Tafuta

Uchumi wa Francisko:Papa yuko Assisi

Hatimaye Papa Francisko amefika Assisi kwa wazalendo na wageni waliokuwa wakimsubiri kwa shuku ili kukutana na vijana wanauchumi,wajasiriamali na wanamapinduzi kutoka nchi zaidi ya miamoja ulimwenguni ili kushiriki Tolepo la III la "Uchumi wa Francisko"ana kwa ana mara baada ya matoleo II kufanyika kwa njia ya mtandao kutokana na janga la uviko.

Na Angella Rwezaula- Vatican.

Mji wa Mtakatifu Francis wa Assisi, Jumamosi tarehe 24 Septemba umempokea Baba Mtakatifu Francisko ili kushirki na vijana wanauchumi, wajasiriamali na wanamapinduzi waliofika zaidi ya nchi 120 kutoka ulimwenguni kote  ili kushiriki Tolepola III la tukio la Uchumi wa Francisko ana kwa ana mara baada ya matoleo mawili kufanyika kwa njia ya mtandao kutokana na janga la uviko.

Papa Francisko amefika Assisi kukutana na vijana wa Uchumi wa Francisko
Papa Francisko amefika Assisi kukutana na vijana wa Uchumi wa Francisko

Economy of Francesco”, ni harakati ya kimataifa iliyoanzishwa na Baba Mtakatifu Francisko kwa kuweka ari ya mchakato wa mazungumzo jumuishi na wa mabadiliko ulimwenguni kueleka katika uchumi mpya. Kizazi kipya cha vijana kina shauku ya kufanya mabadiliko mapya.

Uchumi wa Francisko:Papa Francisko yuko Assisi kukutana na vijana wanauchumo
Uchumi wa Francisko:Papa Francisko yuko Assisi kukutana na vijana wanauchumo

Katika siku ya kwanza ya “Uchumi wa Francisko! huko Assisi tarehe 22  Septemba 2022 ilifunguliwa kwa mfululizo wa mijadala na meza za mduara kutoka pande zote ili kuwasilisha mavuno, yaani kile ambacho  kimefanywa kutokana na mipango iliyofanywa duniani kote ili kushughulikia masuala ya kiuchumi na changamoto za kisasa. Wanauchumi vijana na wajasiriamali walishiriki mbegu na matunda yaliyotawanyika katika kanda mbalimbali za sayari.

Uchumi wa Francisko:Papa Francisko yuko Assisi kukutana na vijana wanauchumo
Uchumi wa Francisko:Papa Francisko yuko Assisi kukutana na vijana wanauchumo
24 September 2022, 09:49