Tafuta

 Briefing ya Sinodi Jumatatu 16 Oktoba 2023. Briefing ya Sinodi Jumatatu 16 Oktoba 2023.  (Vatican Media)

Sinodi:Sinodi siyo maneno mafupi bali ni uzoefu wa kila siku

Katika taarifa ya alasiri Oktoba 16 katika Ofisi ya Vyombo vya Habari vya Vatican,mada sinodi iliyofanyika asubuhi zilioneshwa.Kuanzia roho ya kimisionari hadi mazungumzo ya kidini na jukumu la wanawake katika huduma kwa Kanisa.Mkutano huo ulikumbuka miaka 45 tangu kuchaguliwa kwa Papa Yohane Paulo II 1978.

Vatican News.

Maana ya kweli ya sinodi, wingi wa utofauti, jukumu ambalo wanaume na wanawake waliobatizwa wanatimiza ndani ya Kanisa, shughuli za kimisionari, uekumene na mazungumzo ya kidini, nafasi ya wanawake katika mtazamo wa ushemasi wa kike na mageuzi ya kidijitali, bila kusahau vijana wa nchi maskini duniani ambao wamekataliwa kabisa na matumizi ya teknolojia za kisasa zaidi. Hizi ni baadhi ya mada zilizotolewa  asubuhi tarehe 16 Oktoba 2023 wakati wa kazi ya sinodi inayoendelea mjini Vatican.

Na hayo yamefahamika wakati wa mkutano wa alasiri  Jumatatu hiyo na waandishi wa habari, uliofanyika katika Chumba cha Waandishi wa Habari cha Vatican. "Ripoti za kwanza za mizunguko midogo  pia zilichunguzwa", kwa mujibu wa maelezo ya  Dk.  Paolo Ruffini, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano na rais wa Tume ya Habari, ambaye alisema kwamba kikao "kilifunguliwa kwa kutoa shukrani za washiriki kwa Baba Mtakatifu Francisko katika Waraka wake wa Kitume: “C'est la Confiance” yaani “Ni Uaminifu” uliotolewa kwa heshima ya Mtakatifu Theresa wa Mtoto Yesu na wa Uso Mtakatifu, kama sehemu ya kumbukizi ya Miaka 150 tangu kuzaliwa kwake huko Alençon nchini Ufaransa, na ambao ulichapishwa tarehe 15 Oktoba 2023. Mkuu huyo wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano pia alitaka kusisitiza kwamba washiriki wenyewe walikumbuka "kwa shangwe za muda mrefu siku ya kumbukumbu ya kuchaguliwa kwa Mtakatifu Yohane Paulo II na ukumbusho wa kuwekwa wakfu kwa baadhi ya makuhani". Zaidi ya hayo, Dk. Ruffini alishirikisha na waandishi wa habari habari za mkutano huo, Ijumaa iliyopita, kuhusu  kamati ya kawaida ya Sinodi iliyotathmini "safari iliyofikiwa hadi sasa na ubora na uzuri wa wasikilizaji".

Safari ya sinodi si maneno mafupi

Padre Vimal Tirimanna, wa Shirika la Mkombozi Mtakatifu zaidi, mtaalimungu kutoka Sri Lanka, alijikita katika mchakato wa sinodi unaotekelezwa katika Sinodi, kwa ushuhuda wa kina. "Kuja hapa - alisema - nilifikiri kwamba sinodi ni maneno matupu, lakini ilinibidi kubadili mawazo yangu. Sinodi ilianza Majuma matatu yaliyopita na nikagundua kuwa sinodi inaishi hapa." Padre aliweka wazi  jinsi ambayo  haya yote yanaoneshwa pia katika mpangilio wa meza hizo za mduara: “Unapoketi kwenye meza za duara karibu na maaskofu, makadinali, wanawake na walei, unagundua kwamba uko katika kanisa la kisinodi na si piramidi tu." Sharti ambalo alitaka kutaja, ambalo sio wazo la Papa Francisko, lakini "anakumbuka kabisa Mtaguso wa Pili wa Vatican". Tirimanna alitumaini kwamba mtindo huu ungeweza kusafirishwa “hata nje ya Sinodi yenyewe”.

Maombi na maandalizi

Mtu ambaye ameridhika kujionea mwenyewe kwamba sinodi inazidi kuwa ukweli ni Sista Patricia Murray, wa Taasisi ya Bikira Maria na katibu mtendaji wa Umoja wa Kimataifa wa Mama Wakuu  wa Mashirika. Kwa waandishi wa habari, alikuwa na hamu ya kutaja kwamba "kwa miaka ishirini mimi, katika mkutano wangu, nimekuwa nikijaribu sinodi kwa kumweka Yesu katikati na kusikiliza wengine. Ninafurahi kuona kwamba njia hii imekuwa ya Sinodi yenyewe na inaendelea katika Kanisa lote." Mtawa huyo pia alieleza kuwa wakati wa kazi za sinodi sauti zote zinasikilizwa kwa uhuru na kwamba "tunafika kwenye mikutano midogo iliyoandaliwa ili kuweza kupambanua vyema. Ni lazima pia tutumie wakati vizuri kusali, jambo muhimu tunapochunguza historia zinazotoka kwa ndugu kutoka nchi na tamaduni nyingine.”

Nuru inayoangazia giza

Waraka wa kitume  hivi karibuni juu ya Mtakatifu Theresa wa Lisieux pia ulimsukuma Askofu msaidizi wa Prague, Zdenek Wasserbauer, ambaye aliona hati hiyo kama dira ya Sinodi nzima. "Wakati wa kazi hizi - aliwaambia waandishi wa habari  kuwa  niliona kwa uwazi sana neno 'utume' ni jambo muhimu kwetu. Na Mtakatifu Theresa wa Lisieux ni msimamizi mwenza wa utume wa kimisionari."  Kuna sababu mbili kwa nini askofu anachukulia himizo hilo kama mwongozo, na kama taa: "Ya kwanza inahusishwa na ukweli kwamba Mtakatifu, alipoingia Utawa wa Karmeli, alikuwa na hamu ya kuokoa roho. Naam, nilitambua kwamba hapa washiriki wote 400 hukusanyika kila siku kutafuta wema wa wengine, kwa ajili ya wokovu wao. Sababu ya pili inahusu usiku wa giza ambao Mtakatifu Theresa wa Lisieux alihisi katika nafsi yake mnamo mwaka 1856. Wengine wanasema kwamba hata leo Kanisa la Milenia ya Tatu linapitia giza: kutazama, Sinodi ni nuru inayoangazia giza".

Jihadharini na maumivu

Akijibu baadhi ya maswali kutoka kwa waandishi wa habari kuhusu kama maumivu ya watu wa LGBT+ yamejadiliwa au la, Sista Murray alisema kuwa "kumekuwa na mjadala kuhusu suala la maumivu katika vikundi vidogo. Tulijaribu kuelewa jinsi Kanisa, katika mazingira ya kiliturujia na kichungaji, linavyoweza kuweka wazi kwamba linaomba msamaha kwa maumivu yaliyosababishwa. Kuna ufahamu mwingi."

Kwa kirefu zaidi, swali lingine ambalo mwandishi wa habari alitaka kujua ikiwa mada ya baraka ya wapenzi wa jinsia moja ilikuwa imeshughulikiwa. Mwenyekit wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano Dk. Ruffini alieleza kuwa suala hilo "si la msingi" na kwamba kulikuwa na mazungumzo zaidi kuhusu mafunzo, huduma zilizowekwa rasmi, chaguo la upendeleo kwa maskini, na juu ya ukoloni. Mafundisho ya Kikatoliki, kwa Dk. Ruffini aliongeza, ni msingi wa kila kitu kinachofanyika katika shule hiyo yaaNI ndani ndani ya  Sinodi.

Maaskofu wa China

Zaidi ya hayo, akithibitisha habari kwamba maaskofu wa China waliohudhuria katika Sinodi hiyo wataacha kazi hiyo tarehe 17 Oktoba, Dk. Ruffini mwenyewe alieleza kuwa "itawabidi kufanya hivyo kwa sababu za kichungaji zinazowaita kurejea majimboni kwao."

KILICHOJIRI NDANI YABSINODI 16 OKTOBA 2023
17 October 2023, 11:19