Tafuta

Mji wa Vatican Mji wa Vatican 

Tangu Mosi Oktoba kuingia mjini Vatican na kadi ya kijani

Katika mkutano uliofanyika mnamo Septemba 7, Papa aliomba Serikali itoe agizo la kuchukua hatua zote zinazostahili ili kupambana na dharura ya kiafya ndani ya jiji la Vatican.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Ili kuweza kuingia katika jiji la Vatican, kuanzia Oktoba Mosi wataruhusiwa wale tu ambao wana kadi ya kijani (Green Pass) ya Vatican, ya Ulaya na cheti cha kijani cha UVIKO- 19, ambacho kinathibitisha chanjo au kupona kutoka katika SARS-Cov-2, au kufanya vipimo vya haraka na kuwa na matokeo hasi ya virusi vya SARS-Cov-2.  Hilo ndilo agizo la Rais wa Tume ya Kipapa ya Jiji la Vatican juu ya mada ya dharura ya afya ya umma. Ni uamuzi uliochukuliwa kutokana na pendekezo la Baba Mtakatifu Francisko, wakati wa mkutano wao mnamo Septemba 7, ili kuhakikisha afya na ustawi wa jamii inayofanya kazi wakati huo waki heshimu utu, haki na uhuru msingi wa kila mmoja wa washiriki wake na kupitisha kila hatua inayofaa ya kuzuia, kudhibiti kwa mujibu wa dharura ya kiafya.

Udhibiti wa mchakato wa kuingia katika jijini na  serikali ya Vatican, umekabidhiwa kwa Kikosi cha Ulinzi na usalama kama ilivyo andikwa: “Vifungu hivi vinahusu raia, wakaazi wa Vatican, wafanyakazi katika huduma, kwa sababu yoyote, katika Jiji la Vatican na katika Mashirika ya Kipapa na taasisi zilizounganishwa na wageni na watumiaji wa huduma”. Isipokuwa tu, maadhimisho ya kiliturujia kwa wakati muhimu katika utekelezaji wa ibada, ambapo mahitaji ya kuendelea kutunza afya lazima  kutunza umbali, matumizi ya vifaa vya kinga binafsi, mkusanyiko wa watu na kufuata kanuni na sheria maalumu za usafi zilizo elekezwa. Hatimaye, agizo linakumbusha kwamba Afya na Usalama wa Huduma ya Wafanyakazi mahali pa kazi ya Kurugenzi ya Afya na Usafi inafanya shughuli ya uthibitishaji.

21 September 2021, 16:48