Tafuta

Baba Mtakatifu Francisko tarehe 4 Aprili 2024 amemteuwa Askofu Nicolas Pierre Jean Lhernould kuwa Askofu mkuu mpya wa Jimbo kuu la Tunis, nchini Tunisia. Baba Mtakatifu Francisko tarehe 4 Aprili 2024 amemteuwa Askofu Nicolas Pierre Jean Lhernould kuwa Askofu mkuu mpya wa Jimbo kuu la Tunis, nchini Tunisia.   (AFP or licensors)

Askofu Mkuu Nicolas Pierre Jean Lhernould wa Jimbo Kuu la Tunis, Nchini Tunisia

Baba Mtakatifu Francisko tarehe 4 Aprili 2024 amemteuwa Askofu Nicolas Pierre Jean Lhernould kuwa Askofu mkuu mpya wa Jimbo kuu la Tunis, nchini Tunisia. Kabla ya uteuzi huu, Askof mkuu mteule Nicolas Pierre Jean Lhernould alikuwa ni Askofu wa Jimbo Katoliki la Constantine-Hippone, nchini Algeria. Alizaliwa mwaka 1975, akapewa Daraja Takatifu ya Upadre mwaka2004, akawekwa wakfu kuwa askofu mwaka 2020 na hatimaye kusimikwa rasmi 29 Februari 2020.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S., Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko ameridhia ombi lililowasilishwa kwake na Askofu mkuu Ilario Antoniazzi wa Jimbo kuu la Tunis, nchini Tunisia la kutaka kung’atuka kutoka madarakani. Wakati huo huo, Baba Mtakatifu Francisko tarehe 4 Aprili 2024 amemteuwa Askofu Nicolas Pierre Jean Lhernould kuwa Askofu mkuu mpya wa Jimbo kuu la Tunis, nchini Tunisia. Kabla ya uteuzi huu, Askof mkuu mteule Nicolas Pierre Jean Lhernould alikuwa ni Askofu wa Jimbo Katoliki la Constantine-Hippone, nchini Algeria.

Askofu mkuu Nicolas P. J. Lhernould
Askofu mkuu Nicolas P. J. Lhernould

Itakumbukwa kwamba, Askofu mkuu Nicolas Pierre Jean Lhernould alizaliwa tarehe 23 Machi 1975 huko Courbevoie, Jimbo Katoliki la Nanterre nchini Ufaransa. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 22 Mei 2004 akapewa daraja Takatifu ya Upadre. Tarehe 9 Desemba 2019, Baba Mtakatifu Francisko akamteuwa kuwa ni Askofu wa Jimbo Katoliki la Constantine-Hippone, nchini Algeria na kuwekwa wakfu kama Askofu tarehe 8 Februari 2020. Tarehe 29 Februari 2020 akasimikwa rasmi kuwa Askofu mahalia akiwa na dhamana ya kufundisha, kuongoza na kuwatakatifuza watu wa Mungu. Ilipogota tarehe 4 Aprili 2024, Baba Mtakatifu Francisco akamteuwa Askofu Nicolas Pierre Jean Lhernould kuwa Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Tunis, nchini Tunisia.

Uteuzi

 

05 April 2024, 15:21