Papa Leo XIV:"Huzuni kubwa na sala”kwa ajili ya waathiriwa wa tetemeko la ardhi nchini Colombia
Vatican News
Katika telegramu iliyosainiwa na Katibu Mkuu wa Vatican, Kardinali Pietro Parolin, Baba Mtakatifu Leo XIV alionyesha "huzuni wake mkubwa" kutokana na habari za tetemeko la ardhi la ukubwa wa kipimo cha 7.4 lililoikumba nchi ya Colombia tarehe 10 Agosti 2026, na kusababisha vifo na majeruhi ya mamia na uharibifu mkubwa wa miundombinu katika miji kadhaa na makanisa mengi. Papa pia aliwahakikishia sala kwa ajili ya marehemu na "kwa ajili ya kupona haraka kwa wale walioathiriwa na msiba huu."
Shukrani kwa waokoaji
Kupitia Askofu Mkuu Francisco Javier Múnera Correa, wa Jimbo Kuu la Cartagena na Rais wa Baraza la Maaskofu wa Colombia, ambaye ujumbe huo unaelekezwa kwake, Papa anatoa "rambirambi zake za dhati" kwa familia zote zinazoomboleza kutokana na "kupoteza wapendwa wao" na anaelezea "ukaribu wake wa kiroho" na "shukrani" kwa wale wote ambao, kwa "kujitolea kwa ukarimu," wanashiriki katika shughuli za utafutaji, uokoaji, na usaidizi kwa wale walioathiriwa.
Nguvu na Matumaini
Mwishoni mwa telegramu, Askofu wa Roma, kupitia maombezi ya Mama wa Mungu, anaomba kumiminwa kwa "nguvu ya kiroho" na "tumaini la Kikristo" kwa watu wa Colombia na kuwapa tia baraka zake za kitume.
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku. Just click here.
