Tafuta

Mkutano wa 65 wa Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomic  IAEA kufanyika kwa njia ya mtandao Mkutano wa 65 wa Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomic IAEA kufanyika kwa njia ya mtandao 

Vatican imetoa wito kwa IAEA kuunda dunia isiyo na silaha!

Katibu msaidizi wa Vatican Katika kitengo cha Mahusiano na Mataifa ametoa wito wa kipapa kwa viongozi wa dunia kuchukua wajibu kijasiri wa kufanya maamuzi ya kutumia fedha ambazo zingetumika kununua silaha kutoka katika mfuko wa ulimwengu ili ziweze kutumika kuondoa njaa na kuchangia maendeleo ya nchi maskini.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Kujenga ulimwengu usio na silaha za kinyuklia ndiyo kazi ya Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomic (IAEA) ilivyo kumbushwa Jumatatu tarehe 20 Septemba na Francesca Di Giovanni, Katibu msaidizi wa Vatican katika Kitengo cha katibu-chini wa sekta nyingi ya Mahusiano  na Ushirikiano na Mataifa.  Katika hotuba yake kwa njia ya Video kwenye Mkutano mkuu wa 65 wa IAEA unaondelea huko Vinenna hadi 24 Septemba, Di Giovanni alisema wito ni kusimamisha kuenea kwa silaha za kinyuklia na kufanya uwezekano wa teknolijia ya kinyuklia ya amani kwa manufaa ya ubinadamu wote. Vatican inatambua nafasi muhimu a Shirika hili kwa kile ambacho kinatazama k kutosambaa kwa silaha za nyuklia kupitia mpango wake wa ulinzi na kuhakikisha kuwa nyenzo za nyuklia hazielekezwi kutoka katika malengo ya amani. Kitendo ambacho pia kinategemea uaminifu, kwa upande wa mwakilishi wa Vatican alirudia, kusema kwamba “kwa sababu wakati nchi zinafungua mitambo yao ya nyuklia kwa wakaguzi, katika mfumo wa makubaliano ya ulinzi wa ulimwengu na itifaki za nyongeza, zinasaidia kujenga uaminifu na kupunguza tuhuma. Kwa njia hii, shirika hili linachangia kwa kiasi kikubwa kuunda ulimwengu bila silaha za nyuklia”

Kutoka kwa mwakilishi wa Vatican katika mkutano huo ndipo amekumbusha maneno ya Papa Francisko ambayo mara nyingi amelaani kueane kwa silaha za kinyuklia akizifananisha na suala ambalo hali maadili kwa sahabu zinaleta uharibifu mkubwa kwa namna ya pekee na kuunda usalama wa uongo kwa wale wanaozitumia. Kwa maana hiyo Katibu msaidizi ametoa wito wa kipapa kwa viongozi wa dunia kuchukua wajibu kijasiri wa kufanya maamuzi ya kutumia fedha ambazo zingetumika kununua silaha kutoka katika mfuko wa ulimwengu ili ziweze kutumika kuondoa njaa na kuchangia maendeleo ya nchi maskini. Kwa mtazamo wa Di Giovanni umempeleka hasa kwa maskini na watu walio katika mazingira magumu, hasa wale wanaoteseka kwa kiasi kikubwa na matuko ya janga la UVIKO-19, na kama ilivyo kwa wenye njaa, magonjwa na hali mbaya za mabadiliko ya tabianchi.

De Giovanna amebainisha kwamba wote wanalo jukumu la kuhamasisha utamaduni wa utunzaji ambao unaweka katikati hadhi ya binadamu na wema wa pamoja kwa kila chochote kifanyikacho. Aidha katika matazamio hayo Katibu msaidizi amepongeza jitihada za Vatican kwa ajili ya “Zodiac”, yaani Mpango wa matendo ya dhati ya Shirika hilo kwa ajili ya magongwa yanaoambukizwa kutoka kwa wanya ‘zoonotiche’. Mpango huo uliozinduliwa mnamo 2020, ambao unakusudia kuboresha mwingiliano kati ya wanasayansi, watunga sera na jamii, kukuza ushirikiano ili kugundua hatari na kushughulikia milipuko ya magonjwa ambayo hupita kutoka kwa wanyama kwenda kwa wanadamu, kwa lengo la kuhakikisha upatikanaji wa suluhisho kwa wote. Shukrani hiyo hiyo pia ilioneshwa na mwakilishi wa Vatican kwa mipango ya IAEA iliyowekwa kwa matumizi ya teknolojia ya nyuklia kudhibiti uchafuzi wa plastiki na kutibu saratani, kuhamasisha utuoaji wa chakula zaidi na kusimamia na kulinda akiba ya maji.

Mchango mkubwa zaidi, uliooneshwa na Di Giovanni alisema “Wakala hufanya katika maeneo ya mabadiliko ya tabianchi kufuatilia uchafuzi wa bahari na mifumo ya ikolojia, na kusaidia nchi kukabiliana na hali mpya ya tabianchi, pamoja na uhaba wa chakula na maji”. Kwa njia hiyo, alikumbusha a lengo la Vatican la kuhamasisha elimu katika ikolojia fungamani pamoja na hatua za kisiasa na kiufundi ambazo zinapendelea mfano wa utamaduni wa maendeleo uendelevu kulingana na udugu na muungano kati ya mwanadamu na mazingira.

21 September 2021, 17:30