Tafuta

2023.01.19 Watumishi wa Mungu 6 wapya wa Kanisa 2023.01.19 Watumishi wa Mungu 6 wapya wa Kanisa  

Kanisa limepata Watumishi wa Mungu wapya sita

Hawa ni kutoka Italia na Hispania ambao miongoni mwao ni sura nne za kikuhani,mtawa mmoja na mwanamke mlei.

Angella Rwezaula;- Vatican

Baba Mtakatifu Francisko, wakati wa mkutano Alhamisi 19 Januari 2023  na Kardinali Marcello Semeraro, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Kuwatangaza  Watakatifu, aliidhinisha Baraza hilo kuhusu utambuzi wa fadhila za kishujaa za Watumishi sita wa Mungu ambao kuanza sasa wanaheshimika  kama Watumishi wa Mungu.  Hao ni Miguel Costa y Llobera, Gaetano Francesco Mauro, Giovanni Barra, Vicente López de Uralde Lazcano, Maria Margherita Diomira wa Neno lililofanyika Mwili na Bertilla Antoniazzi.

Kuabudu Ekaristi na ibada ya Maria

Katika Kanisa Kuu la Majorca kwa amri ya Mtakatifu Pio X, Miguel Costa y Llobera aliishi Hispania kati ya nusu ya pili ya karne ya kumi na tisa na miaka ishirini ya kwanza ya karne iliyopita. Alizaliwa katika familia yenye hadhi na tajiri, akawa Padre , licha ya upinzani wa awali wa baba yake. Alikuwa mhubiri mwenye shauku na kuungamisha, mtu wa sala na mshairi, pia alikuwa profesa wa akiolojia takatifu na historia ya fasihi. Wale waliomfahamu walimtaja kama “hombre muy piadoso e ilustrado”.

Mtumishi wa Mungu Miguel Costa y Llobera
Mtumishi wa Mungu Miguel Costa y Llobera

Ibada ya Ekaristi na ibada ya Maria zilikuwa nguzo za maisha yake ya kiroho. Aliishi umiliki wa mali ya kidunia akiwa na kikosi, ambacho alikiona kuwa njia ya kuwasaidia maskini. Uangalifu hasa ulikuwa  kwa wagonjwa. Alikufa ghafla, akiwa na sifa ya utakatifu,mnamo mwaka wa 1922, alipokuwa akihubiri kutoka kwenye eneo la kuhubiria la  Kanisa la watawa wa Wakarmeli wa Majorca wakati wa fursa ya miaka mia moja tangu kutangazwa  kwa Mtakatifu Teresa wa Avila kuwa mtakatifu.

Mwinjilishaji kati ya wakulima

Gaetano Francesco Mauro, ambaye mnamo 1928, alianzisha Shirika la  Wafanyakazi Makatekesta wa Vijijini  ambaye  alikuwa kuhani wa jimbo na aliishi kati ya mwisho wa 19 na mwanzoni mwa karne ya 20. Wakati wa Vita vya Kwanza vya dunia, alikuwa Padre wa kijeshi huko Friuli na, alitekwa, huko na wakati huo huo alitumia muda wa kufungwa katika kambi mbalimbali za mateso za Austria, ambapo aliugua kifua kikuu. Aliporudi huko Calabria alijitolea kupunguza umaskini, dhuluma na ujinga wa kidini kwa wakulima kwa kazi za uinjilishaji na uhmasishaji wa watu, na  baadaye mnamo 1925 akaanzisha Chama cha Kidini katika vituo vya  Vijijini (A.R.D.O.R.), kwa ajili ya mafundisho ya Kikristo mashambani ambapo  makao yake makuu aliyaanzisha kwenye jumba la kitawa la zamani la  Mtakatifu Francisko wa  di Paula huko Montalto Uffugo ambalo alikuwa amerikarabati  miaka michache kabla.

Mtumishi wa Mungu Gaetano Francesco Mauro
Mtumishi wa Mungu Gaetano Francesco Mauro

Mnamo mwaka 1943, Vatican  iliamua kuunganisha Shirika changa la Makatekista wa Vijijini na lile la Wafanyakazi wa Pii  lililoanzishwa na Carlo Carafa mnamo mwaka 1602: hivyo wakazaliwa Makatekista wa Vijijini Wapio Wafanyakazi ambao baada ya Vita Kuu ya Pili walizidisha kazi zao za kimisionari vijijini ya Calabria na ambayo Mtumishi wa Mungu aliteuliwa kuwa Mkuu wa Jeshi katika 1956. Katika shajara zake anasimulia “usiku wa giza”, ambao ni aina ya mfadhaiko, lakini daima aliishi imara katika imani na kwa matumaini, na  majaribu ya kiroho ambayo yalimsindikiza hadi siku zake za mwisho.

Kuhani mwenye furaha

Mtumishi wa Mungu Giovanni Barra alizaliwa mnamo mwaka wa 1914 kutoka katika  familia ya watu masikini huko Riva ya  Pinerolo, jimbo la Torino, Italia. Padre wa Jimbo, na msaidizi wa Chama cha Vijana Katoliki, ambapo mwaka 1943 alianzisha sehemu ya Shirikisho la Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Italia (FUCI) huko Pinerolo, ambalo alilisimamia hadi mnamo 1965. Liturujia na upendo daima vilihuisha kujitolea kwake katika vyama vingine vya Kikatoliki. Alifungua nyumba “Casa Alpina” kwa ajili ya  vijana huko Pragelato, kuwa mahali pa sala na mkutano kwa vijana na familia wakati wa kiangazi. Siku zote aliishi ukuhani wake katika kuungana na Kristo kama zawadi kutoka kwa Bwana na tangu 1969 alikuwa Mkuu wa Seminari ya Miito ya Watu Wazima huko Torino ambapo aliweka sala katikati ya malezi ya waseminari.

Mtumishi wa Mungu  Giovanni Barra
Mtumishi wa Mungu Giovanni Barra

Kuhani na mchunguzi  mkali wa roho ya mwanadamu, alikuwa na neno la matumaini kwa kila mtu, kama mwalimu alikuwa mtangulizi wa tabia ya kikanisa ambayo ilikuwa imekomaa na Mtaguso Mkuu wa Pili wa Vatikani. Padre na Mwandishi wa habari, pia alianzisha baadhi ya magazeti na kuingia kwenye mazungumzo na wasomi mbalimbali. Katika wosia wake wa kiroho, aliandika: “Nikitazama zamani, ninahisi wimbi la furaha na shukrani likipanda kutoka moyoni mwangu. Hakika mimi ni kuhani mwenye furaha katika ukuhani wangu”. Hata katika ugonjwa hakupoteza furaha yake, aliishi kama kielelezo cha utimilifu wa maisha katika Mungu.

Shuhuda wa amani na matumaini

Miongoni mwa Watumishi wapya kuna Mtumishi wa Mungu Vicente López de Uralde Lazcano, Padre wa Shirika la Maria, aliyeishi Hispania kati ya 1894 na 1990. Mtu wa sala, katika muungano wa kina na Bwana, alikuwa mwalimu, kuhani msimamizi wa kikanisa na muungamishi aliyethaminiwa na wanafunzi, wale wanafunzi wa zamani, mapadre na waamini wengine wa Chuo cha “San Felipe Neri” yaani “Mtakatifu Filipo Neri” huko Cádiz, ambako aliishi huko  kwa miaka 62.

Mtumishi wa Mungy  Vicente López de Uralde Lazcano
Mtumishi wa Mungy Vicente López de Uralde Lazcano

Alipendwa sana na wanafunzi ambao alijua jinsi ya kuwapa amani na matumaini, hakuwahi kukatiza shughuli zake za ufundishaji, hata wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe, na huo wakati hakusita kuwatetea vijana  wa chuo kwa shambulio la  wanamgambo na kuokoa Ekaristi. Baada ya kustaafu alijitolea kwa bidii kwa  ajili ya sakramenti ya Upatanisho akitumia hada masaa nane kwa siku katika maungamo na kuwa sehemu ya  kukumbukwa kiroho kwa jiji la Cadiz.

Mshiriki wa machungu ya Mateso ya Kristo

Kwa tabia ya upole  na utulivu, iliyojitolea kwa sala katika  maisha ya kustaafu, kwa upendo maalum kwa ajili ya Ekaristi na Bikira Maria alikuwa  ni Mtumishi wa Mungu,  Maria Margherita Diomira wa Neno aliyefanyika Mwili, mzaliwa wa Maria Allegri, wa Shirika la Imara upendo wa Mchungaji Mwema ambaye aliishi maisha mafupi duniani, kati ya 1651 na 1677  huko Toscana Italia. Ili kufanya malipizi ya dhambi zake alipitia toba na mateso. Akipinga upinzani mkali wa baba yake, alijiunga kwanza katika monasteri ya Camaldolesi ya Mtakatifu Yohane Mwinjili huko  Boldrone, baadaye akaendea huko Firenze katika  Monasteri ya Upendo wa Yesu Mchungaji mwema, na kujikita katika elimu ya wasichana maskini na kuwakaribisha mahujaji.

Mtumishi wa Mungu  Maria Margherita Diomira wa Neno aliyefanyika mwili (zamani: Maria Allegri)
Mtumishi wa Mungu Maria Margherita Diomira wa Neno aliyefanyika mwili (zamani: Maria Allegri)

Maria Margerita Diomira alitajirishwa na Mungu kwa karama za ajabu za kiroho, kama vile unabii, maono, furaha, uwezo wa kushauri na kushiriki katika maumivu ya Mateso ya Kristo, pia kupokea unyanyapaa. Hakukuwa na upungufu wa vipindi vya mateso ya ndani. Watu wengi, wakiwemo wakuu, mapadre na maaskofu walimwendea kumwomba ushauri na faraja ya kiroho. Akiwa anaugua kifua kikuu, alijitoa kama mwathirika wa upendo kwa Bwana na akafa huko Firenze akiwa na umri wa miaka 26 tu.

Kujitoa maisha na udhaifu

Miongoni mwa watumishi wapya wa Mungu  pia kuna mwanamke mwingine, ambaye ni mlei wa  kawaida. Huyu ndiye Mtumishi wa Mungu Bertilla Antoniazzi aliyeishi miaka ishirini tu, kati ya 1944 na 1964 huko Veneto Italia. Alilazwa katika hospitali ya Vicenza alipokuwa na umri wa miaka tisa tu kutokana na ugonjwa wa maumivu ya mifupa  (rheumatic endocarditis), alikaana na ugonjwa huo ambao ulimlazimu kukaa nyumbani wakati wote: akiwa na ujasiri mkubwa, kwa hiyo alielewa kuwa dhamira yake ilikuwa kuwafariji walioteseka na kuwaleta wenye dhambi na roho karibu na Mungu kwa sadaka ya uzima na udhaifu.

Mtumishi wa Mungu  Bertilla Antoniazzi
Mtumishi wa Mungu Bertilla Antoniazzi

Hakujifungia kamwe: alianzisha urafiki na madaktari na wauguzi na mawasiliano mazito na wagonjwa wengine. Katika kujikabidhi kamili kwa Mungu katika maombi, hakuwahi kulalamika, hata katika miaka miwili ya mwisho ya maisha yake alitumia kitandani, na wakati vidonda vya kitanda vilipoonekana, moyo uliingia katika upungufu na mapafu kwenye edema. Katika hija ya Lourdes mnamo 1963, hakumwomba Mama Yetu uponyaji, lakini utakatifu.

Watumishi wa Mungu wapya wa Kanisa
19 January 2023, 17:51