Tafuta

2022.08.10 Kazakistan Nursultan 2022.08.10 Kazakistan Nursultan 

Mazungumzo na amani ni moyo wa ziara ya kitume ya Papa nchini Kazakhstan

Septemba 9,Msemaji wa Ofisi ya Habari ya Vatican aliwasilisha ratiba ya Ziara ya 38 ya Kitume ya Papa huko Nur-Sultan,mji mkuu wa nchi kubwa ya Asia ambako atakwenda kushiriki Kongamano la VII la viongozi wa dini za dunia na za jadi.Kwa kuchochewa na maswali ya waandishi wa habari,alisema mikutano ya nchi hizo mbili bado inakamilishwa,bila kutoa ufafanuzi wowote kuhusu kutokuwepo kwa Patriaki Kirill au dhana ya mkutano na Xi Jinping.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Msemaji wa Ofisi ya Vyombo vya Habari Vatican, Dk. Matteo Bruni, katika ziara ya kitume ya  Papa Francisko inayotarajiwa kwenda katika nchi kubwa iliyo kwenye makutano ya makabila, imani na tamaduni nyingi, Ijumaa asubuhi tarehe 9 Septemba 2022, amesema: “Katika moyo wa ziara hii inawezekana kuwa na mazungumzo, kukutana, na kutafuta amani tu kati ya ulimwengu tofauti wa kidini na kiutamaduni”. Njia ya ndege ya papa inajumuisha kupitia juu ya nchi ya: Italia, Kroatia, Bosnia-Herzegovina, Serbia, Montenegro, Bulgaria, Uturuki, Georgia, Azerbaijan.

Ni ziara baada ya ile ya Yohane Paulo  II miaka 21 iliyopita

Ziara ya Papa  Francisko ni sehemu ya wakati wa mlinganisho wa kina na ile iliyofanywa  kwa miaka ishirini na moja iliyopita na Matakatifu Yohane Paulo  II, ambaye alikwenda huko, akionesha ubinadamu,na  ujasiri usio na kipimo siku chache baada ya shambulio la kigaidi la minara miwili na  Pentagon huko New York Marekani. Hata leo hii hali ya kimataifa imeathiriwa na wasiwasi wa kimataifa wa vita vya Ukraine na migogoro mingi ya dunia. Katika tukio hilo ambalo lilirejezeshwa uhuru na umoja wa taifa na ulimwengu usio na jeuri, mashahidi wa imani wa karne ya ishirini walikumbukwa na Papa. Kwa hakika alikuwa na maneno ya kutia moyo katika nyakati ambazo si rahisi za kupotoshwa. Dk Bruni alikumbusha baadhi ya vifungu vya hotuba ya Papa Yohane Paulo II alipowasili Kazakhstan. Kwa namna ya pekee  akanukuu: "Kazakhstan, Ardhi ya mashahidi na wamini, Ardhi ya wahamishwaji na mashujaa, Ardhi ya wanafikra na wasanii, msiogope! Ikiwa ishara za majeraha yaliyowekwa kwenye mwili wenu yamebaki ndani na mengi, ikiwa shida na vizuizi,vinarundikana katika kazi ya ukarabati wa vifaa na kiroho: “Ubinadamu una upendo na haki kama kanuni yake, ni utukufu mkuu wa kazi ya Aliye Juu ( Maneno ya Abai Kunanbai sura 45).

Kongamano la Viongozi wa Dini katika Jumba la  Uhuru

Fursa ya  ziara ya Papa  Francisko ni Kongamano la VII la viongozi wa dunia na dini za jadi  kuanzia tarehe (14-15 Septemba) ambalo linafanyika katika Jumba la  Uhuru, kubwa zaidi kuliko lile la   Amani na Upatanisho, lililokuwa limechaguliwa awali. Limejangwa katikati ya jiji,likiwa na muundo wa sura ya trapezoidal, ambalo limepambwa kwa nje na kimiani kilichoundwa na mirija inayokumbuka muundo wa yurt, nyumba za wapita njia yaani za wahamaji wa nyika ya Asia. Kwa sasa wajumbe  wapatao 108 kutoka nchi 50 wamethibitishwa; na katika matoleo yaliyopita, ujumbe uliwakilishwa na Kardinali lakini, wakati huu ni Papa mwenyewe. Kaulimbiu inayoongoza  mkutano huo ni “Wajibu wa viongozi wa dini za ulimwengu na za jadi katika maendeleo ya kiroho na kijamii ya mwanadamu katika kipindi cha baada ya janga”. Mada zitazo shughulikiwa:  ni “Jukumu la dini katika kuimarisha maadili ya kiroho na maadili katika ulimwengu wa kisasa”; “Jukumu la elimu" kwa kuishi pamoja kwa dini na tamaduni na "kuimarisha amani na maelewano"; “Mchango wa viongozi wa dini na wanasiasa katika kuendeleza mazungumzo na amani ya dini mbalimbali duniani, katika mapambano dhidi ya itikadi kali, na ugaidi, hasa kwa misingi ya kidini”; na “Mchango wa wanawake katika ustawi na maendeleo endelevu ya jamii na nafasi ya jumuiya za kidini katika kusaidia hali ya kijamii ya wanawake”.

Ukaribu wa vizazi vya mashuhuda wa imani wa karne ya ishirini

Katika kurejea mpango wa ziara ya Papa Francisko, Dk Bruni alibainisha kwamba katika adhimisho la Misa Takatifu mnam tarehe 14 Septemba, katika uwanja wa Maonesho (ambapo Maonesho ya Kimataifa ya 2017 yalifanyika na  kwamba inawezekana kuwapo watu wapatao elfu kumi ) kuna uwezekano wa uwepo wa wakristo , wana wa mateso na serikali ya Kisoviet na kuishia kuwa wafungwa katika gulags. Papa Francisko atazungukia uwanja huo. Miongoni mwa uteuzi uliopitiwa kwa upya katika uwasilishaji wa Ijumaa 9 Septemba, wa  Papa katika Kanisa Kuu la Mama Msaada wa Kudumu, ambalo Dk Bruni alikumbuka mwanzoni kwamba : baadhi ya wakazi wa Belarusi na mkoa wa Volga na maeneo mengine ya (USSR) ya zamani walifukuzwa kwa miaka Thelathini huko Kazakhstan na hapa, ili kutoroka kutoka kwa serikali, nyumba ya sala iliwekwa wakfu nje kidogo ya jiji kwa heshima ya picha ambao Jumuiya  walikusanyika pamoja wakati wa kujificha. Katika miaka ya tisini, Kanisa kuu lililowekwa kwa ajili ya picha lilijengwa. Pia lilitembelewa na Papa Yohane Paulo II na mkutano na maaskofu na watawa  utafanyika hapo kwa baraka ya Picha ya  Mama wa steppe kubwa.

Mikutano baina ya nchi mbili bado inafafanuliwa

Wakati wa maombi ya kimya ya viongozi wa kidini, kabla ya ufunguzi wa Kongamano, utafanyika mahali pale pale. Kuhusu hotuba tano ambazo Baba Mtakatifu atatoa,  kwa mujibu wa msemaji huyo wa Vatican alidokeza kwamba inawezekana kureje juu ya kukomesha hukumu ya kifo, ambayo ilifikiwa na Katiba mpya kupitishwa nchini mwezi Juni mwaka huu. Marejeo mengine ambayo yanatarajiwa kuwepo, yale yanayohusiana na jamii ya Kazakhistan na taasisi ambazo ziko katika mabadiliko kamili, inawezekana kufikiria maandamano yaliyoshtua Kazakhstan mwanzoni mwa mwaka. Mikutano ya nchi mbili ambayo Papa atafanya kama sehemu ya kukaa kwake Kazakhstan bado inawafanyiwa kazi kwa fafanuliwa:  kwa maana hiyo Nyakati na mbinu bado zinahitaji kuchunguzwa, alisema Bwana  Bruni. Na kuhusiana na kutokuwepo kwa Patriaki Kirill na katika mkutano wa dhahania wa nchi mbili na rais wa China, Xi Jinping, huko Kazakhstan katika siku hizo hizo, Msemaji wa  Ofisi ya Vyombo vya Habari Vatican hakutoa ufafanuzi wowote au nyongeza.

Ziara ya Papa nchini Kazakhistan
09 Septemba 2022, 18:23