Tafuta

Sudan Kusini inasherehekea kuwasili kwa Papa Francisko

Furaha ya wazi ya kutua kwa Papa yenye kuleta faraja katika majeraha ya wazi ya taifa na mji mkuu Juba,ambao unajionyesha jinsi ulivyo,kati ya umaskini ulioenea na mapambano ya kutafuta usawa wa upatanisho wa ndani,wakiwa na imani kwamba safari hiyo ya kitume italeta mwanzo mpya

Na Angella Rwezaula; - Vatican.

Hatimaye kile kilichosubiriwa kwa muda mrefu kimetimia, Papa Francisko sasa yuko ziara yake ya Kitume na Kiekumene nchini Sudan Kusini ambayo imeanza Ijumaa tarehe 3 Februari. Amelakiwa kwa nyimbo na kauli mbiu akishangiliwa huko jijiniJuba kwa furaha tele, japokuwa  furaha hizo zikiwa na hisia za ndoto ambazo kwa wengi waliamini kuwa hisingewezekana, hasa baada ya kusitishwa kwa ziara hiyo mwezi Julai mwaka 2022, na kumtuma Kardinali Pietro Parolin, kutokana na kuahirishakwa sababu ya ya matibabu ya goti.

Rais wa Sudan Kusini akimlaki Papa uwanja wa Ndege
Rais wa Sudan Kusini akimlaki Papa uwanja wa Ndege

Waliomkaribisha Papa anapowasili jijini Juba, akitokea Congo DRC, kwa ndege ya ATI ni Rais Salva Kiir, ambaye alikutana na  Papa Francisko mnamo mwaka 2019 katika nyumba ya Mtakatifu Marta, pamoja na makamu wa rais, ambapo katika tukio hilo lilionesha  picha zake, Papa anainama kuibusu miguu ya watawala wa nchi iliyoliwa na ghasia tangu kuzaliwa kwake mnamo mwaka 2011 na ambazo bado ziko hai katika kumbukumbu ya Wasudan Kusini.

Mavazi ya kiutamaduni, waliocheza ngoma wakimkaribisha Papa
Mavazi ya kiutamaduni, waliocheza ngoma wakimkaribisha Papa

Kupitia taarifa za moja kwa moja kutoka kwa wawakilishi wetu huko Juba Francesca Sabatinelli na JohnBatist Tumsime waliofika mapema kwa ajili ya ziara hiyo wamebainisha kwamba ngoma na nyimbo zimesikika zikimkaribisha Papa Francisko kwenye uwanja wa ndege ambazo kwa hakika ni kielelezo cha furaha kubwa wanayopata wananchi kwa uwepo wake, jambo ambalo kwa wengi hapo litamaanisha kuthibitishwa katika imani ambayo imeendelea kuwa thabiti. Na hii hata hivyo licha ya vurugu za kidugu ambazo hazijakoma za kuharibu maisha ya watu na kusababisha watu waliokimbia makazi yao, kama vile wale ambao Papa Francis atakutana nao Jumamosi tarehe 4 Februari katika Ukumbi wa Uhuru, inafafanuliwa na wengi kuwa ni uteuzi mzito zaidi ambao Papa atakuwa nao nchini humo hadi siku ya kuondoka kwake, tarehe 5 Februari 2023.

Kikundi cha ngoma katika uwanja wa ndge kumlaki Papa Francisko
Kikundi cha ngoma katika uwanja wa ndge kumlaki Papa Francisko

Papa Francisko amepita katika barabara pekee yenye lami katika mji ambayo imetengenezwa kwa sababu ya ujio wake na ambayo pia inaelekeza kwenye Ubalozi wa Vatican ambayo pia ilikamilishwa haraka haraka kwa masaa ya mwisho wa siku za ujio wake na kupambwa. Kufika kwa Papa Sudan Kusini kunaleta tumaini kwa watu wanaotafuta kabisa amani na umoja, wa nchi nzima ambayo, licha ya ardhi yake tajiri sana, imekandamizwa na vita, umaskini, na sasa pia na hali ya tabianchi ambayo inajidhihirisha yenyewe kuwa kama kichaa cha mafuriko yanayoendelea na mabaya kwa  sababu ya uchumi ambao tayari ulikuwa kwa bahati mbaya na ambayo haufanyi chochote zaidi ya  kuongezeka hali mbaya ya kutisha ya wakimbizi na watu waliokimbia makazi yao ndani.

Baba Mtakatifu anaonekana katikati ya nwahija wenzake Askofu Mkuu Welby na Mchungaji Greenshield na Rais wa Sudan Kusini
Baba Mtakatifu anaonekana katikati ya nwahija wenzake Askofu Mkuu Welby na Mchungaji Greenshield na Rais wa Sudan Kusini

Mji wa Juba kwa hakika ulijiandaa kukutana na Baba Mtakatifu,  na ulijitayarisha kwa kutafakari juu ya thamani ya upatanisho, ambayo kwa hapo imesalia kuwa changamoto kubwa lakini inayobebwa mbele na wale wote wanaomwona Papa kuwa ndiye atakayeweza kuzungumza na viongozi ili kuwachochea katika makubaliano ya amani ya mwaka 2018 kati ya makundi yaliyotia sahini yasiendelee kuwa katika karatasi bure na kuwataka ili washirikiane kwa manufaa ya watu wao.

Papa sasa yuko Sudan Kusini hadi tarehe 5 Februari 2023
Papa sasa yuko Sudan Kusini hadi tarehe 5 Februari 2023

Hija ya kiekumene inayoanza tarehe hii 3 Februari ya Papa  Fransisko, Askofu mkuu wa Canterbury Welby na msimamizi wa Kanisa la Scotland  Mchaungaji Greenshields, kwa hiyo inataka kuwa ni ushuhuda wa amani na haki, kwa mshikamano na watu, si lazima tena kulilia wafu na uharibifu bali matumaini mapya. Ratiba ya siku ni Mara baada ya kuwasili na kukutana na rais na makamu wa rais katika ikulu ya rais, Papa atakutana na mamlaka, mashirika ya kiraia na mabalozi katika bustani ya ikulu hiyo, ambapo atahutubia hotuba yake ya kwanza ya hatua hiyo ya Sudan ya kusini, mara baada ya kutakuwa na uhamisho kwenda Ubalozi wa Vatican mahali atakapokuwa kwa siku hizi za ziara yake.

03 February 2023, 15:10