Tafuta

Uanja wa Mtakatifu Francisko utageuka bustani au kichaka cha kijani. Uanja wa Mtakatifu Francisko utageuka bustani au kichaka cha kijani. 

Together:Kijani na mimea tofauti kama ishara ya Ikolojia Uwanja wa Mtakatifu Petro

Mandhari nzuri ya memea,vichaka,nyasi na maua itaweka ukijani.Itatengenezwa na Confagricoltura na Assoverde ambapo utakuwa ishara ya "Pamoja -Kusanyiko la Watu wa Mungu",katika mkesha wa kuombea sinodi Septemba 30 katika Uwanja wa Mtakatifu petro.Mbunifu wa mazingira anasema sio mapambo tu bali ni msukumo wa bioanuwai ya mifumo ikolojia.

 Vatican News

Vipande vipande vya asili vingi ili kuamsha bioanuwai ya mazingira na ikolojia utakuwa ni uundaji wa kijani utakaopamba Uwanja wa Mtakatifu Petro kwenye tukio la “Together yaani Pamoja - Kukusanyika kwa Watu wa Mungu”, katika mkesha wa maombi ya Kiekumeni kuombea Mkutano wa  XVI wa kawaida wa Sinodi ya Maaskofu, uliopangwa kufanyika Jumamosi ijayo, tarehe 30 Septemba 2023 jioni. Kwa hiyo yatakuwa ni mapambo ya maua na mimea mbali mbali ili kuibua uzuri wa bayoanuwai na heshima inayohitaji, ambayo shukrani kwa Confagricoltura, Shirikisho nyeti kwa masuala ya uwajibikaji wa kijamii na mahitaji ya jamii katika suala la mazingira, kwa ushirikiano wa Assoverde na mbunifu wa mazingira, Virna Mastrangelo, ambaye ni mtu wa kuwasiliana na Mkoa wa Lazio kwa ajili ya Chama na Ofisi yake ya Greenatelier.

Mbunifu huyo akihojiana na Vatican News kuhusu Confagricoltura ya kuleta bayoanuwai kwenye Uwanja wa Mtakatifu Petro, kuna maana gani? Alijibu kuwa: "Sio Confagricoltura tu lakini pia Assoverde, Jumuiya ya Italia ya Wajenzi wa Mazingira, iliyounganishwa na Confagricoltura, ambayo pia imejitolea kulinda mazingira. Sisi ni chama kinachojumuisha zaidi ya kampuni 200 za vitalu na wafanyakazi huria Nchini Italia. Kufuatia waraka wa Papa Francisko wa Laudato si', tulisoma ushauri wake  kuhusu kijani na tulipenda sana, kwa hivyo tulijaribu, kupitia ishara hii ndogo, kutoa heshima kwa Baba Mtakatifu ambaye alikumbuka tunu za ulimwengu za mazingira, zilea mbazo  tunaunga mkono na wale ambao tunajaribu kufanya sasa zaidi ili kila mtu awafahamu, kwa sababu kuna mengi ya majadiliano juu yake, lakini ufahamu wa kina, kwa maoni yangu, bado haujakuwapo. Kwa sababu ikiwa mmea una kiu na hakuna mtu aliye tayari kutoa tone la maji, ufahamu huo haupo.”

Je, mimea hiyo ilichaguliwa kulingana na kigezo fulani?

“Ilichaguliwa kutoka katika mitazamo tofauti: kwanza kuwakilisha alama na kisha, kama nilivyokwisha sema, kwa sababu tulilazimika kulinda sakafu na usanifu. Na hivyo tulilazimika kufanya uchaguzi, lakini mimea yote ni muhimu daima, hasa milele, ni alama za maisha, kifo na kuzaliwa upya.”

Zaidi ya mpango katika wa Uwanja wa Mtakatifu, ni nini lengo la Confagricoltura pamoja na Assoverde kwa ajili ya bioanuwai?

Kwa pamoja daima na Assoverde na sasa pia na Kèpos, shirika la kuhamasisha jamii ambalo limekuwa nasi pamoja na Confagricoltura, tunapanga kufanya bustani ya kiafya za mijini ambamo sifa zote katika viwanja lazima ziwe nazo kwa kuzingatiwa hivyo na kupata zitaakisiwa na uthibitisho. Kila kitu kutoka katika bayoanuwai hadi mimea vamizi kitazingatiwa. Mada ni tofauti sana.

28 September 2023, 16:19