Tafuta

Kardinali Raniero Cantalamessa, Mhubiri wa Nyumba ya Kipapa. Kardinali Raniero Cantalamessa, Mhubiri wa Nyumba ya Kipapa. 

Kard.Cantalamessa:Wakati ulipowadia utimilifu,Mungu alimtuma Mwanae!

Katika tafakari ya kwanza kwa ajili ya majilo mwaka huu,mhubiri wa Nyumba ya Kipapa anataka kuweka nuru ya ndani ya Kanisa na maisha ya kikristo bila kufunga macho kuhusu uhalisia wa matendo ili kila mmoja aweze kukabiliana na uwajibikaji katika matarajio ya kweli.Mtakatifu Yohane Paulo II,katika barua ya Ekaristi,aliyoiandika muda mfupi kabla ya kifo alizungumza fumbo la Ekaristi ambalo Wakristo wanapaswa kugundua tena.

Na Sr. Angella Rwezaula – Vatican.

Padre Raniero Cantalamessa, ambaye ni mhubiri wa Nyumba ya Kipapa Ijumaa tarehe 3 Desemba 2021, katika tafakari yake ya kwanza ya Kipindi cha  Majilio amependekeza kutazama Kanisa kutoka ndani, kwa maana kubwa hasa katika nuru ya fumbo hilo ambalo linazaliwa na linalokaa ndani yake lisipotee. Mada ya tafakari iliyoandaliwa katika Ukumbi wa Paulo VI, mjini Vatican kwa kuudhuriwa na wahusika wa Viongozi wa Mabaraza ya Kipapa na wahudumu mbali mbali wa Vatican ilikuwa ni : “Wakati utimilifu ulipowadia, Mungu alimtuma Mwanae (rej. Wag 4  4-7 ) ambao ni muhtasari wa fumbo lote la Kikristo. Kardinali Cantalamessa amependa kuendeleza hata hivyo mchakato wa mahubiri yake ya Kwaresima iliyopita mwaka huu, ambayo alijaribu kuangazia hatari ya kuishi kwa mujibu wa Kristo na siyo kwenda kinyume'kana kwamba Kristo hayupo. Kardinali amesema: "Mbele ya kukabaliwa na hatari ya kuishi kana kwamba Kanisa lina kashfa, mabishano, migongano ya watu binafsi, masengenyo au kwa hakika sifa fulani katika nyanja ya kijamii kwa ufupi ni mambo ambayo yanatokea katika historia".

Mungu alimtuma mwanae ili sisi tuwe wana wa Baba yake

Katika tafakari hiyo Kardinali Cantalamessa amezungumzia sehemu ya kwanza ya maandiko ya Mtume wa Watu Paulo ambaye ataongoza kwa hakika mahubiri yake katika kipindi hiki cha Majilio. Mungu alimtuma Mwanae ili sisi sote  tuweze kuwa wana wa Mungu na kwamba ubaba wa Mungu huko moyoni mwake katika mahubiri ya Yesu. Na ikiwa katika Agano la Kale Mungu alionekana kama Baba, mapya ya Injili sasa Mungu haoekani sana kama baba wa watu wa Israeli tu, bali kama baba wa kila mwanadamu, mwenye haki au mdhambi na anamwangaikia kila mmoja kama wa kipekee. Kwa kila mmoja anajua mahitaji yake, mawazo yake hadi kufikia kuhesabu nywele za kichwa chake. Kwa maana hiyo kile ambacho Yesu anafundisha si tu kuwa aliumba mbingu na dunia na kutunza watu wake, lakini kabla ya hapo ni baba wa kweli na asili, mwenye mtoto wa kweli na asili ambaye aliumbwa naye. Kabla ya wakati na kwa neema hiyo watu wote wanaweza hata wao kuwa wana wa Mungu kwa maana ya kweli na wala si kwa mfano.

Yesu alitupatia jina na vinasaba

Padre Cantalamessa amebainisha kwamba kama fumbo la kifo na ufufuko wa Kristo,na neema ya ukombozi iliyotendwa na kutolewa kwetu kwa njia ya ubatizo, kama asemavyo Mtakatifu Paulo, sisi sote tumekuwa Wana katika Wana ambao Yesu Kristo amekuwa mzawa wa kwanza kati ya ndugu walio wengi. Kwa njia hiyo kuna haja ya kuelelewa vizuri uhusiano ambao alitupatia Kristo na kutimizwa kwa watu. Mfano huo hata hivyo unataka kueleza utimilifu wa fumbo. Hii ni kwa sababu, tendo la kuchukuliwa binadamu katika sheria na mtoto aliyechukuliwa anapata ubini, uraia na makao ya yule ambaye amemchukua, hata bila kushirikishana damu au vinasaba, na ndivyo inakuwa hata kwetu sisi. Yesu atupatia jina la kuwa watoto na  anatupatia maisha ya ndani, roho yake ambayo ndiyo tunaweza kusema ni vinasaba. Kwa ubatizo sisi tumegeuka kuwa na maisha sawa na Mungu.

Kubatizwa ni kuzaliwa upya: Wakristo hatugundui uhalisia wa kuwa wana 

Padre Cantalamessa akiendelea na tafakari hiyo amejikita kuelezea Mtakatifu Yohane ambaye anazungumza ukweli na uzao wa kwanza kwa Mungu na hivyo katika ubatizo linatimizwa tendo la kuzaliwa ambapo ni kuzaliwa upya kwa aliye juu. Ni muhimu kwa maana hiyo kama alivyosema Papa Francisko wakati wa Katekesi yake mnamo tarehe 8 Septemba 2021 kuwa: "Sisi  wakristo mara nyingi hatugundui uhalisia wa kuwa wana wa Mungu. Kinyume chake ni ni vizuri  kuwa na kumbu kumbu na kushukuru wakati tunapopokea ubatizo wetu, kwa kuishi na utambuzi zaidi wa zawadi kubwa tuliyojaliwa. Kwa kuangazwa na maneno yao, Kardinali Cantalamessa amebainisha:“Tazama hii ndiyo hatari yetu ya kufa: kutochukulia kwa uzito mambo makuu zaidi ya imani yetu, yakiwemo hata yale yale ya kutojali kuwa watoto wa Mungu, wa Muumba wa ulimwengu, wa Mwenyezi, wa milele na mleta uzima". Mtakatifu Yohane Paulo II, katika barua yake juu ya Ekaristi, aliyoiandika muda mfupi kabla ya kifo chake, alizungumza "juu ya fumbo la Ekaristi ambalo Wakristo wanapaswa kugundua tena. Vile vile lazima kusema juu ya wana wa kimungu: kupita kutoka katika imani hadi kufikia mshangao”.

Neema ya ubatizo ni kubwa na yenye utajiri

Katika Sakramenti ya ubatizo, sehemu ya Mungu au neema ya ubatizo ni kubwa mno na yenye utajiri, ameeleza Kardinali Cantalamessa. "Wana wa mungu, msamaha wa dhambi, kukaa katika Roho Mtakatifu, fadhila za kitaalimungu za imani, tumaini na mapendo vinaingizwa ndani ya roho, mchango wa mwanadamu, kwa upande mwingine ni imani. Lakini inahitaji imani ya mshangao, kwa kupanua macho kuona maajabu mbele ya karama ya Mungu, kufurahia ukweli wa mambo yanayoaminika na ladha ya kweli, ikiwa ni pamoja na ladha chungu ya ukweli wa msalaba". Kwa kifupi, ukweli unaoaminika lazima uwe halisi. Padre Cantalamessa amejiuliza: “Je, tunawezaje kuruka kwa namna gani ubora kutoka katika imani hadi kufikia mshangao wa kujua kwamba sisi ni watoto wa Mungu iwezekanavyo? Jibu lake, kwanza ni neno la Mungu! (Kuna njia ya pili muhimu katikati ambayo ni Roho Mtakatifu lakini tunaiacha kwa ajili ya tafakari inayofuata). "Mtakatifu Gregori Mkuu analinganisha Neno la Mungu na gumegume, yaani, jiwe ambalo hapo awali lilitumiwa kutoa cheche na kuwasha moto. Ilikuwa ni lazima,kufanya Neno la Mungu kile kinachofanywa kuwa jiwe gumu lipigwe tena na tena mpaka cheche zitokee. Kwa maana hiyo ni lazima neno litafunwe, kurudia kulisoma hata kwa sauti ya juu”.

Kukomaa kwa udugu wa ulinwengu pia ni kutomjaribu Mungu

Mwaliko kwa upande wa Kardinali Cantalamessa ni ule wa kusali ili kuwa na dhamiri ya kuwa wana wa Mungu na wenye hadhi sawa  za kikristo. Haya yote pia yatapelekea kutambua hadhi ya wengine, ambao pia ni wana na binti wa Mungu na ubaba wa Mungu kwa wanadamu wote. Kwetu sisi Wakristo, udugu wa kibinadamu una sababu yake kuu katika ukweli kwamba Mungu ni baba wa wote, kwamba sisi sote ni wana na binti wa Mungu na kwa hiyo kaka na dada kati yetu. Haiwezekani kuwepo na kifungo chenye nguvu zaidi kuliko hiki na kwetu sisi Wakristo ni sababu ya dharura zaidi ya kukuza udugu wa ulimwenguni kote. Kwa mujibu wa Mhubiri wa nyumba ya Kipapa, amesema kukomaa kwa udugu wa kiulimwengu pia unamaanisha kutomjaribu Mungu kwa kumwomba akubali sababu zetu dhidi ya ndugu zake, bila kutaka kuwa sawa na makosa mengine, kuhurumiana, jambo ambalo ni la lazima kwa ajili ya kuishi maisha ya Roho na ya jumuiya katika aina zake zote, kwa familia, kwa kila jumuiya ya kibinadamu, ya kitawa, ikiwemo pamoja na ya Sekretarieti ya Vatican. Hatimaye,amehitimisha tafakari yake akitumaini kwamba Maandiko Matakatifu yatasaidia kugundua maana halisi ya kuwa wana wa Mungu na sababu za haraka kwa ajili ya kuhamasisha udugu wa ulimwengu mzima.

03 December 2021, 15:09