Tafuta

Hija ya Kitume ya Papa Francisko Cyprus na Ugiriki:Mkutano na Hieronymos II

Papa Francisko akiwa Atene amekutana na Kiongozi mkuu wa Kiorthodox Patriaki Hieronymos II,Jumamosi alasiri tarehe 4 Desemba 2021.Video fupi na picha zinaonesha wakati muhimu wa tukio hilo la kihistoria katika kisiwa cha Ugiriki,kwenye ziara ya 35 ya kimataifa iliyoanza tarehe 2 Desemba.Papa ametoa mwaliko wa kutafuta umoja ambao unafanya kuaminika ushuhuda wa kikristo.

Na Sr. Angella Rwezaula – Vatican.

Papa Francisko Jumamosi alasiri tarehe 4 Desemba 2021 akiwa huko Atene mara baada ya asubuhi kufanya mikutano mingine na viongozi wakuu wa taasisi, kisiasa na kidiplomasia amekutana pia na Patriaki Hieronymos II, Mkuu wa Kanisa la Kiorthodox Ugiriki.

Papa akitia saini ya Kitabu cha Patriaki wa Ugiriki
Papa akitia saini ya Kitabu cha Patriaki wa Ugiriki
Ziara ya Papa Ugiriki
Ziara ya Papa Ugiriki
Ziara ya Papa Ugiriki
Ziara ya Papa Ugiriki

Mada zao kwa viongozi hawa wawili wamejikita juu ya Injili ambapo mara baada ya salamu na saini  Papa amehutubia akianza na maneno ya Mtakatifu Paulo mtume wa watu: “Neema na amani kwa Mungu” ambayo yalikuwa ni  yale yale yaliyotamkwa na mtme Paulo wakati alipokuwa katika ardhi ya Ugiriki. Papa Francisko amesema mkutano wao leo hii unapyaisha neema na amani ile ile na kwa maana hiyo amewaalikwa kutafuta umoja ambao unafanya kuaminika ushuhuda wa kikristo.

Ziara ya Papa Ugiriki: Papa akiwa na Patriaki wa Kiorthodox
Ziara ya Papa Ugiriki: Papa akiwa na Patriaki wa Kiorthodox
Ziara ya Papa Ugiriki: Papa akiwa na Patriaki wa Kiorthodox
Ziara ya Papa Ugiriki: Papa akiwa na Patriaki wa Kiorthodox

Video fupi na picha zinaonesha wakati muhimu wa tukio hilo la kihistoria katika kisiwa cha Ugiriki, kwenye ziara ya 35 ya kimataifa ya Papa Francisko aliyoanza tarehe 2 Desemba na itamalizika Jumatatu tarehe 6 Desemba 2021.

Papa akibusu Msalama katika kanisa Kuu la Mtakatifu Dionizi
Papa akibusu Msalama katika kanisa Kuu la Mtakatifu Dionizi
04 December 2021, 17:10