Tafuta

2021.12.04 Mapango ya kuzaliwa kwa 100 kuoneshwa mjini Vatican. 2021.12.04 Mapango ya kuzaliwa kwa 100 kuoneshwa mjini Vatican. 

Tangu Desemba 5 hadi 9 Januari kuna maonesho ya mapango 100 jijini Vatican!

Katika nguzo za uwanja wa Mtakatifu Petro,zinawasha taa kwa mara nyingine tena kuwakilisha maonesho ya mapango 100 ya kuzaliwa kwa Bwana ambapo dunia nzima inashiriki kwa kutimiza kazi zilizoandaliwa na zana mahalia.Maonesho yameandaliwa na Baraza la Kipapa la kuhamasisha Uinjilishaji Mpya yanayozinduliwa kuanzia Dominika 5 Desemba 2021 hadi 9 Januari 2022.

Na Sr. Angella Rwezaula – Vatican.

Kwa njia ya tamasha ambalo linakumbusha muziki  na dansi ya Taiwan, ndiyo itazindua maonesha ya Mapango 100 kimataifa jijini Vatican mnamo Jumapili tarehe 5 Desemba 2021, yanayokusanya kazi mbali mbali za mafundi wengi wa ulimwengu nzima. Kutokana na janga la Uviko -19,maonesho hayo yanawekwa kwenye nguzo za Bernin katika uwanja wa Mtakatifu Petro kama walivyonesha hata mwaka 2020.

Dunia nzima iko Vatican

Mwaka huu mapango hayo ya Kuzaliwa kwa Bwana yatakuwa 126 kutoka katika mataifa mbali mbali ya Ulaya kama vile Ujerumani, Hungeria, Slovenia, Slovakia na Kroazia na katika ulimwengu ni pamoja na Kazakistan, Perù, Indonesia, Uruguay, Colombia na Marekani. Moja ya Nchi hizo tayari zina wakilishwa na ubalozi wao  Jiji la Vatican na ambao wanakabidhiwa wajibu huo wa kuhamasisha matukio mbali mbali ya Nchi.

Mapango asili

Mapango mengi asili ya kuzaliwa kwa Bwana yapo kama vile lililotengenezwa sehemu ya mbele ya Bus la chama cha Atac au  Pango la kuzaliwa kwa Bwana kwa kutumia chokoleti yenye uzito wa kilo 100, iliyofanywa na kampuni ya Choleti ya Trappisti. Hata shule 30 za Mkoa wa Lazio, Italia zimejiunga kwa furaha na mpango huo, kama kila mwaka na uandaaji wa kazi zilizoundwa na watoto. Pia kuna matukio ya mapango ya kuzaliwa kwa Bwana kutoka parokia za Roma. Mabaki kadhaa ambayo yanatengenezwa mapango ya kuzaliwa kwa Bwana: kutoka katika utengenezaji wa karatasi, hadi vitambaa, kutoka kwenye cork, hadi kuni.  Vile vile kuna hata ufumaji wa pango la kuzaliwa kwa Bwana unaowakilisha taswira ya mtaa mmoja wa Roma. Kwa maana hiyo maonesho hayo yatafunguliwa kwa wiki 5, tangu  Jumapili tarehe 5 Desemba 2021 hadi Jumapili 9 Januari 2022, kuanzia saa 4:00 asubuhi hadi 2:00, usiku kila siku. Maonesho hayo yanawezekana kwa shukrani hata kwa kampuni ya UnipolSai, ambayo iliunga mkono tukio hilo lifanyike.

04 December 2021, 16:09