Tafuta

Masafa ya Radio Vatican yanafika mbali: imeongeza lugha ya 53. Masafa ya Radio Vatican yanafika mbali: imeongeza lugha ya 53.  (Vatican Media)

Kuanzia Aprili 2,lugha ya Kikannada pia ni sehemu ya vyombo vya habari vya Vatican!

Lugha ya Kikannada ni lugha ya 53 ya Radio Vatican-Vatican News.Kuanzia Aprili 2 kwenye tovuti ya Vatican utaweza kusoma habari katika lugha hii inayozungumzwa na mamilioni ya watu nchini India.Uwezekano huo unatokana na ushirikiano kati ya Baraza la Kipapa la Mawasiliano na Jimbo Kuu la Bangalore,katika Serikali ya India huko Karnataka.

Vatican News

Ninafuraha kwa kuzinduliwa kwa kurasa hizi katika lugha ya Kikannada katika  habari juu ya Papa, Vatican, Kanisa la Ulimwenguni kote na katika ulimwengu zitakuwa muhimu sana kwa Kanisa la mahali hapa Karnataka.” Alisema hayo Askofu Mkuu Peter Machado wa Bangalore kuhusiana na tukio hili. Akiendelea “Ninamshukuru Baba Mtakatifu wetu mpendwa, Papa Francisko, kwa kuendelea kukazia sinodi na kulifikisha Kanisa pembezoni. Waamini hakika watafaidika kwa kusoma makala hizi na, katika hatua ya baadaye inapowezekana, pia kutokana na uwasilishaji wao kupitia utengenezaji wa sauti/video. Nina hakika kwamba Kituo chetu cha Mawasiliano cha Jimbo Kuu la Bangalore kitaleta Kanisa la Ulimwengu karibu na watu.”

Ruffini:Tendo la heshima na huduma kwa mawasiliano halisi

Lugha mpya inaongezwa kwa zile zinazozungumzwa na Vatican News. Lugha ya kale. Lakini bado ni hai.” Amesema hayo Dk.  Paolo Ruffini, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano.  Sawa na jumuiya ya Kikatoliki inayotusaidia katika shughuli hii ndogo ya kuzungumza lugha ya Wahindi milioni 35. Ni kitendo cha heshima kwa utamaduni wao. Huduma kwa mawasiliano halisi. Njia ya kutembea pamoja. Hatua kwa hatua. Ni juhudi, hakika. Lakini kama methali ya Kannada inavyosema kuwa ಕೈ ಕೆಸರಾದರೆ ಬಾಯಿ ಮೊಸರು, yaani Juhudi hulipa kila wakati.”

Tornielli:Kuongeza lugha ya kikannada ni wito wa Huduma ya Askofu wa Roma

“Chaguo la kuongeza pia lugha ya Kikannada kwa zile 52 ambazo tayari zipo katika Radio Vatican - Vatican News ili kupeleka maneno ya Papa katika lugha mama ya mamilioni ya Wahindi inathibitisha wito wetu kama huduma kwa Askofu wa Roma na kwa Makanisa yanayounda Kanisa la Ulimwengu. Katika wakati wenye matatizo na mashaka, vita na ghasia, inafariji kwamba Kanisa linashuhudia ushirika na ushirikiano, likiimarisha uhusiano kati ya Roma na ulimwengu.” Alithibtisha yao pia Dk. Andrea Tornielli, mkurugenzi wa uhariri wa vyombo vya habari vya Vatican.

Menichetti:Wakristo wa Kanisa lililo hai

Na kwa upande wake Dk. Massimiliano Menichetti, Mhusika wa Radi Vatican , Vatican News alisisitiza kuwa “ “Pumzi ya Kanisa ni ya ajabu. Miaka 93 iliyopita Papa Pius XI alimuagiza Guglielmo Marconi kujenga Radio Vatican ili kupeleka matumaini kwa dunia, kueneza ujumbe wa Kikristo, kujenga Kanisa la Kristo.” Katika miaka ya 90, masafa ya Radio ya Papa yalifika Vietnam, na hivyo Tangazo hilo lilizalisha “Wakristo wa radio,” na Kanisa jipya lililo hai. Leo hii teknolojia mpya (masafa, satelaiti, intaneti) hutupatia fursa nyingi za kupeleka Habari Njema katika ulimwengu unaojeruhiwa mara nyingi. Lugha ya Kikannada ni mfano mwingine wa uhai na udugu na matumaini yetu ni kuendelea kusuka njia hizi katika uwajibikaji na umoja.”

 

02 April 2024, 16:46