha Lubelsk,Jana Pawła II (Poland).

Safari iliyoanza zaidi ya miaka 70 iliyopita

Kamati ya Kipapa ya Sayansi ya Kihistoria ilianzishwa mwaka 1954 na Papa Pio XII, ikirithi utamaduni wa Tume ya Msingi wa Masomo ya Kihistoria, iliyoanzishwa na Papa Leo XIII kwa Barua ya Kitume ‘Saepenumero considerantes’ ya mnamo tarehe 18 Agosti 1883.

Kazi ya Kamati ina sifa ya kuzingatia mara kwa mara urithi wa kumbukumbu za kikanisa, hasa Kumbukumbu za Vatican. Wito mwingi umeelekezwa na Mapapa ili kuruhusu wasomi kushauriana zaidi na ubora zaidi kuhusu makusanyo ya kumbukumbu zinashirikishwa na Vatican.

PAPA ATEUA WAJUMBE WA KAMATI YA KIPAPA YA HISTORIA

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku. Just click here.

 

13 Agosti 2026, 16:17