Tafuta

2023.10.18 Washiriki wa Sinodi ya Maaskofu wakati wa Misa Katika kanisa Kuu la Mtakatifu Petro Vatican. 2023.10.18 Washiriki wa Sinodi ya Maaskofu wakati wa Misa Katika kanisa Kuu la Mtakatifu Petro Vatican.   (Vatican Media)

Padre Radcliffe:‘nimewambiwa Sinodi haitabadili lolote lakini ni kukosa imani’

Katika Sinodi inayoendelea mjini Vatican kwa washiriki wote,maaskofu,mapadre,watawa wa kike na kiume na waamini walei,mara baada ya Misa Takatifu katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro,wameunganika katika Ukumbi wa Paulo VI mjini Vatican.Baada ya utangulizi wa msemaji Mkuu wa Sinodi,imefuata Tafakari ya Padre Radliffe.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Ifuatayo ni Tafakari ya Padre Timothy Radcliffe OP,  kwa washiriki wa Sinodi ya kisinodi inayoendelea mjini Vatican aliyoitoa tarehe 18 Oktoba 2023 wakati Mama Kanisa anaadhimisha Siku Kuu ya Mtakatifu Luka Mwinjili. Ilikuwa ni mara baada ya utangulizi wa Msemaji mkuu wa Mkutano Mkuu wa Sinodi ya XVI ya Maaskofu katika Kikao cha Kumi mbili cha Sinodi tangu walipoanza tarehe 4 Oktoba  2023. Kardinali Jean-Claude Hollerich Jumatano alitoa utangulizi wa kipengele  cha Nne cha Instrumentum Laboris kuhusu mada za mamlaka, huduma, utambuzi, shughuli pana za  ndani ya maeneo. Kwa mujibu wake alisema ni "Masuala tete ambayo yanaathiri ukuaji wa mila na utamaduni kama vile utambuzi mbaya unaoweza kuivunja au kuifunga."

Kwa njia hiyo katika Tafakari hiyo  Padre   Mdominikani anasema: 'Ushiriki, serikali na mamlaka: Je, ni taratibu gani, miundo na taasisi zinazohitajika kwa Kanisa la Sinodi ya kimisionari? Luka, ambaye sikukuu yake tunaadhimisha leo hii, anazungumza nasi katika Matendo ya Mitume 15 kwa "Baraza la Yerusalemu", lililoitwa kukabiliana na shida kuu ya kwanza ya Kanisa baada ya Pentekoste. Kanisa limegawanyika sana. Kwanza kabisa, kati ya Kanisa la Yerusalemu na Paulo, pamoja na Injili yake ya uhuru kutoka kwa sheria; ndani ya Kanisa la Yerusalemu, Mafarisayo walioongoka wanasimama kando na wengine, na mitume wakiongozwa na Petro labda wametenganishwa na “wazee” wanaomgeukia Yakobo, ndugu ya Bwana. Kwa hiyo Kanisa limekabiliwa na mgogoro wa utambulisho ambao unapita zaidi ya chochote tunachoweza kufikiria leo

Papa Francisko alitangaza huko Lisbon majira ya joto kwamba "maisha bila shida ni maisha ya usafi ... maisha bila shida ni kama maji yaliyotuama, hayafai kitu, hayana ladha." Tunakomaa kupitia shida, kutoka kwa shida ya kuzaliwa kwetu hadi shida ya kifo. Tukikaribisha mikasa kwa matumaini, tutastawi. Tukijaribu kuziepuka, hatutakua kamwe. Ndugu zangu Waamerika walinipa t-shirt iliykuwa imeandikwa: “Kuwa na mgogoro mzuri! Tunasoma kwamba: Mitume na wazee wakakusanyika ili kulitafakari jambo hilo” (Mdo 15:6) Kanisa bado linakutana, kama tunavyofanya leo katika sinodi. watu pamoja, ili tangu mawio ya jua hata machweo ya jua kutolewa sadaka safi kwa jina lako.” Neno la Kigiriki la Kanisa, ekklesia, linamaanisha “kukusanyika.” Je, tuko tayari kuletwa pamoja, si kimwili tu, bali pia katika mioyo na akili zetu? Akitazama juu ya Yerusalemu kabla ya kifo chake, Yesu alisema, “Ni mara ngapi nimetaka kuwakusanya watoto wako, kama vile kuku akusanyavyo vifaranga wake chini ya bawa lake, lakini hamkutaka” (Luka 13:34). Je, tuko tayari kujiruhusu kubebwa zaidi ya kutoelewana na kushuku? Au tutakuwa kama ndugu mkubwa katika mfano wa mwana mpotevu ambaye anasimama kando, akikataa kuungana katika furaha ya kurudi kwa ndugu yake?

Wanafunzi walikusanyika Yerusalemu ili kutumwa Antiokia na ulimwenguni kote. Tumekusanyika katika Ekaristi ili kutumwa. Ni pumzi ya Roho Mtakatifu ndani ya mapafu yetu, akitukusanya na kututuma nje, akitia oksijeni damu ya Kanisa. Tumekusanyika ili kugundua amani kati yetu sisi kwa sisi na kutumwa kuitangaza kwa ulimwengu wetu maskini, uliosulubishwa na vurugu nyingi zaidi, huko Ukraine, katika Nchi Takatifu, huko Myanmar, Sudan, na katika maeneo mengine mengi. Je, tunawezaje kuwa ishara ya amani ikiwa tumegawanyika kati yetu wenyewe? Baraza la Yerusalemu lilikutana “katika jina la Yesu,” kama sisi pia tunafanya. Katika Sinodi tunaomba kila siku: "Tunasimama mbele yako, Roho Mtakatifu, tunapokusanyika kwa jina lako." Kukusanywa pamoja katika jina la Bwana kunamaanisha kwamba tuna uhakika kwamba neema ya Mungu inafanya kazi kwa nguvu ndani yetu. Petro alimwambia yule kiwete aliyekuwa kwenye lango la Hekalu, “Sina fedha wala dhahabu, lakini nilicho nacho ndicho ninachokupa: kwa jina la Yesu Kristo Mnazareti, simama utembee” (Mdo 3:6). (Mdo 3:6).

Mara nyingi watu wameniambia: “Sinodi hii haitabadilisha chochote.” Wengine kwa matumaini, wengine kwa hofu. Ni kukosa imani katika jina la Bwana, “jina lipitalo kila jina” (Fil 2:9). Wimbo wa zamani unaanza, "Ninajifunga leo kwa jina kuu la Utatu." Ikiwa tutakusanyika pamoja katika jina kuu la Utatu, Kanisa litafanywa upya, labda kwa njia zisizo dhahiri. Sio juu ya matumaini, lakini juu ya imani yetu ya kitume. Mwalimu wangu mkuu wa kwanza alikuwa Mdominikani  wa Sri Lanka, Cornelius Ernest. Aliandika juu ya uwezo wa neema ya Mungu kufanya kitu kipya. Ninanukuu: "Ni alfajiri, ugunduzi, majira ya kuchipua, kuzaliwa upya, kuja kwa nuru, kuamka, kupita mipaka, ukombozi, furaha, ridhaa ya ndoa, zawadi, msamaha, upatanisho, mapinduzi, imani, matumaini, upendo .... uwezo wa kubadilisha na kufanya upya vitu vyote: “Tazama, nafanya kila kitu kuwa kipya” (Ufu. 21:5) Kanisa daima ni jipya, kama Mungu, Mzee anayesimamia Siku na mtoto mchanga.

Wanafunzi walikusanyika pamoja kwa sababu waliona kwamba tayari Mungu alikuwa amefanya jambo jipya. Mungu alikuwa amewatangulia. Iliwabidi wampate Roho Mtakatifu. Petro anatangaza hivi: “Mungu, ajuaye mioyo ya watu, ameshuhudia kwa kuwapa Roho Mtakatifu, kama alivyotupa sisi; na katika kuitakasa mioyo yao kwa imani, hakufanya tofauti kati yao na watu, sisi” (Mdo 15:8). Hili kwa hakika lilikuwa gumu zaidi kukubalika kwa Mtakatifu Yakobo, ndugu wa Bwana, ambaye utambulisho wake uliegemezwa kwenye uhusiano wa damu na Bwana. Ni ajabu kwamba ni yeye ambaye anatangaza utambulisho huu mpya. “Ilionekana kuwa njema kwa Roho Mtakatifu na kwetu sisi.” Ni ujasiri na imani iliyoje anapaswa kuwa nayo kusema “sisi”, utambulisho unaoleta pamoja Kanisa zima lililogawanyika.

Bado anamwita Petro kwa jina lake la mwisho, "Simoni." Anaamsha polepole utambulisho huu mpya, Kanisa la Wayahudi na Mataifa. Ilichukua muda, kama inavyofanya kwetu. Wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini  Burundi, nilisafiri nchi nzima pamoja na ndugu zangu wawili, Mhutu na Mtutsi. Jioni, sisi watatu tuliadhimisha Ekaristi. Mwingereza na Waafrika wawili, Mhutu na Mtutsi: Maana mpya ya "sisi". Tulipokea Ekaristi kabla ya kuiweka katika akili na mioyo yetu. Leo, Mungu wetu tayari anazaa Kanisa ambalo si la Magharibi tena: Kanisa Katoliki la Mashariki, Asia, Afrika na Amerika Kusini. Ni Kanisa ambalo wanawake tayari wanachukua majukumu na kufanya upya taalimungu na hali yetu ya kiroho. Tayari, vijana kutoka kote ulimwenguni, kama tulivyoona huko Lisbon, wanatupeleka katika mwelekeo mpya, kwenye bara la dijiti.

Katika Dibaji ya Watakatifu, tunamshukuru Mungu kwa sababu “unalifanya upya Kanisa katika kila enzi kwa kuwainua wanaume na wanawake watambuliwe kwa utakatifu wao”. Tayari wako kati yetu. Tunauliza kwa usahihi: tufanye nini? Swali la msingi hata zaidi ni: Mungu anafanya nini? Je, tunakubali upya wa neema ya Mungu? Je, unaweza kuamini, baadhi ya Wadominika hata walimpinga Mtakatifu Ignatius wa Loyola! Nostra culpa, ‘yaani nimekosa mimi’. Inafurahisha kutambua kwamba Jacques anaweza tu kuelewa mpya kama ujenzi wa zamani. Ananukuu Amosi hivi: “Baada ya hayo nitarudi, na nitaijenga nyumba ya Daudi iliyoanguka; na kutoka katika magofu yake nitaijenga tena na nitaiinua tena, ili mataifa mengine yote wamtafute Bwana.  Mataifa yote ambao jina langu limeitwa. Upya daima ni upya usiotarajiwa wa zamani. Hii ndiyo sababu upinzani wowote kati ya tamaduni na maendeleo ni mgeni kabisa katika Ukatoliki. Sasa tutachunguza ni taratibu gani mpya, taasisi na miundo zinahitajika. Haya hayatakuwa suluhisho kwa matatizo ya usimamizi, lakini maneno kamili zaidi ya sisi ni nani. Historia ya Kanisa ni moja ya ubunifu wa kitaasisi usio na mwisho. Baada ya Ukristo kuwa dini halali katika Milki ya Roma, aina mpya za maisha ya Kikristo zilizuka kati ya baba na mama wa jangwani, ili kukabiliana na hatari mpya za mali.

Katika karne ya 13, vyuo vikuu vipya viliibuka ili kuunga mkono maono mapya ya kuwa binadamu. Wakati wa Mapinduzi ya Viwandani, mamia ya aina mpya za maisha ya kidini yalijitokeza kudhihirisha sisi ni nani kama kaka na dada wa maskini wapya wa mijini. Je, ni taasisi zipi tunahitaji kujieleza sisi ni nani kama wanaume na wanawake wa amani katika enzi ya vurugu, wenyeji wa bara la kidijitali? Kila mtu aliyebatizwa ni nabii. Je, tunawezaje kutambua na kukaribisha jukumu la unabii katika Kanisa leo? Namna gani sauti ya kiunabii ya wanawake, ambayo bado mara nyingi huchukuliwa kuwa “wageni katika nyumba zao wenyewe”? Hatimaye, Baraza la Yerusalemu liliondoa mizigo isiyo ya lazima iliyokuwa juu ya wapagani. Kwa maana “ilimpendeza Roho Mtakatifu na sisi tusiwatwike ninyi mzigo mzito zaidi ya hayo yaliyo lazima.” ( Mdo msitari 28 ) Wamewekwa huru kutokana na utambulisho uliotolewa na sheria ya kale.

Je, tunawezaje kutuliza mabega yaliyochoka ya kaka na dada zetu leo ​​ambao mara nyingi huhisi kukosa raha katika Kanisa? Hili halitafanyika kupitia jambo la kushangaza kama kufutwa kwa Sheria. Wala haitahusisha mabadiliko ya kimsingi katika utambulisho wetu kama kukiri kwa wapagani. Lakini tumeitwa kuimarisha utambulisho wetu kama marafiki wasiowezekana wa Bwana, ambao urafiki wao wa kashfa unavuka mipaka yote. Wengi wetu tulilia tuliposikia kuhusu msichana huyu aliyejitoa uhai kwa sababu alikuwa na jinsia mbili na hakujisikia kukaribishwa. Natumaini hii imetubadilisha. Baba Mtakatifu alitukumbusha kwamba wote wanakaribishwa: todos, todos, todos. Huko Ireland, mtu mmoja alipotea. Alimuuliza mkulima, “Ninawezaje kufika Dublin?” Mkulima alijibu: “Kama ningetaka kwenda Dublin, nisingeondoka hapa.” Lakini mahali watu walipo ni kutoka huko, acha safari ya kurudi nyumbani ianze nyumba ya Kanisa na nyumba ya Ufalme.

18 October 2023, 13:04