Tafuta

2021.09.19 Mkutano huko Warsaw, Poland: Kardinali  O'Malley katika siku ya kwanza ya Mkutano huo. 2021.09.19 Mkutano huko Warsaw, Poland: Kardinali O'Malley katika siku ya kwanza ya Mkutano huo. 

Mkutano Warsaw juu ya nyanyaso:jitihada za pamoja na ukaribu wa wahanga

Mara baada ya salamu na hotuba ya Askofu Mkuu Stanisław Gądecki rais wa Baraza la maaskofu Poland na ujumbe wa Papa Francisko,ilifuata hotuba ya Kardinali Seán Patrick O'Malley katika Mkutano wa Kimataifa juu ya ulinzi wa watoto na watu wazima waathirika katika Makanisa ya Ulaya ya Kati na Mashariki.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Jumapili tarehe 19 Septemba 2021 umefunguliwa Mkutano wa kimataifa kuhusu ulinzi wa watoto na watu wazima waathiriwa wa nyanyaso ya kijinsia huko Warsaw nchini Poland. Mkutano huo unaongozwa na mada “Utume wetu wa kulinda watoto wa Mungu”. Papa Fancisko alituma ujumbe wake katika ufunguzi huo wa mkutano kanda ya Ulaya ya Kati na Mashariki, nchini Poland. Katika tukio hilo Papa amewataka washiriki kujikita kwa dhati katika kufanikisha upatikanaji wa njia thabiti ya mageuzi na hasa uongofu wa kichungaji. Kanisa Katoliki limekuwa katika mtikisiko mwingi  baada ya kukumbwa na mfululizo wa kashfa za manyanyaso ya kijinisia kwa upande wa makleri.Papa Francisko aliznisha Tume hiyo maalum kwa ajili ya shughuli hi ina ambayo imeanza kufanya matendo yake ya dhati ya usikilizaji wa dhati kwa wajhanga na kutafuta namna ya uponeshaji wa ndani.  Mara baada ya salamu na hotuba ya Askofu Mkuu Gądecki, limefuatia neno kutoka kwa Kardinali Seán Patrick O'Malley, Rais wa Tume ya Kipapa kwa ajili ya Ulinzi wa Watoto. Kardinali amesisitiza juu ya mada ya ulazima wa uongofu kichungaji, na amesema kuwa hii ni mchakto wa safari muhimu ambayo Papa Francisko anaiita kuwa  ni mabadiliko kimisionari kwa Kanisa.

Katika Mchakato huo wa uongofu kwa kutambua ukweli wa kile ambacho kilitokea, ni lazima uanzie katika moyo ambao unasikiliza. Watu ambao walio wasikiliza shuhuda za wahanga, wanatambua jinsi gani uzoefu huu ulivyo mgumu na unawakilisha changamoto.   Yeye binafsi amethibitisha jinsi alivyo kutana na mamia ya wahanga. Shuhuda zao zinaumiza sana hasa wanapoeleza kuwa hakuna ambaye aliwaamini wakati waliripoti unyanyasaji huo kwa mara ya kwanza. Kardinali O’Malley aidha alizungumzia heshima kubwa ambayo lazima waipokee ya  ushuhuda wa watu ambao ni waathiriwa wa unyanyasaji. Mtu lazima pia kujua ukweli kwamba kuna watu wengi, ambao wamepata janga la unyanyasaji wa kijinsia Kanisani, ambao hawajawahi kumwambia mtu yeyote juu ya uzoefu wao. Ili kufikia uongofu wa kichungaji, watu ambao wametendwa vibaya lazima watambuliwe kwa uaminifu na kwa uwazi. Kusikiliza maumivu ya wengine, mateso ya watu wa Mungu hupelekea kukubali mabaya yaliyofanywa na mateso yaliyosababishwa. Na ni muhimu kuomba msamaha wa dhati waathirika. Lakini kuomba msamaha hakuhitaji chochote zaidi ya kutoa taarifa au kufanya mkutano. Ni mchakato ambao hufanyika mara chache kwa muda mfupi na wakati mwingine hautakamilika. Kuwasikiliza waathirika, kuwatambua na kuwaomba msamaha kwa dhati ni hatua muhimu katika njia hii ya upyaisho.

Shuhuda mbili za waathiriwa: Katika mpango wa siku ya kwanza ya Mkutano ilifuatia na shuhuda mbili ambapo ya kwanza Padre Tarsycjusz Krasucki alikumbaka tukio la mnamo mwaka 1993 akiwa katika nyumba ya Settino, kituo ambacho kilianzishwa na Padre Andrzej Dymer. Siku moja alimwendea mkurugenzi saa nne usiku katika ofisi yake ili kuzungumza naye. Lakini unyanyasaji ndimo ulipomkuta. Yote haya katika mazingira ya usaliti, kwani alijua kwamba ikiwa atasema basi angeweza kufukuzwa kutoka katika eneo hilo. Siku iliyofuata, Padri Krasucki aliwaambia vijana wenzake juu ya tukio hilo. Kutokana na majibu yao alielewa wazi kuwa hali kama hizo zilikuwa zimewapata wao pia. Miaka miwili baadaye, Padri Krasucki alijiunga na shirika la Wafransiskani. Mnamo 2003 mtawa huyo  alitoa ushuhuda wake huko Szczecin kwenye mchakato wa kisheria.

Ushuhuda mwingine ulikuwa ule wa mwanamke ambaye alisema alinyanyaswa na Padre. Alikumbuka vipindi vigumu kwake ambavyo vilifanyika wakati alikuwa mtoto katika nyumba ya babu na bibi yake. “Nakumbuka nilihisi kizunguzungu, kuchanganyikiwa, sikuelewa kabisa kilichotokea. Nimeishi maisha yangu nikiwa na aibu, nikiwajibika. Niliishi na unyogovu. Ndoa yangu iliishia kwa talaka”. Maisha yake pia yamefunuliwa kupitia matibabu ka miaka. “Nimehisi hali ya kuchanganyikiwa kwa muda mrefu. Sasa, sifuati dini yoyote. Nilipata njia yangu kwa Mungu na kiroho”.

20 September 2021, 16:07