Papa Leo XI awaombea wanaoteseka duniani na hasa Wakristo wanaobaguliwa!
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Leo XIV akiwa huko Nyumba ya Kipapa la Castel Gandolfo, katika Siku ya Sherehe ya Bikira Maria Mpalizwa Mbinguni, na mara baada ya Misa Takatifu katika Kanisa Parokia ya Mtakatifu Thomas wa Vila Nuova, vile vile aliongoza Tafakari na sala ya Malaika wa Bwana.
Jumuiya zinazohitaji kufarijiwa
Mara baada ya Sala hiyo, Mawazo ya Papa yaliekezwa kwa ulimwengu mzima ambapo alisema:” Leo ninapendelea kumwomba maombezi yake ya kimama kwa niaba ya Jumuiya ambazo zinahitaji kufarijiwa na kuendelea kuwa na matumaini. Ninawafikiria kaka na dada zetu katika Nchi Takatifu, ambayo pia ni Nchi ya Maria bora kabisa. Ninawafikiria watu wa Ukraine na Urusi, wote wakiwa wamefungamana na ibada ya kifamilia kwa Mama Mtakatifu wa Mungu.
Wakristo wanaobaguliwa
Papa Leo XIV aidha alisema pia ninafikiria "Wakristo wanaobaguliwa au hata mateso na kuomba katika siku hizi kwa ajili ya watu wa Colombia wanaoteseka kutokana na tetemeko la ardhi." Papa alisema: “Bikira aliyepalizwa katika utukufu wa mbinguni, ni ishara ya tumaini na faraja kwa watu wote wa Mungu," na kwa sababu hiyo liongeza: Ninaungana na jumuiya hizi na wale wote wanaoishi katika hali ngumu, na pamoja nao naomba: "Maria Mtakatifu, utuombee!"
Mapumzko mema na kuwasiliana na maumbile
Zaidi ya salamu kwa umati, lilikuwa ni tumaini ambalo Papa alihitimisha huku akiwaalika wote kuonana Dominika na kwamba "kila mtu aweze kupata wakati wa kupumzika, kurejesha mwili na roho, pia kwa kusoma vizuri na kuwasiliana na maumbile."
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku. Just click here.
